Nimefikiria sana kabla ya kuandika singa hii, kwa vile wengi wameshaandika juu ya maudhui. Lakini, kama mfuatiaji wa karibu wa yale yanayoendelea Burkina Fasso, wivu, uchungu na tafrani vimenifanya nilirejee suala hili kwamba, siye Tanzania kitu gani kinafanya nchi yetu izorote?
Ni miaka kadhaa tu iliyopita Rwanda ilikuwa 'a basket case'.
Wanyarwanda walikuwa wakitaka kuona picha inayolingana na nchi iliyoendelea walikuwa wanakuja Tanzania.
Leo hii ni sisi ndiyo tunakwenda Rwanda kujionea maendeleo. Yaani maendeleo ya miaka yetu 64 ya Uhuru yanashindwa na maendeleo ya miaka 30 tu iliyopita, ingawaje tuna rasilimali mara 10 ya Rwanda!
Suala hilo hilo linajikariri tena Burkina Fasso. Miaka minne tu tangu kuja Captn Ibrahim Traore, sisemi BF imekwishatupita, lakini wanaelekea huko, na kwa kweli tayari kuna mambo mengi wameshatupita. Hebu angalia, Burkina Fasso nchi tunayoishinda karibuni kwa kila rasilimali, katika miaka hiyo minne~
1- wameanzisha mkakati wa kujenga wenyewe kilomita 5,000 za barabara za lami kila mwaka (wamekwishakamilisha awamu ya kwanza). Yaani wameweza kuwa train vijana wao, wakanunua zana zote zinazohitajika katika ujenzi wa barabara mpaka za juu kwa juu- angalia picha uone kinyemi! Sisi twamngoja Mchina atujengee kilomita mia kwa mwaka, ili tupate 10 percent!
2- Na hii imeniuma sana! Burkina Fasso inajenga mtambo wa nuklia wa kufua umeme utakaofunguliwa 2030. Mtambo huo utatosheleza nchi na kuuza kwa nchi jirani. Burkina Fasso haina Uranium. Siyo hivyo tu, katika clause ya mkataba wamewaambia Warusi lazima waache maarifa ya ufundi wa kujenga mtambo kama huo, kwa Waburkinabe wenyewe ili hapo baadaye wajenge wenyewe kwa usimamizi mdogo tu! Sisi tunayo Uranium lakini hadi sasa twafikiria kuichimba na kuiuza tupate hela! Nadhani bado wako katika 'mchakato wa kufikiria' kama wajenge mtambo wa nuklia wa kufua umeme!
3- Elimu bure hadi Chuo Kikuu. Ni katika miaka hiyo minne tu. Hivi sasa ujenzi wa vyuo vikuu 20 unaendelea, vingi vya ufundi, licha ya mamia ya Msingi na Sekondari. Kumbuka nchi hii haituzidi kwa lolote.
4- Tangu kufika Traore hadi mwaka 2025 Burkina Fasso imefikia daraja la kwanza Afrika kwa kuzalisha pamba! Ilikuwa ya tisa. Si kilimo tu. Wanachambua na kutengeneza nguo wenyewe. Marufuku Wanajeshi, Wanafunzi na Wanasiasa kuvaa nguo zilizotengenezwa kutoka nje(nadhani wana exemption kwa Mabalozi na safari za nje)! Hii ni ili kuwapa wenye viowanda wa ndani soko la uhakika, na pia ukitumia kitu chako ndiyo unawakinaisha wengine kuwa ni bora.
5- Bima kwa wazee wote kuanzia 60+ . Si hivyo tu, wazee wanafanyiwa upimaji wa afya kila mwaka, bure!
6- Burkina Fasso ina kiwanda kikubwa Afrika Magharibi cha kuchakata tomato. Inauza tomato za mikebe si kwa nchi jirani tu kama Ghana na Ivory Coast, bali hadi Italy!
7- Hivi karibuni wamefungua kiwanda kikubwa cha kuzalisha maziwa ya unga (nadhani watatuuzia hata sisi)!
Sitaendela maana kama nilivyosema, hushikwa na uchungu, wivu, fihi na tafrani.
Swali la kwa nini Tanzania (baaadhi ya vitu hivi tulikuwa navyo vikafa) haiwi hivyo?
Nitajibu lakini sitasema sababu zote, hivyo changieni.
Kwangu sababu kubwa ni kuwa hatuna viongozi wenye maono na walio tayari kuweka maslahi ya nchi mbele. Viongozi wawili tu Tanzania ndiyo nadhani kwa mbaali walikuwa angalau na maono fulani> Mkapa na Magufuli (pamoja na shortcomings zake).
Pili- Na hii naitaja kwa vile wengi hawataitaja: serikali zetu zote zilizopita, ukitoa ya Nyerere, ni serikali za ki 'mercantile' yaani za kufanya biashara, Wao huwaona Wananchi ni wateja wa kufanyiwa biashara, Ndiyo maana serikali za Tanzania hazina msaada wowote kwa Wananchi. Na wakifanya kitu ni kwa kukiuza si huduma! Angalia 'bei' za matibabu, mikopo, na kila kitu wanachokiingiza, watataka faida mara 100! Serikali imeachia kila kitu kwa soko liamue.
Hayo niliyoyasema juu ya Traore ni serikali inajenga, inaleta zana za kilimo, za kutengeneza barabara.... mara nyingi inawapa bure wananchi wake, na ikipasa kuwauzia, huwa wanawachaji pesakidogo yaani wana subsidize, au kwa kuwakopesha kwa muda mrefu bila riba. Hiyo ndiyo serikali inayojali ustawi wa raia. Kwa kufanya hivyo, raia wanakuwa na imani zaidi na serikali yao.
Hadi sasa majaribio 43 ya Mabeberu kumpindua Traore yamefeli na raia ndio waliofelisha kwa sababu wanaona wana maslahi kutoka serikalini kwao. Thubuuutuuu Tanzania!