Tatizo la macho kutoa machozi

Tatizo la macho kutoa machozi

OCC Doctors

Senior Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
114
Reaction score
172
Macho kutoa machozi mara kwa mara (Epiphora). Kazi ya macho ni kulainisha, kusafisha na kulinda jicho, ikiwa yatazalishwa mengi au ikiwa kitu kitayazuia kutoka vizuri - kunaweza kuwa na tatizo la macho kutokwa machozi mara kwa mara. Tatizo linaweza kuwa la muda, lakini pia inaweza kuwa ishara ya maambukizi makubwa ya jicho au kuziba kwa mirija ya machozi.

Hali inaweza kutokea kwa jicho moja au macho yote mawili. Kulingana na kile kinachosababisha kutokwa na machozi, macho yanaweza kukumbwa na matatizo mengine ndani au karibu na macho ikiwemo maumivu ya macho, kuwashwa, uwekundu wa jicho, maono ya mawingu yasiyoeleweka na maumivu ya kichwa.

1745308982079.png
 
Back
Top Bottom