Tatizo la umeme Arusha imekuwa kero

Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,219
370
Wana JF na wananchi wote,

Hapa Arusha kumekuwa na tatizo la umeme tokea mwaka jana 2015 esp tokea kipindi cha kampeni mpaka sasa Umeme umekuwa shida na wala hakuna maelezo yoyote au taarifa yoyote kutoka Office za TANESCO Mkoa au Makao makuu Dar kutujurisha kinachoendelea na kwanini umeme unakatika mara kwa mara na bira taarifa yoyote kwa UMMA, kama juzi na jana umeme unakatika hovyo hovyo tu.

Last December 2015 nilikuwa Dar sikukutana na tatizo kama nililokutana nalo Arusha.Mfano usiku wa kuamkia leo umeme ilikuwa kata rudi kata rudi khaaaaa.

TANESCO ARUSHA MTUPE TAARIFA KAMILI KULIKONI TATIZO HILI LITAISHA LINI HAPA ARUSHA MJINI
 
Ni kweli kbsa.hili tatizo ss kwa Arusha limezd.Tanesco tunaomba mje mtoe maelezo hapa
 
Nimekaa Arusha nikawa naziona siku zinarudi nyuma badala ya kwenda mbele, yaani ile mitaa niliyokaa ( Majengo ya juu) kila kitu ni shigda,kuanzia umeme,maji, bei ya vitu iko juu, uchafu, vijana wala mirungi na bhangi kibao na nyumba za udongo kibao na pesa ni ngumu mno kupatikana. Yaani kuishi Arusha ni kujitoa ufahamu ndio uweze kuishi na aliyeweza kuishi Arusha hashindwi maisha sehemu yoyote Arusha ni zaidi ya jela.
 
Ndio Arusha sasa Uijuavyo alafu wanasema ni Giniva ya Africa usipime ni kweli ujito ufahamu kuishi arusha maana ni magumu watu hawataki kukubali mji upanuke wana razimishia kubanana hapo hapo mjini alfu mbaya zaidi mji hauko wel planned kabisaaaa viwanja kupimwa kwanza ni shidaaaaa
 
Umeme arusha ni tatizo la kudumu inavyoelekea tanesco wanaona ufahari hali ilivyo ndo maana hawachukui hatua za kukabiliana na hili suala.
 
Ndio Arusha sasa Uijuavyo alafu wanasema ni Giniva ya Africa usipime ni kweli ujito ufahamu kuishi arusha maana ni magumu watu hawataki kukubali mji upanuke wana razimishia kubanana hapo hapo mjini alfu mbaya zaidi mji hauko wel planned kabisaaaa viwanja kupimwa kwanza ni shidaaaaa
Arusha kuwa Geneva ya Afrika ni kwa wale wanaoishia pale mjini ( maana kwa pale mjini si haba hasa kama umetokea kule Babati,Monduli au kule Longido) hawajaingia huko vichochoroni tena vile vichochoro vya Ngarenaro ndio watakaosema kiusahihi kama kweli Arusha inastahili kuwa GENEVA ya Afrika au la, sifa kubwa ninayoikubali bila kificho kuwa lile ni jiji la kitalii na watalii ni wengi mno na hali ya hewa safi sana.
 
haaaa jaman samsun.
we ndo ulienda kukaa na watu wa dizain hyo.na haimaanish arusha yote ndo tunamaisha hayo
 
Arusha ni sehemu nzuri sana ya kuishi, ndio huwezi kupata hela bila kufanya kazi kama unategemea uje Arusha uishi kama mission town umekwisha. Mie nilivyokuwa nasikia Dar nikafikiri bonge la jiji loh! hapafai vilevile hali ya hewa chafu, maji ya bomba shida, nyumba asilimia 90 hazijamaliziwa ujenzi matofali nje nje no finishing, maji taka kila sehemu ya jiji, kuona kinyesi kwenye lami ni kawaida kabisa, kifupi Dar ni shida kuishi kuliko mkoa wa Arusha, labada kwa kuwa wauza unga ni wengi na mapunda ni wengi ndio wanao isifia Dar.
 
Arusha na hisi kunakubaguliwa sio bure .mikoa mingine angalau naona wanatangaziwa kukatwa umeme lakini Arusha nikama tunaonyeshwe hakuna tutakapo kwenda Kulalamika tupatiwe msaada.navile tena Waziri Wa nishati ana bifuu na mtu Wa kazikazini Mengi.ndio kabisa atutegemei ataa zile zziara za ghafla za hapa kazi tuu.
 
Alafu cha ajabu Arusha meneja Tanesco nikama anakimbia ofisi mwezi Wa tatu sasa uwezi mkuta ofisini.kila ukifika kuulizia unaambiwa yuko field Mara semina dar Mara Sijui nini .ni ili mradi tuu apatikani
 
Niko kijenge tangu nihamie huku mwaka Jana kwel huku umeme n shida,ajabu mitaa ya ushuani nayoshinda hapa a town umeme haukatwi hovyo kama mitaa ya uswaz huku arachuga n makusud tu ya tanesco navyoweza kusema
 
Arusha kama unategemea kuishi kijanja janja,lazima maisha yakupige.Panda hiace za asubui uone wamama wanavyojituma na mikapu mikubwa wakauze mboga.Wababa wanaojitambua maisha yanasonga tu,pamoja na hujuma za makusudi za Tanesco ambazo zimesabisha maisha kuwa magumu,lakini Arusha bado ni sehemu salama na pazuri kuishi
 
Na mwanza napo umeme ni shiiida,hauwezi pita siku umeme umekatika,na ukikatika kurudi ni masaa ya kutosha
 
tatizo la umeme hapa Arusha lilianza mwezi. wa sita mwaka jana kwa kweli tinapata shida sana
 
Wana JF na wananchi wote,

Hapa Arusha kumekuwa na tatizo la umeme tokea mwaka jana 2015 esp tokea kipindi cha kampeni mpaka sasa Umeme umekuwa shida na wala hakuna maelezo yoyote au taarifa yoyote kutoka Office za TANESCO Mkoa au Makao makuu Dar kutujurisha kinachoendelea na kwanini umeme unakatika mara kwa mara na bira taarifa yoyote kwa UMMA, kama juzi na jana umeme unakatika hovyo hovyo tu.

Last December 2015 nilikuwa Dar sikukutana na tatizo kama nililokutana nalo Arusha.Mfano usiku wa kuamkia leo umeme ilikuwa kata rudi kata rudi khaaaaa.

TANESCO ARUSHA MTUPE TAARIFA KAMILI KULIKONI TATIZO HILI LITAISHA LINI HAPA ARUSHA MJINI
Nani aliwadanganya kuchagua machadema!?!

Hiyo ndio faida ya kuchagua chama cha wanafiki
 
Hapa mmekuja kuleta uzuri wa majiji au kuelezea kero za umeme.!? umeme ni kero arusha na hakuna maelezo yoyote ya maana, huyu meneja sijui anasubiri nini asijitumbue mwenyewe, kuna hizi mita za luku za juu ya nguzo ni shida kinyama, nimeomba nibadilishiwe hata kwa gharama nyingine wanasema hawana mita lakini kuna waliobadilishiwa, Tanesco Arusha ni jipu linalohitaji kutumbuliwa haraka sana..!!
 
Tatizo la umeme limekuwa sugu hapa arusha . Watu wamekata tamaa wengi wao wanatumia solar au M power kwa sbb umeme Umekuwa kero sana .
 
Back
Top Bottom