Tatizo la ‘ Watendaji ‘ walioaminiwa na Rais Dkt. Magufuli huwa linaanzia kama hivi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,292
110,919
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametengua kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ya kuzuia wananchi wa Ilala kuabudu katikati ya wiki, ameamuru wananchi waendelee na ibada kwa kufuata utaratibu.

Chanzo: #MwananchiUpdates

Kuna Mtu Siku nyingi sana aliwahi kuniambia kuwa Wawili hawa japo huwa wanachekeana mbele ya ‘ Bosi ‘ wao lakini ukweli ni kwamba hawa ni Paka na Panya kwani kuna Mmoja wao hapo (namuhifadhi) ni Mtoto wa Mjini hasa halafu hata Chama anakijua vyema na alianza Kupikwa Siku nyingi akiwa bado Kijana kabisa huwa hamkubali Mwenzake ambaye Historia yake ndani ya Chama cha CCM imejaa ‘ Ushamba ‘ mwingi na yupo juu kwa ‘ Kubebwa ‘ tu lakini hakijui Chama kama mwenzie.

Na kama haitoshi pia hata hapa Juzi kati tena nikasikia jingine kuwa kuna Mmoja wao hapo (namuhifadhi) ametokea Kutomuamini na Kumchukia mwenzie hasa baada ya kujua kuwa huyo Mwenzie anamtengenezea ‘ Hujuma ‘ kwa Watendaji ambao kwa bahati nzuri wote Ofisi zao ziko ndani ya Jengo moja na kwamba Yeye na Wenzake wengine Wawili (ukiachana tu na Yule wa Kigamboni) hawampendi na wapo katika ‘ Mkakati ‘ wa Kumpigisha Shoti (Kumuhujumu) ili ‘ atumbuliwe ‘ na ‘ Mtumbuaji ‘ Mkuu.

Kazi ipo!
 
Back
Top Bottom