Pole sana.
Hii kitaalamu inaitwa Chalazion (meibomian cyst/eyelid cyst ), ni uvimbe wa kope (sio tafsiri rasmi).
Chalazion ni uvimbe unaotokea kwenye sehemu kope (eyelid ) kutokana kuziba kwa tezi ya mafuta (meibomian gland) iliyoko kwenye kope. Tezi ya meibomian huzalisha mafuta ya kufanya jicho kuwa na unyevunyevu wake, hivyo ikizibwa uvimbe huo hutokea.
Chalazion huwapata watu wenye umri wa miaka 30 hadi 50 japo inaweza pia kutokea kwa watoto.
Chalazion huanza taratibu lakini mara nyingi haiumi lakini inaweza kusababisha muwasho kidogo, uoni hafifu nk.
Matibabu:
-Kanda kwa kitambaa kisafi kilicholowekwa kwa maji ya uvuguuvgu kwa dakika 15 (warm compresses).
-Usafi macho: epuka makeup, epuka kugusa macho mara kwa mara.
-Mara nyingi chalazion hupotea yenyewe: kama haitaisha basi muone daktari ili iweze kutolewa.
Kila la kheri.