Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Mafuta ya kuku ni kiboko ya magonjwa ya sikio!
Nakumbuka nilipokuwa mdogo nilisumbuliwa sana na sikio lakini mama alinitibu na mafuta ya kuku na mara alipoyamimina tu sikioni,hata kama linauma vipi,linaanza kutulia kabisa.Hakukuwa na pharmacy na wala zahanati haikuwa na dawa za sikio.
 
Habari wapendwa!
Naombeni msaada huwa napatwa tatizo la kuwashwa washwa maskioni ndani.
Je, ni nini kisababisho?
Je, nitaondoaje hilo tatizo?
KARIBUNI!
 
Una tabia ya kuingiza vitu sikioni? Kwa mfano ear buds, funguo n.k.?

Kuwashwa kwa sikio kunaweza kusababishwa na mambo kadhaa, ikiwemo bacterial infection au fungus.

Tafadhali nenda ukamwone mtaalamu wa masiko akague masikio yako na bila shaka tatizo lako litatatuliwa.
 
Una tabia ya kuingiza vitu sikioni? Kwa mfano ear buds, funguo n.k.?

Kuwashwa kwa sikio kunaweza kusababishwa na mambo kadhaa, ikiwemo bacterial infection au fungus.

Tafadhali nenda ukamwone mtaalamu wa masiko akague masikio yako na bila shaka tatizo lako litatatuliwa.
Asante mkuu
 
Una tabia ya kuingiza vitu sikioni? Kwa mfano ear buds, funguo n.k.?

Kuwashwa kwa sikio kunaweza kusababishwa na mambo kadhaa, ikiwemo bacterial infection au fungus.

Tafadhali nenda ukamwone mtaalamu wa masiko akague masikio yako na bila shaka tatizo lako litatatuliwa.
Kweli huwa nikiwashwa napitisha cotton buds hata funguo.
 
H
habari ,

Nna matatizo na sikio langu la kushoto tangu nipo mdg, niipima n kupewa "hearing aid" bt nkashndwa kuitumia kwa mda mrefu maana nilkua naskia saut kuubwaa ad kichwa kinauma,,, so nkaamua kuvaa darasan af nikitoka navua.

Tatizo langu ss lmezd kdg,yan sikio la kulia pia lnauma istoshe nackia saut za ""zyiiiiiiiiiiiiii"" , nijuavo mimi ,hii hali ya kupata hii saut maskion huitwa TITTUNIS .Mnisadie ni vip naeza kupona hii hali n pia ka kuna uwezekano wa kupata matibabu ili nipone n kuweza kusikia vzr kama wenzangu.
Habari Je Umefanikiwa tiba. Nina mdogo wangu anatatizo kama Lako Naomba kujua Kama Umefanikiwa utujuze twende wapi my namba 0786855280
 
Mimi pia ninatatizo hilo nasikia kengere mda wote pia nimepoteza uwezo wa kusikia! Lakini nimeenda muhimbili kitengo cha ENT wamedai kuwa wao wanashugulikia tatizo la kutosikia tu hayo makelele niachane nayo,wameniandikia hizo hearing aid! Na ndo sikuelewa hayo makerer kama yanatibika ama la!
 
Kama mada ilivyo nimekua nikiteseka na kuto kusikia vizuri kwa muda mrefu kidogo, Naombeni mtu ambaye anajua tiba aweke dawa hapa ili anisaidie mimi na watu wengine walio na hili tatizo ama watu wao wengine wanaokumbwa na hili tatizo.
 
Tumia dawa hii Boric acid ear drops 2drops kila baada ya masaa 12 kwa muda siku Saba mfululizo mkuu pia pole sana
 
Je masikio (sikio) hilo halitoi sauti kama kengele sometimes? Naamini ulichoma sindano za quinine kwaajili ya malaria. Hizo dawa zinaathiri sana kwenye upande wa masikio, huku kwetu watu wengi ni waathirika wa tatizo hilo.

NB Dawa sizifahamu ila hata mimi hiyo hali ilinitokea tangu mwaka jana na kufikia mwezi may hilo tatizo likatoweka lenyewe bila ya kutumia dawa yeyote. Yaani sikio lilikuwa zito mnoo na nilikuwa najaribu kuziba sikio moja kwa kidole ili kupima kama sikio moja linafanya kazi kama lingine nikaona nikiziba sikio la kushoto, basi la kulia sisikii hata kidogo yaani hata nikifungua mziki na kupandisha volume hadi juu ndo nasikia kwa mbaaaaali, ila nikiziba sikio la kulia bhasi la kushoto nasikia vizuri sana bila ya tatizo.

Nilikuwa mzembe wa kwenda hospitali ila limepona lenyewe. Hizo dawa ziogope, japo huenda kuna vitu vingi vinaweza kusababisha hiyo hali ikiwemo bacterial infections n.k
 
Back
Top Bottom