Tatizo la tumbo kujaa gesi na kupelekea mara kwa mara kutoa hewa chafu linahatarisha ndoa yangu

Mojojo

Member
Jun 7, 2017
39
39
Waungwana naomba ushauri wenu katika hili tatizo hili limekuwa sugu kwangu huwa natumia dawa za kupunguza gesi lakini zikiisha tatizo linaendelea

Mwenzi wangu kwa maana ya mke kanivumilia kwa kipindi chote lakini sasa anasema nisipo tafuta utatumizi wa hili swala anaachana nami

Njia pekee inayo nipunguzia maumivu ya tumbo kujaa gesi na kunifanya nijihis na ahueni ni hii ya kupumua yaan kujamba

Nishauri ndugu zangu nifanye nini ili niondokane na hili tatizo lakini pia ni inusuru ndoa yangu
 
Jamba tu mkuu.
Angalia pia aina ya vyakula unavyokula. Kunywa maji ya kutosha.
Muone daktari kwa ushauri.
Kama shemeji akikuacha, kuna warembo wengi humu watakaba nafasi.
 
Waungwana naomba ushauri wenu katika hili tatizo hili limekuwa sugu kwangu huwa natumia dawa za kupunguza gesi lakini zikiisha tatizo linaendelea

Mwenzi wangu kwa maana ya mke kanivumilia kwa kipindi chote lakini sasa anasema nisipo tafuta utatumizi wa hili swala anaachana nami

Njia pekee inayo nipunguzia maumivu ya tumbo kujaa gesi na kunifanya nijihis na ahueni ni hii ya kupumua yaan kujamba

Nishauri ndugu zangu nifanye nini ili niondokane na hili tatizo lakini pia ni inusuru ndoa yangu

Ulishaenda hospital aisee ukapma ?
 
amiba walio kubuhu
vidonda vya tumbo hivyo kupelekea mmeng'enyo kuwa wa hovyo.

tatizo likizidi hata performance wakati wa tendo la ndoa itapungua.

cha msingi kapate vipimo upate tiba sahihi
 
Nilienda Hospatal nikakutwa na hyprol nikapewa mabox ya vidonge vya mwezi mzima nikanywa nikamaliza hali ikawa imetulia kidogo na masharti mengi kweli ya vyakula vya kutumia lakin baada ya muda hali ikajirudia lakn safari hii hyporol sikuwa nae ni hali ya tumbo jaa gesi tuu hivyo na tumia dawa za ges ikiwapo tuu sema zikiisha hali inarudi vile vile

Kuna mtu kaniambia mlongelonge ni dawa pia ya hili tatizo ni kweli wa ndugu ni utafute
 
Mkuu pole sana asee ina maana unajamba tu hovyo hadi imekuwa kero kwa mwenzi wako???Itakuwa ni kero kweli aseee.Jaribu kuepukana na aina ya vyakula vya protini hasa nyama,maziwa na maharagwe.Badala yake ule matunda kwa wingi na mboga mboga.Pia fanya mazoezi ya kutosha kuwezesha uyeyushaji mzur wa chakula na pia kunywa maji mengi zaidi.
IKISHINDIKANA WAAMBIE WATU WANAOHUSIKA NA UWEKEZAZI WA GESI WAJE KUCHIMBA.
 
Mkuu mara ya mwisho kunywa dawa ya minyoo ni lini??
Maana unaweza ukawa unakula vzuri lakini choo unapata kidogo sababu ya hao minyoo tumboni na pia kusababisha tumbo kujaa gesi na kutoa hewa yenye harufu mbaya pindi unapopumua.
Nashauri kama hujatumia dawa ya minyoo jitahidi sana utumie mapema.
 
Mkuu pole sana asee ina maana unajamba tu hovyo hadi imekuwa kero kwa mwenzi wako???Itakuwa ni kero kweli aseee.Jaribu kuepukana na aina ya vyakula vya protini hasa nyama,maziwa na maharagwe.Badala yake ule matunda kwa wingi na mboga mboga.Pia fanya mazoezi ya kutosha kuwezesha uyeyushaji mzur wa chakula na pia kunywa maji mengi zaidi.
IKISHINDIKANA WAAMBIE WATU WANAOHUSIKA NA UWEKEZAZI WA GESI WAJE KUCHIMBA.
Ha ha ha we jamaa hatar wawekezaji tena..
 
Kamahajaupenda mpakaushuzihajakupenda huyo bado.

Inatakiwa umchengue mpaka aseme "baby huo si ushuzi,hiyo ni perfume natural"
 
Huyo mke wako mkuu ana nongwa,.kama vp mtafunie karanga mbichi na dagaa wa mwanza yaani ukijamba kama kafa panya.
 
Kanunue dawa moja ya edmark inaitwa shake off utakuja kuniambia inatoa uchafu wpte tumbo linakuwa safi hutopata kujamba ovyo utaharisha hasa watakupa maelekezo namna ya kutumia kisha njoo utupe marejesho
 
Waungwana naomba ushauri wenu katika hili tatizo hili limekuwa sugu kwangu huwa natumia dawa za kupunguza gesi lakini zikiisha tatizo linaendelea

Mwenzi wangu kwa maana ya mke kanivumilia kwa kipindi chote lakini sasa anasema nisipo tafuta utatumizi wa hili swala anaachana nami

Njia pekee inayo nipunguzia maumivu ya tumbo kujaa gesi na kunifanya nijihis na ahueni ni hii ya kupumua yaan kujamba

Nishauri ndugu zangu nifanye nini ili niondokane na hili tatizo lakini pia ni inusuru ndoa yangu
Yaani ushuzi umfanye mke akuache? Anakutafutia visa, mwahi yeye...
 
Back
Top Bottom