Wama Jukwaa naombeni msaada
Panya wamevamia nyumba yangu mwezi wa tano huu. Nimejaribu sana kupambana nao kwa namna zote imeshindikana kabisa. Mwanzoni nilijaribu kuwauwa kwa sumu. Kwa hakika walikufa sana. Nyumba ikawa kimya kabisa. Waliporudi mara hii, sumu hata ukiweka nyama hawaikaribii. Wanapita mbali kabisa. NImejaribu gundi ya panya. Mwanzoni walinasa kadhaa na kufa. Lakini sasa hivi nikiweka njia zao ama hawapita au wanaruka!
Ni tatizo kubwa sana. Nawaomba wajuzi wa kupambana na panya wanisaidie.
Natanguliza shukrani sana
Panya huwa hawahitaji hasira mzee. Uliwachukia ukaamua kuwapa sumu kali ili wafe. Lakini huwa hawafi wote kinamna hiyo.
Kwanza ufahamu kuwa ukitaka kuwacontrol wasije kwako, lazima na majirani zako wafanye hivyo hivyo. vinginevyo ukiwaua ndani ya nyumba yako, wale wa jirani wanachukulia nyumba yako kama hilo ni jimbo huru, wanajimuvuzisha na kuanzisha makao.
Pili ufahamu kuwa panya ana akili kuliko kuku na ana kumbukumbu inayokaa muda wa karibu miezi 6. Na huwa anatilia mashaka kitu chochote kipya kwenye eneo lake. Hivyo ukimwekea mtego mpya leo, anaweza akaushit kwanza mpaka auzoee.
Ukiwapa sumu kali inayoua haraka, si wote watakula ile sumu. Na watakapokufa, waliobaki watakumbuka muda mrefu kuwa hiyo kitu siyo ya kugusa. Ndio maana mtego au sumu za namna hiyo zinafanikiwa mwanzo halafu baadaye hamna kitu.
Dawa inayofaa ni ile inayoua taratibu (chronic poisoning). Leo wanakula, hawafi, kesho wanakula tena hivyo hivyo, baada ya siku kadhaa wanaanza kufa. Na hapo hawawezi kukumbuka chakula gani ndio kimewaua kwa vile wanakula na kuchanganya na vingine. Utawazoa mpaka utafurahia.
Dawa ya namna hiyo inatakiwa iambatane na juhudi zingine kama vile usafi wa jumla, kuziba maeneo wanakofichama, pamoja na ufugaji wa paka. Pia kama unaweza kula (
kanyafu nkanwa) nayo inasaidia kuwapunguza (
Don't take this seriously, It is just a joke).
Sumu inayoua taratibu, inapatikana katika kitengo cha utafiti wa mapanya (wizara ya kilimo) pale morogoro, njia ya kwenda Mzinga karibu na lango kuu la kuingilia SUA. Wameichanganya kwenye tambi za rangi ambayo ndege hawaipendi kwa hiyo usiwe na wasi wasi kama wewe ni mfugaji.