Tatizo la kukwama sauti,msaada tafadhali

mwankuga

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
334
120
Naomba msaada tafadhali,

SAUTI yangu imekwama zaidi ya mwezi sasa,mara ya kwanza nilikuwa nakohoa kidogodogo,lakini baadae sauti ikapotea kabisa,nikaenda hospitali wakanipa dawa za kikohozi,lakini hadi sasa hamna nafuu yoyote,nisaidieni wakuu
 
Ongeza maelezo mkuu ili ueleweke....imekwama huti kabisaaa sauti? au inatoka lakini imebadilika inakuwa ya kukwaruza hivi? Unakohoa? kwa muda gani? Una uvimbe wowote shingoni, hata mdogo?
 
kapotea,kakaa kimya! sasa ndugu yangu maelezo hayajajitosheleza,lakini KANUNUE dawa inaitwa BRO-ZEDEX TUMIA MARA 3 SIKU TATU
KAMA HUNA TATIZO JINGINE UTAONA UNAANZA KUONGEA VIZURI BAADA YA SAA 18 TU,HAYA KAZI KWAKO
 
Nashukuru sana wakuu kwa ushauri wenu,ni kweli nilipotea.Kimsingi nina tatizo la kukwama sauti zaidi ya mwezi sasa,sauti haitoki,na hata ikitoka utafikiri nanong'ona,sikohoi na wala sina uvimbe wowote shingoni.Ninapoamka asubuhi inakuwa afadhali kidogo.
 
kapotea,kakaa kimya! Sasa ndugu yangu maelezo hayajajitosheleza,lakini kanunue dawa inaitwa bro-zedex tumia mara 3 siku tatu
kama huna tatizo jingine utaona unaanza kuongea vizuri baada ya saa 18 tu,haya kazi kwako

kwa kweli mkuu nakushukuru sana,kama ulivyonishauri nimenunua dawa hiyo na ndani ya masaa 18 sauti ikawa imerudi,kwa sasa niko safi kabisa,asante sana
 
Hii bro zedex inauzwaje kwenye maduka ya dawa!

Naitafuta,...Shida ya haya maduka holela ya dawa hayana hospitality siku hizi...wanajali sana fedha, dawa ya tsh 2000 unaweza kuuziwa kwa 20,000 kwa kutokujua tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom