Kuna kitu ambacho huwa kinanishangaza sana. Hospitali na vituo vya afya vingi havina dawa, ukienda hospitali daktari anakuandikia dawa lakini ukienda dirishani dawa hakuna. kuna wakati daktari anaweza kukuambia nenda duka fulani kanunue dawa sisi tunalaumu na inawezekana hilo duka si la kwake ila kafanya uungwana usihangaike kutembea maduka mengi.Sasa hapa kosa ni la nani, Serikali ambayo haijapeleka dawa au daktari?.katika kitu ambacho serikali hakikisemi ni pale wanapoambiwa dawa hakuna mahospitalini ambacho mimi nafikiri ingekuwa ni kitu cha kwanza mawaziri husika kufuatilia lakini wakisikia kuna kosa kafanya daktari wanawaka sana.