Msaada: Mjomba anatatizo la kupata choo

bCg

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
384
688
umri wake ni miaka 47 Kwa Sasa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la tumbu yaani akienda hospital kupima anakutana na shida za kawaida tu kama typhoid au minyoo au vidonda vya tumbo na wakati mwingine hakutwi na tatizo lolote. Na amekuwa akipewa dawa, lakini anapata unafuu wa mda mfupi.

Hali hiii imekuwa ya miaka mingi mpaka Kwa Sasa imempelekea kuwa na choo kigumu (nitaambanisha mwishoni).

Kutokana na alivyonieleza ilinilazimu kumwambia apige picha haja yake Ili tuambatanishe Kwa lengo la kupata uhalisia wa kitu ninachoeleza lakini pia kinisaidie kumwelezea Dr. Nitakapoenda Bugando ( Kwa yeye huwa anakigugumizi hawezi kujieleza Moja Kwa Moja, hivyo huwa naambatana naye kwenye shida zinazohusiana na kujieleza).

Licha ya yeye kukata tamaa, Nimemshauri twende Bugando Hospital nikishauri apimwe Kwa kutumia vipimo vikubwa kubaini tatizo.

Kwa upande mwingine nimeanzisha maada hii, Ili kupata ushauri wa watalaamu wa afya waliomo katika jukwa hili. Kwa hiyo naomba msaada Kwa yeyote anayejua/ au mwenye ushauri.

Update.
Mgonjwa alikutwa na tatizo la H.pyroli ( baadae nilifuatilia google nikagundua ni bacteria anayesababisha vidonda tumbo).

Akaandikiwa akanunue dawa inayoitwa Heligo-kit, lakini baada ya kwenda dukani waliponionesha hizo dawa nikagundua kuwa alishawahi kupewa zaidi ya mbili lakini anapata nafuu ya kama wiki mbili tu.

Sasa ikanibidi niingie google Ili kujua zaidi namna ya kukabiliana na changamoto hii.

Sasa katika mitandao nikaoata maple dekezo ya dose zifuatazo.

Wa kwanza.

Matibabu ya Siku 10
Siku 5 za mwanzo
1. Amoxicillin 2000mg Kwa siku.

Siku 5 baada ya Siku Tano za mwanzo
1.Clarithromycin 1000mg Kwa siku.
2.Tinidazole 1000mg Kwa siku.
3. Pantoprazole 1x2

Wa pili dozi aliyopendekeza
1. Amoxicillin 1g mara mbili Kwa siku 14.
2. Clarie OD 500mg mara 2 Kwa siku 14
3. Tinidazole 500mg mara 2 Kwa siku 7, then ornidazole 500mg mara 2 Kwa siku 7
Esomepraole 40 mg x 2 Kwa siku 14.

Na wa tatu.
Clarithrimycin extended 1x1
Tinidazole 1x2
Pantoprazole sodiam 1x2
............................................
Sasa wadau!
1. Je ipo tofauti kati ya hiyo Heligo-kit na hizi dozi.
2. Kati ya hizo dozi ipi inaweza kufaa au mchanganyiko mzuri.
3. Pia ule mchanganyiko wa dozi ya pili sijauelewa mnawaza nifafanulia?

Watalaamu naombeni msaada
 
Kwa rangi hiyo ya hajja. Ndugu yako ana vidonda vya Tumbo mkuu. Akitumia dozi ya Heligo Kit kwa siku 14 then aaanze kumeza PANTOPRAZOLE SODIUM kwa siku 30 kupunguza acid kuzalishwa tumboni atapata choo kizuri na kilaini wakati woote. Kwa hali hiyo hata Nguvu za Kiume zimepotea na Tumbo ni mwendo wa kujaaa gesi na Usingizi hapati ng'ooo.
 
Alichokisema Mmteulemmteule ni asilimia 💯 ya maelezo ya mgonjwa yaani Kwa Sasa Hana nguvu za kiiume, tumbo wakati wore limejaa gesi, usingizi shida kingine ni kuwa anakojoa mkojo unaouma halafu unaasili ya rangi Jano kibichi na kinaharufu Kali
 
Akafanye x-ray ya tumbo na ultrasound ya abdominal-pelvis kwanza halafu lete picha hapa nikusaidie na ripoti ya ultrasound. Lakini pia mwili haumuwashi? muulize
Mwili anavosema hauwashi ila unakuwa kama unamoto na dalili zingine kama alizozisema Mmteule
 
Je,mgonjwa ana dalili/shida nyingine zaidi ya hizo ulizosema?

Anapata choo kigumu tu pekeake ama kuna siku anapata choo laini?

Ulaji wake ukoje?anakula vyakula vya aina gani?anakunywa maji kiasi gani kwa siku?
 
Kuna dawa inaitwa sanamaki inapatikana duka la dawa za asili itamasaidia kwenye iyo shida ya choo ipo ya unga na majani yoyote utayopata chukua achemshe anywe
 
mazingira uliopo hali yake ni vipi ya vyakula na maji
Ni ya mjini; Vyakula vinapatikana maji hutumia ya kuchemshwa. vyote! Labda ushauri wa vyakula vinavyotakiwa na vile visivyotakiwa plse.
 
Je,mgonjwa ana dalili/shida nyingine zaidi ya hizo ulizosema?

Anapata choo kigumu tu pekeake ama kuna siku anapata choo laini?

Ulaji wake ukoje?anakula vyakula vya aina gani?anakunywa maji kiasi gani kwa siku?
Ndiyo! Tumbo kuwaka moto, mate kuwa machungu, mkojo kuwa wa langi na unaunguza wakati akojoapo, gesi tumboni, nguvu za kiiume zimepungua.
 
Kuna dawa inaitwa sanamaki inapatikana duka la dawa za asili itamasaidia kwenye iyo shida ya choo ipo ya unga na majani yoyote utayopata chukua achemshe anywe
Asante! IPO maduka yapi ya wauzaji dawa za kienyejia au maduka ya dawa asili za kichina?
 
Dawa za asili hizi za kiswahili haizidi 3000 ila inasaidia sana hata kwa watoto wanaosumbuliwa na kitumbo
Asante! IPO maduka yapi ya wauzaji dawa za kienyejia au maduka ya dawa asili za kichina?
 
Alichokisema Mmteulemmteule ni asilimia ya maelezo ya mgonjwa yaani Kwa Sasa Hana nguvu za kiiume, tumbo wakati wore limejaa gesi, usingizi shida kingine ni kuwa anakojoa mkojo unaouma halafu unaasili ya rangi Jano kibichi na kinaharufu Kali
Tumbo linajaa gesi

Anakosa choo

Choo kina rangi ya njano na harufu kali

Mkojo una changamoto...

Conclusion

Nenda hospital fanya vipimo Especially LIVER FUNCTION TEST, X-RAY
 
umri wake ni miaka 47 Kwa Sasa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la tumbu yaani akienda hospital kupima anakutana na shida za kawaida tu kama typhoid au minyoo au vidonda vya tumbo na wakati mwingine hakutwi na tatizo lolote. Na amekuwa akipewa dawa, lakini anapata unafuu wa mda mfupi.

Hali hiii imekuwa ya miaka mingi mpaka Kwa Sasa imempelekea kuwa na choo kigumu (nitaambanisha mwishoni).

Kutokana na alivyonieleza ilinilazimu kumwambia apige picha haja yake Ili tuambatanishe Kwa lengo la kupata uhalisia wa kitu ninachoeleza lakini pia kinisaidie kumwelezea Dr. Nitakapoenda Bugando ( Kwa yeye huwa anakigugumizi hawezi kujieleza Moja Kwa Moja, hivyo huwa naambatana naye kwenye shida zinazohusiana na kujieleza).

Licha ya yeye kukata tamaa, Nimemshauri twende Bugando Hospital nikishauri apimwe Kwa kutumia vipimo vikubwa kubaini tatizo.

Kwa upande mwingine nimeanzisha maada hii, Ili kupata ushauri wa watalaamu wa afya waliomo katika jukwa hili. Kwa hiyo naomba msaada Kwa yeyote anayejua/ au mwenye ushauri
Habari!
Kuna mambo naweza kushauri hapa:

1: Dalili ya kutopata choo vyema/kigumu inaweza kuwa ni dalili ya tatizo ndani ya mfumo wa chakula au nje ya mfumo wa chakula nfani ya mwili.

2: Tatizo hili pia laweza kuwa ni tatizo la mwenendo wa kimaisha: ulaji/aina ya vyakula kama vyenye mizizi, vs kiasi cha maji.

3: Kuna watu ambao wamezaliwa na matumbo/ya kurithi, ambayo yako very sensitive (irritable bowel syndrome vs inflammatory bowel syndrome). Matumbo haya huwa na tabia tofauti kulingana na mwenendo wa maisha kwa ujumla wa mhusika.

4: Unapoenda kufanya vipimo ni vyema kuainisha lengo la kipimo ni kupata nini ambacho kitasaidi kukubali au kukanusha matatizo unayowaza. La sivyo, utafanya vipimo vingi ambavyo vitamvuruga mgonjwa kiakili na kisaikolojia na kiuchumi. Na hapo ni pale unapokuwa umechukua historia ya kutosha na au kumwangalia mgonjwa kwa mazingira ya mambo complex.

5: Kumekuwa na matumizi yasiyo mazuri/sahihi ya Heligokit. Kwa sasa inaonyesha kuwa resistant kwenye molecule mojawapo ya Clarithromycin.

6: Wakati mwingine tiba/dawa ni muhimu kuandamana na mabadiliko kwenye mwenendo wa kimaisha 2 na 3 hapo juu ili mambo yakae sawa. Hii ni pale utakapomtambua vyema mgonjwa na matatizo yake ya msingi.

NB: Ushauri wangu kwa eneo ulilipo na aina ya mgonjwa, ni muhimu kumwuona daktari bingwa wa magonjwa ya njia ya chakula/ Gastroenterologist au yeyote LAKINI very DEDICATED kwa asili na changamoto alizonazo mgonjwa.
 
Asante Kwa ushauri
 
Kwa rangi hiyo ya hajja. Ndugu yako ana vidonda vya Tumbo mkuu. Akitumia dozi ya Heligo Kit kwa siku 14 then aaanze kumeza PANTOPRAZOLE SODIUM kwa siku 30 kupunguza acid kuzalishwa tumboni atapata choo kizuri na kilaini wakati woote. Kwa hali hiyo hata Nguvu za Kiume zimepotea na Tumbo ni mwendo wa kujaaa gesi na Usingizi hapati ng'ooo.
Msaada wako plse
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom