Tatizo la kuvimba miguu

ulimi waupanga

JF-Expert Member
Aug 31, 2014
470
1,162
Wadau naomba ushauli wenu au anayejua tatizo ili ni nini au tiba yake ni ipi.
Mwaka 2012 nikiwa kidato cha tano apo Singida nilipata tatizo la kuvimba joints ( za vidole vya mikono, kiwiko, bega na magoti). Nilijaribu kwenda hospitali za apo Singida sikupata majibu mazuri, baada ya mda wa kusumbuka na kuangaika mwaka 2013 joints zingine zote ziliacha kuvimba tatizo likabaki kwenye magoti tu.
Baadaye ikabidi niende Bugando Mwanza baada ya kuona tatizo linazidi, pale Bugando nilifanya vipimo vingi sana tofauti tofauti, kama kupima Uric acid level, RA test, X-Ray, Rheumatoid factor na mengine mengi tu. Lakini yote majibu yalitoka NEGATIVE.
Nikachoka zaidi dakitari aliposema nirudie kupima mara ya pili kupata uhakika lakini majibu yakawa yale yale mpaka dakitari akadai labda arejee darasani kusoma maana nampatia changamoto ambayo hajawai kukutana nayo, kwa maelezo yake anasema sina sifa za kuvimba joints maana mimi siyo mwana michezo, siyo mzee(29age) wala joints zangu ni nyembamba.
Ndugu zangu kuanzia apo nikaanza kuchoka na sijui la kufanya ni nini maana pale Bugando waliishia kuniandikia vidonge vya kuchua tu.

Jinsi ugonjwa ulivyo

Magoti yanavimba sehemu ya mbele ya goti kuelekea juu, yakivimba hayaumi sema tu unajihisi uchovu mda wote na huwezi yakunja kwahiyo pata picha ukitaka kwenda kujisitiri aja kubwa, kwa pembeni mwa goti kushoto na kulia kuna kinyama kigumu kama misuli ya nyama ya sikio ilivyo iki ukikunja goti kinatembea juu na chini na maumivu kwa ndani unayasikia japo si sana, yanavimba na kusinyaa yaani siyo mda wote yanakuwa yamevimba tatizo hasa linajitokeza nikifanya kazi ngumu ya kukunja miguu au kutembea sana.


Hitimisho
Watanzania wenzangu naomba ushauri ni dakitari au dawa gani inaweza nisaidia maana kijana mdogo lakini nashindwa kufanya kazi ngumu kwa kuogopa kuyatibua magoti.
Apa chini nimeweka vipimo vya Bugando hospital angalau mwenye uelewa apate pa kuanzia kunishauli.
1544335881606.jpeg
1544336016553.jpeg
1544336069156.jpeg
 
Back
Top Bottom