Tatizo la ombaomba jijini Dar

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Nchi yetu ya Tanzania inavutia kwa kila hali. Ukiwepo mlima mkubwa kuliko yote Barani Afrika. Misitu na Mbuga nzuri za wanyama ni kivutio kizuri sana cha utalii. Tatizo lililopo hapa nchini ni hili suala la ombaomba ambao wanaharibu sifa nzuri ya nchi hii.

Nimeona mara nyingi watalii wakitembea katika miji ya Arusha na Dar wakijiandaa kwenda kutembelea Mbuga zetu za wanyama na kupanda mlima Kilimanjaro. Wawapo mjini wanakumbana na kundi la ombaomba ambao kila hatua wanayopiga ombaomba waliotapakaa kila kona ya miji hiyo hawaachi kuwaganda watalii hao wakiwaomba chochote. Ombaomaba hao huwa na kundi la watoto wadogo ambao ni kama siafu. Mimi binafsi huwa ninaona ni kero kwani watalii wengine hudiriki kuwapiga picha. Nadhani ni nia ya kutaka kwenda kuonyesha makwao kero wazipatapo wajapo nchini kwa mapumziko na kujionea vivutio vilivopo Tanzania.

Ninadhani muda umefika kwa nchi yetu kulivalia suala hili njuga na kulimaliza ili lisiendelee kuiletea aibu nchi yetu.
 
Back
Top Bottom