Mr's goole
Member
- Aug 30, 2011
- 17
- 8
Nipo kwenye ndoa miaka 2 hadi sasa sijawahi kushika ujauzito.
Nimepima vipimo vyote mie na mume wangu hatuna tatizo. Naenda mwezini kama kawaida. Sijawahi kutoa mimba wala kutumia njia yoyote kuzuia mimba. Nimekunywa dawa na kuonana na madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake naambiwa sina tatizo. Mume wangu naye hana tatzo.
Huyu ni mwanaume wangu aliyenitoa usichana na amenioa sijawahi kuwa na mwanaume mwingine. Sijawahi kuugua gonjwa lolote la gono. Nipo makini na vyakula ninavyokula.
Nisaidieni mwenzenu kwani nimechanganyikiwa. Sijui inmerogwa? Natamani niende kwa jadi ila naogopa. Tatizo hili ni nini?
WADAU WENGINE WENYE TATIZO HILI
Ndugu zangu wana JF. Mimi nimeolewa nina miaka 5 ya ndoa. Mwaka 2011 nilipata ujauzito, miez 3 nikawa namwaga maj meupe na mepes kama maji ya bomba, nilikua naenda hospkila baada ya cku 1 au kila cku mana hali ilizid kuwa mbaya, lakini host hawakuona tatizo, mgongo ukawa unauma mpaka nikawa siwezi kusimama, nilikaa na hiyo hali mpaka mimba ya miezi 6 nazunguka hosp na maombi.
Miez 6 na wk 2 nilimwaga dam nying sana nikakimbizwa miko tegeta wakakuta mtoto yuko vizur na dam haikukata mpaka wk 2 nikajifungua njit alifarik baada ya masaa 8, bas nilipumzka miez 6 nikiuguza kiuno mana hakikupona then nikapata ujauzto ukatoka miez 2, nikabeba tena ikatoka miezi 3, nikapumzka miez 8 nikabeba tena na kila nikipata ujauzto wiki moja tu nakuwa na hal ya kuwashwa, kuwaka moto kiuno kama uchungu uchungu damu huanza kudondoka mpaka mimba itoke. Mimb ya mwsho ilikua 2013 Nov. Ilivoanza dalili dokta akanipa duphastone had miez 5, miez 7 wk 2 nikaumwa nikapata oprtion alifarik pia.
HIVI SASA NINA MIEZ 8 YA OPERATION, TATZO NIN? NAWEZA BEBA TENA?
Nina rafiki yangu ambaye ana mwaka wa nne katika ndoa yao ana tatizo la kutoshika mimba. Wameshaenda hospitali nne tofauti na mumewe kuchekiwa na wameambiwa wote wawili hawana tatizo lolote. Nilipomuuliza je huwa wanafanya kwenye zile siku hatari alijibu ndio huwa wanafanya kwani kila mmojawao ana hamu na mtoto kwa muda huu na hajawahi kutoa mimba maishani mwake.
Tatizo kubwa linamsumbua huyu dada ni kuwa wanataka mtoto, pia mumewe na ameshamuambia mwaka huu ukiisha kama hajapata mimba ni lazima atatafuta mtoto nje ya ndoa ili aitwe baba.
Jamani naomba mumsaidie huyu rafiki yangu kwani hajui tatizo ni nini hadi hashiki mimba, yupo radhi hata kutumia tiba mbadala/ dawa ya asili itakayomsaidia kuweza kushika mimba haraka. Nakaribisha mawazo, ushauri n.k
Niko na mme wangu it's about 3 years now toka tuishi pamoja. Kila tukikutana na kushiriki on danger days naishia kubleed damu nyingi sana na maumivu makali. Tulienda hospitali tukapima zinaa zote bila mafanikio, but nkikaribia kubleed nahisi dalili zoote za ujauzito then tunaishia uzuni kwa kubleed damu rundo. One doctor alibaini mbegu za mme wangu kutokua na nguvu za kutosha kutungisha akatupa ushauri na vyakula vya kutumia but tatizo liko palepale.
Juzi dokta mwingine kasema nina shida mimi kwenye mfuko wa uzazi, akanipa dawa nkatumia na ziliisha last week.
Please madaktari, hebu tupeni ushauri ili Mungu atufungulie tupate mtoto. G'time
Poleni kwa mgomo unaogusa maisha yenu.
Asitokee mtu kuwalaumu kana kwamba hatumjui adui ni nani.
USHAURI/ MAONI YA WADAU
HOW TO GET PREGNANTSome women are blessed with fertility and get pregnant quickly and easily the old-fashioned way. For others, conceiving is not so simple. These step-by-step baby-making basics will help any woman understand when she is most fertile, how often and when to have sex and when to seek help for infertility.
- Ready for motherhood?
Difficulty:Moderately Easy[h=2]Instructions[/h]
Tips & Warnings
- 1 Find a partner. For some, this is the hardest part.
- 2 If you are currently on the pill as a form of birth control, discontinue taking it. Most doctors recommend that women wait three cycles while their bodies adjust to being off the pill before trying to conceive.
- 3 Start taking a prenatal vitamin before getting pregnant. Medical professionals recommend that women get a daily dose of 400 micrograms of folic acid starting at least a month before trying to get pregnant and at least 600 micrograms a day once pregnant. Research has indicated that doing so can reduce the risk of neural tube defects in babies by up to 70 percent.
- 4 Balance your hormones with good nutrition and herbal supplements. Zinc, calcium, magnesium and B6 are great for sustaining hormonal balance. Various herbs associated with balanced hormones include chamomile, raspberry leaf, ginkgo biloba, saw palmetto, ginseng, licorice root and black cohosh. Consult your doctor if you are unsure of the effects of any herbal supplements.
- 5 The best time to develop a healthy lifestyle is before pregnancy. Maintain a healthy weight, exercise regularly, eat healthy foods, reduce stress and don't smoke, consume alcohol or do any other recreational drugs. These good habits may help you get pregnant more easily and will certainly serve you and your baby well during pregnancy.
- 6 Determine when you ordinarily ovulate. For most women, this is in the middle of their menstrual cycle, around day 14, although the exact timing varies among women. There are a number of ways to determine when you are ovulating, from tracking your basal body temperature and watching for changes in cervical mucus to simply purchasing an ovulation calculator at the drug store.
- 7 Have regular, unprotected sex around the time you ovulate. Since sperm cells can survive in the reproductive tract for two to three days, it's best to have sex every day for at least a few days leading up to ovulation. So for example, if the average woman ovulates on day 14, it's best to have sex on days 12, 13 and 14 of her menstrual cycle.
- 8 On the first day of a missed period, take an early pregnancy test and find out if all of your hard work has paid off.
- 9 Repeat these steps each month until you are pregnant.
If you are concerned about any existing health issues or unhealthy habits that you or your partner may have, consider preconception planning. Your doctor can assess your overall health and help you identify lifestyle changes that may improve your chances for a healthy pregnancy.
A healthy couple without any known fertility problems only has a 25 percent chance of conceiving during any given cycle. So if it's taking a while to get pregnant, be patient. Medical professionals define infertility as the inability to get pregnant after 12 consecutive cycles of trying.
Infertility affects both men and women but treatment is available. Depending on the source of the problem, your gynecologist, your partner's urologist, a family doctor or a fertility specialist may be able to help. Nowadays, there are many options for infertile couples trying to conceive, including infertility drugs, artificial insemination, in vitro fertilization (IVF) and other assisted reproductive technologies.
Avoid taking synthetic horomones, anti-depressants and other drugs leading up to getting pregnant. Chemicals can alter your body's natural hormonal state and make pregnancy more difficult.
The odds of conceiving each month decrease as you get older.
NJIA ASILI YA KUONDOKANA NA UGUMBA (INFERTILITY)
Asali inaaminika kuamsha nyege na wapenzi wa jinsia zote mbili wanashauriwa kunywa angalau vijiko viwili {vya mezani} kila siku kabla ya muda wa kulala {usiku}.
Mdalasini umetumika kwa muda mrefu kwenye dawa za kihindi na kichina ili kuongeza uwezo wa uzazi ka kina mama wenye kuhitaji kuzaa.
Kiungo hiki {mdalasini} huchanganywa na kiasi cha asali na kufanya mgando {paste} ambao hupakwa kwenye fizi za meno na kunyonywa na kuingia mwilini taratibu.
Familia moja iliyokuwa haina watoto iltumia mgando huu kwa mafanikio na kupata mapacha wa kike baada ya kushindwa kwa muda wa miaka 14 kupata mtoto. Walikuwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto hadi waliposikia kuhusu mchanganyiko huu wa asali na mdalasini.
ONDOA HOFU KWANZAHakuna sababu ya kuwa na hofu kwa muda huu wa miezi 3 kwa sababu tafiti zinaonesha kuwa kwa watu wasio na matatizo ya uzazi , na ambao wanafanya tendo la ndoa bila ya kinga kawaida ushikaji mimba ni kama ifuatavyo;
50% hupata mimba ndani ya miezi mitatu ya mwanzo
22% hupata mimba baada ya miezi 6
13% hupata mimba ndani ya miezi 12
15% waweza wapate mimba baada ya mwaka moja hadi miwili.
Ushauri wangu ni kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwa wakatu huu unless unataka kujiondoa wasiwasi kwa vipimo, kwa kwasababu hata madaktari hutafsiri mtu mwenye matatizo ya uzazi ni yule aliyekaa na mwenza kwa miaka isiyopungua miwili wakijamiana kwa uchache mara tatu kwa wiki bila ya kinga.
NJIA HII HUENDA NI SULUHU INGAWA YA AJABUNinachojaribu kusema hapa siyo kuwashawishi wanawake wasioshika mimba kunywa pombe, ili waweze kupata mimba, hapana. Maana najua wahafidhina watanitia vidole vya macho. Ninachotaka kusema ni kwamba, huenda pombe hufanya mambo fulani yenye kuweza kuchochea upatikanaji wa mimba kwa haraka.
Kama ukichukua wanawake na kuwaambia kila mmoja apange kupata ujauzito kwa kipindi cha miezi miwili ijayo, tegemea kuona karibu wanane kati ya kila kumi kati ya watakaopata mimba, kuwa ni wale ambao wanakunywa pombe, angalau kwa kiwango cha chupa zisizozidi mbili kutwa. Halafu mmoja katika kumi atakuwa ni yule asiyekunywa pombe.
Wale wanaokunywa sana pombe kwa kiwango cha zaidi ya chupa tatu kwa siku hawa itawalazimu wasubiri kwa mwaka mzima kabla hawajapata mimba. Ni vigumu kwao kuamua kupata mimba na wakaipata kwa muda mfupi. Watafiti wanasema, kiwango cha wastani cha pombe huwachosha wanawake kushiriki zaidi kwenye tendo la ndoa, hivyo yamkini ya kupata ujauzito huongezeka sana.
Kama wanakunywa wastani wa bia mbili, wanakuwa kwenye nafasi ya kuhitaji kufanya tendo la kujamiiana kila baada ya siku moja, wakati wale wasiokunywa wanaweza kukaa wiki nzima bila kujisikia kujamiiana hasa kama mambo yanayowasonga ni mengi. Kupata mimba pia kunahitaji utulivu wa mawazo kwa kiasi fulani. Mwanamke akishakunywa bia mbili kwa mfano, mawazo yake huweza kutulia, hata kama ni kwa muda. Hapo uwezekano wa mimba nao huongezeka.
Dk. Peter Bowen, yeye anasema, kama mwanamke ni mnywaji pombe na anahitaji mimba, inabidi kila jioni anywe glasi moja ya ya mvinyo (wine) kabla hajaenda kulala. Anazungumzia mwanamke mwenye mume au mpenzi na mbaye mumewe yuko tayari kukutana naye kila anapohitaji. Vinginevyo mvinyo huo unaweza kuwa kero kwake. Dk. Bowen anasema, kusongeka kimawazo huwa kunawafanya wanawake wengi kushindwa kupata ujauzito. Hivyo kupata kitulizo cha mawazo cha muda mfupi kunaweza kusaidia.
View attachment 57995
Wakati mwingine inawezekana:-
1. High sperm DNA damage
One prominent cause is high sperm DNA damage. Fortunately, there are available medical examinations that can detect this kind of disorder. The test results will return a percentage of damaged sperms: a result below 15% is considered normal, while results higher than 25% mean that there is a lower chance of successful conception even with infertility treatments.
2. Follicle or fallopian tube problems
On the other hand, there can be other reproductive system malfunctions that cause infertility, but cannot be detected by the above-mentioned set of standard tests. One such abnormality occurs when the fallopian tubes cannot receive the matured egg successfully, therefore the egg never meets the sperm. There is a chance that the woman produces deformed eggs, or that the follicles do not rupture properly to release the matured egg. It remains trapped inside the follicle (Luteinized Unruptured Follicle).
3. Immunological factors (hii ni muhimu aijue)
There are certain immunological factors to be taken into account, such as sometimes the body of the woman may misinterpret the sperms to be hostile organisms, and might kill them, or immobilize them.
4. Infections
Sometimes infections are responsible for infertility, that don’t show up in clinical examinations, but are nevertheless present in the patient’s system, which is why some doctors use antibiotics during therapy.
5. Sperm problems
The problem can be with the man’s sperms: occasionally it is too weak to penetrate the egg. This possibility can be easily excluded by performing a donor test. If the donor’s sperm is able to penetrate the woman’s egg, then the problem is definitely with the man’s sperm. Even the uterine lining can have hardly detectable abnormalities which do not allow the egg to implant. But with multiple vaginal ultrasound tests this problem can be detected. If the uterine lining is too thin, the root cause may be related to smoking, which can prevent blood flow to the uterus.
PIA, SOMA:
SABABU ZA MWANAMKE KUSHINDWA KUPATA UJAUZITO
Moja ya matatizo yaliyoko katika jamii zetu na yamesababisha wanandoa wengi au wanawake wengi kukosa furaha, ni kukosa uwezo wa kupata ujauzito kwa mwanamke. Sote tunafahamu kuwa, swala la mwanamke kupata ujauzito linahusisha pande zote mbili, yaani upande wa mwanamke na pia upande wa mwanamme, wote wawili wanapokuwa katika afya nzuri ndipo ujauzito unaweza kupatikana kwa mwanamke.
Miongoni mwa sababu zinazoweza kumfanya mwanamke ashindwe kupata ujauzito ni kama zifuatazo:
Matatizo katika homoni, hii ni kutokana na kwamba, mzunguko (Menstrual cycle) katika mwili wa mwanamke hutawaliwa na hizi kemikali asilia ndani ya mwili ambapo mabadiliko madogo yakitokea katika uzalishaji wa hizi homoni au homoni kuzalishwa katika wakati ambao siyo muafaka huweza kupelekea mwanamke akashindwa kupata ujauzito, pia tatizo la kuwa na uzito wa mwili mdogo sana au mkubwa sana pia huathiri hali nzima ya homoni na kupelekea kushindwa kupata ujauzito.
Umri, kwa wanawake uwezo wa kupata ujauzito unapungua kwa kadri umri unavyoongezeka, hii inatokana na kupungua kwa uzalishaji wa homoni husika wakati umri unavyoongezeka. Kuanzia miaka 35 na kuendelea huwa kunakuwa na tatizo la kushindwa kupata ujauzito kwa wanawake wengi.
Kuziba kwa mirija (fallopian tubes), hii husababisha mbegu za kiume (sperms) zishindwe kulifikia yai na kulirutubisha ili ujauzito utokee. Kuziba kwa mirija huweza kusababishwa na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana, matatizo katika kizazi au upasuaji. Mara nyingi wanawake ambao mirija yao imeziba, hawahisi dalili zozote.
Ute ute katika kizazi (mucus problems), ute unaopatikana katika kizazi cha mwanamke huwa na sifa ya kuruhusu mbegu za kiume ziweze kusafiri kwa urahisi na kulifikia yai ili kulirutubisha. Kwa baadhi ya wanawake ute huu unakuwa na uzito na kemikali ambazo ni vigumu kwa mbegu za kiume kuweza kupita, na wakati mwingine mwili wa mwanamke huzalisha sumu ambazo huziua mbegu za kiume, haya yote husababisha kukutana kwa yai na mbegu za kiume kusitokee na hivyo ujauzito kutopatikana.
Uvimbe katika kizazi (fibroids), hii huchangia asilimia tatu (3%) katika mwanamke kutopata ujauzito. Uvimbe huu ambao hutokea katika kuta za mji wa mimba, kwa namna moja au nyingine huweza kuzuia yai lililorutubishwa lisikae sehemu yake na hivyo kuathiri kizazi.
Matibabu ya kansa, kwa kutegemeana na aina ya matibabu, aina ya dawa au njia ya mionzi, hizi huweza kumuathiri mwanamke na kumsababishia kushindwa kupata ujauzito.
Ukomavu katika kizazi, kwa baadhi ya wanawake wanayo matatizo ambayo kizazi chao huwa hakijakomaa vizuri au katika kuzaliwa kwao walizaliwa na tatizo hili ambalo, kizazi hakiko sawa (abnormally developed uterus).
Asilimia kubwa ya matatizo ya mwanamke kushindwa kupata ujauzito yanayo tiba, kama unalo tatizo katika kupata ujauzito usikate tamaa, onana na wataalamu wa afya ili uweze kujua chanzo cha tatizo lako na kupatiwa msaada unaostahili.
Chanzo: tanzlife.co.tz