Tatizo la Gonjwa la Sukari (Diabets Mellitis): Fahamu chanzo, aina na ushauri wa tiba ya tatizo hili

Copy na paste hiyo ndo shida.Kwa ufupi mimea mingi inatibu sukari sema mpaka ikukubali unaweza tumia na usipone,mf ukichanganya mbuyu na mzambarau unashusha sukari haraka sana ukiongezea na alovera umemaliza.Ila wengi wakipata nafuu wanavunja masharti kujiona wamepona.
 
Fiati naomba unisaidie namna ya kutengeneza hiyo dawa ya mbuyu,mzambarau na Alovera pamoja na dose yake.Sukari inamtesa sana mzazi wangu.
 
Kuna wakati unakuwa mazingira ambayo si rafiki na huduma ya afya na hii sukari ukahisi inapanda au ndugu yako imepanda. Basi chukua magome ya mzambarau na mbuyu, chemsha kunywa, hii husaidia kushusha sukari na ikikukubali inaweza kuwa tiba yako, ikikataa kupona kuna kitu kinafanyika.
 
Wakuu wa nchi naombeni kwa mtu anayejua clinic ya watu wenye matatizo ya diabetes, kisukari , kwa mkoa wa Arusha mjini au Moshi mjini .

Maana nimechoka na hawa watu wasiokuwa na ujuzi wanakuambia usile tunda lolote labda tangoo tuu ,usinywe maziwa yeyote, usile mayai kabisa wali ,sembe ,machalariiii ,nyama hapana kabisa , mafuta ya aina yeyote ya kupikia.

Na wamesema kama ni ugali uwe wa mtama ,na mboga za majani basi.

Kama kuna mtu anafahamu diet ya mgonjwa wa diabetes please ashushee menu please.
 
Kuna wakati unakuwa mazingira ambayo si rafiki na huduma ya afya na hii sukari ukahisi inapanda au ndugu yako imepanda. Basi chukua magome ya mzambarau na mbuyu, chemsha kunywa, hii husaidia kushusha sukari na ikikukubali inaweza kuwa tiba yako, ikikataa kupona kuna kitu kinafanyika.
Hii dozi inakua kwa muda gani? Unakunywa kiasi gani?
 
Kuna wakati unakuwa mazingira ambayo si rafiki na huduma ya afya na hii sukari ukahisi inapanda au ndugu yako imepanda. Basi chukua magome ya mzambarau na mbuyu, chemsha kunywa, hii husaidia kushusha sukari na ikikukubali inaweza kuwa tiba yako, ikikataa kupona kuna kitu kinafanyika.

it will be wise to give a full clinical trial and prove that this is a right remedy, i'd advice people to be cautious with these kinds of medications, because they are not tested because most times they look like they worked on person purely based on individual faith and not on proved scientific formulae
 
UGONJWA WA KISUKARI ni kundi la magonjwa yanayohusiana na ufanyaji kazi wa mwili ambapo mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya glucose katika mwili kutokana na mwili wake kukosa uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha au seli za mwili wake haziwezi kutumia insulin iliyopo au pengine mwili kuwa na matatizo yote mawili kwa pamoja. Mgonjwa wa kisukari hupata haja ndogo mara kwa mara (polyuria), kusikia kiu kila wakati (polydipsia) na njaa (polyphagia). Kuna aina tatu za kisukari;
<strong>Type 1 Diabetes,
Type 2 Diabetes na
Gestational Diabetes.</strong>

<strong>#1. TYPE 1 DIABETES</strong>
Mwili wa mgonjwa wa aina hii ya kisukari hautengenezi insulin kabisa. Kisukari cha aina hii mara nyingine huitwa insulin-dependent diabetes, juvenile diabetes, au early-onset diabetes. Watu huwa na kisukari aina hii wanapokuwa na umri wa chini ya miaka 40 na hasa katika miaka ya mwanzo kabisa ya ujana wao. Kisukari cha aina hii huwapata watu wachache ukilinganisha na aina nyingine za kisukari, karibu asilimia 10 tu ya wagonjwa wote wa kisukari huwa na aina hii ya kisukari.

Mgonjwa mwenye kisukari cha aina hii atapaswa kutumia sindano za kumwongezea insulin mwilini katika maisha yake yote na lazima kila wakati ahakikishe kuwa kiwango chake cha sukari mwilini kinakuwa sawa kwa kuchukua vipimo na kufuata mpango wa chakula maalum.

<strong>#2. TYPE 2 DIABETES</strong>
Mwili hautengenezi insulin kwa kiwango cha kutosha au seli za mwili zinashindwa kuitumia insulin iliyopo (insulin resistance). Karibu asilimia 90 ya wagonjwa wa kisukari katika ulimwengu husumbuliwa na aina hii ya kisukari.

Watu wenye unene usio wa kawaida na wenye uzito mkubwa wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata kisukari cha aina hii ukilinganish na wale wenye miili ya kawaida. Kuwa na uzito mkubwa au unene usio wa kwaida husababisha mwili kutoa kemikali zinazovuruga mfumo wa namna ya mwili unavyotumia chakula kilichoyeyushwa ili kuupa mwili nguvu na kuuwezesha kukua.

Kuwa na uzito mkubwa, kutofanya mazoezi na kutozingatia namna ya kula chakula kinachofaa, humweka mtu katika hatari kubwa ya kupata aina hii ya kisukari . Kwa mfano, kunywa soda moja tu kwa siku kunaongeza uwezekano wa kupata aina hii ya kisukari kwa kiwango kikubwa sana.

Hatari ya kupata kisukari cha aina hii huongezeka pia na umri, sababu kamili haijajulikana bado lakini labda kwa vile umri ukiongezeka mtu huongezeka uzito na hupunguza shughuli za kuutumia mwili wake.

Inaonekana pia kuwa mtu mwenye ndugu wa karibu mwenye ugonjwa huu, naye pia huweza kuupata ugonjwa huu. Watu wa asili ya Mashariki Ya Kati, Afrika na kusini mwa mwa Bara la Asia hupatwa sana na kisukari cha type 2 Diabetes.

Kuwa na kiwango kidogo cha homoni ya testosterone kumeonyesha kuwa na mchango katika kusababisha aina hii ya kisukari. Wataalamu wanasema kuwa kuwa na kiwango kidogo cha testosterone katika mwili kunahusiana na tatizo la mwili kutoweza kuitumia insulin (insulin resistance).

Kuna baadhi ya watu ambao wameweza kuudhibiti ugonjwa huu kwa kupunguza uzito wa miili yao, kufuata mipango mizuri ya chakula, kufanya mazoezi ya miili yao na kuchukua vipimo vya mara kwa mara kujua viwango vya sukari katika miili yao. Lakini kisukari cha aina hii ya pili ni ugonjwa unaokua kila siku na dalili zake kuongezeka kila siku, hivyo mwishowe mgonjwa itabidi aongezewe insulin. Mara nyingi wagonjwa wa aina hii ya kisukari mwishowe huongezewa insulin ya vidonge.

#3.GESTATIONAL DIABETES
Hiki ni kisukari wanachopata wanawake wakati wanapokuwa wajawazito. Baadhi ya wanawake wanakuwa na viwango vikubwa sana vya glucose katika damu zao na miili yao haina uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha kuweza kusafirisha glucose hiyo hadi kwenye seli za miili yao hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha sukari katika miili yao. Kisukari hiki huweza kudhibitiwa vizuri kwa kula chakula kinachofaa na kufanya mazoezi, Ni asilimia ndogo kati yao ambao huhitaji kupewa dawa. Gestational diabetes isipodhibitiwa huweza kusababisha matatizo wakati wa uzazi au kufanya mtoto anayezaliwa kuwa mkubwa kuliko alivyostahili.

Kisukari Ni Tatizo La Matumizi Ya Chakula Mwilini



Kisukari (diabetes mellitus) huhesabiwa kama ni tatizo la matumizi ya chakula katika mwili. Mwili wa binadamu hutumia chakula kilichoyeyushwa ili kuuwezesha kuwa na nguvu na kukua. Chakula cha aina nyingi tukilacho huvunjwavunjwa na kupata glucose, aina ya sukari katika damu ambayo ndiyo chanzo kikuu cha nguvu katika mwili wa binadamu.

Chakula baada ya kuyeyushwa, glucose huingia katika mfumo wa damu. Seli za mwili hutumia glucose hiyo ili kupata nguvu na kukua. Lakini seli haziwezi kuchukua glucose hiyo bila uwepo wa insulin, insulini ndiyo inayoziwezesha seli hizo kuchukua glucose.

Insulin ni homoni inayotengenezwa na kongosho. Baada ya kula, kongosho hutoa insulin ya kutosha kuwezesha seli kuchuka glucose iliyopo katika damu, na mara baada ya glucose hiyo kuchukuliwa na seli, kiwango cha sukari katika damu hushuka.

Mtu mwenye kisukari ni yule ambaye kiwango chake cha glucose katika damu ni kikubwa mno (hyperglycemia) kutokana na kwamba mwili wake hautengenezi insulin, hautengenezi insulin ya kutosha au seli kushindwa kuitumia insulin inayotengenezwa na kongosho. Mapato yake ni kuongezeka kwa kiwango cha sukari katika damu ambayo baadaye hutolewa nje ya mwili kupitia katika mkojo. Mgonjwa wa kisukari ana zahana kubwa ya glucose katika damu yake lakini mwili unashindwa kuitumia glucose hiyo kwa matumizi yake ili upate nguvu na kukua.

Katika kurasa zifuatazo tutaona dalili za kisukari na madhara yanayotokana na kuwa na ugonjwa huo, chakula na mazoezi kwa mtu mwenye kisukari na mwisho tiba ya mtu mwenye kisukari kwa kutumia insulin.

Ndugu msomaji wetu tunakuomba usisite kutuuliza maswali au kutoa maono yako kuhusu mada hii. Tutafurahi sana kukujibu au kupokea maoni yako.

<a href="DALILI NA MADHARA YA KISUKARI" target="_blank">DALILI NA MADHARA YA KISUKARI</a><strong>Kisukari </strong>

Tiba na Ushauri
Tovuti ya Uelimishaji na Ushauri wa magonjwa sugu, kisukari, shinikizo la damu, kansa, ugumba, upungufu wa nguvu za kiume n.k.
whatsapp/sms/call +255 714 206 306.
 
Ugonjwa wa kisukari ni ile hali ya mwili kushindwa kubalance uwiano wa sukari mwilini inayosababisha sukari inakuwa nyingi kwenye damu
Na kwa sasa ugonjwa huu umekuwa ukitibiwa kwa njia ya kupewa dawa na kuchoma sindano sinazoenda kuupa mwili insulin haijagundulika bado dawa zitakazousaidia mwili kubalance sukari wenyewe yaani kongosho liweze kupata afya na kuzalisha insulin lenyewe
Ugonjwa huu wa sukari upo katika aina mbili yaani Type I na Type II
... Kwa sasa njia pekee ya kuweza kuutibu ugonjwa huu ni kwa njia ya dawa asili na virutubisho vitakavyolisaidia kongosho kupata nguvu ya kuzalisha insulin lenyewe na Better Melon imekuwa ikitumika toka miaka ya nyuma huko China kutibu ugonjwa wa kisukari
Better mellon inamsaidia mgonjwa wa kisukari kubalance sukari katika damu kuongeza metabolism na pia kulipa kongosho nguvu ya kuweza kuzalisha insulin lenyewe
Better melon inaingredient zinazomsaidia mgonjwa kupata nguvu na kuondoa hata side effect zilizompata kutokana na ugonjwa huu


Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba 0653299934 kujipatia dawa hizo.
 

Attachments

  • thY7E5ABLR.jpg
    thY7E5ABLR.jpg
    27.9 KB · Views: 128
  • thLAD3VVBE.jpg
    thLAD3VVBE.jpg
    35.4 KB · Views: 118
  • 12642478_10206611322375709_7826115204214913702_n.jpg
    12642478_10206611322375709_7826115204214913702_n.jpg
    32.3 KB · Views: 105
Wakuu wa nchi naomba kuuliza kama Kuna Dr wa hospital ambaye anajua dawa nzuri ya Kushusha kisukari type 2 please msaada isiwe metroformin.

Shukrani and have a good day.
 
Nimekuandikia Private Massage, naomba unijibu kwa namba za simu nilizokuachia
 
Dawa zipo na baadhi ya hospital zinakuwa na special clinic kwa magonjwa ambayo huuitwa 'non communicable disease'. Ushauri wa msingi nenda clinic Ambapo utapata pia na 'health education'. Ni muhimu kwani dawa peke yake hazimalizi tatizo bila kupata Ushauri wa wataalam kwani hata life style pia ina mchango mkubwa kumsababia mtu kupata DM type 2.
 
Naomba kujua wadau. kwa sababu siku za hivi karibuni nimejikuta nakunywa maji mengi sana hasa nyakati za usiku na kupata haja ndogo mara kwa mara hasa nyakati za usiku. sasa kabla sijaenda kwenye vipimo naomba kujua zipi ni dalili za awali za kisukari. je ni vyakula gani mgonjwa wa kisukari anatakiwa asile.

=========
UFAFANUZI KUHUSU DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
madhara-ya-kisukari.jpg


Kisukari ni ugonjwa ambao humsababishia mtu kuwa na kiwango kikubwa cha sukari katika damu na kushindwa kuitumia sukari hiyo ipasavyo ili kumpa nguvu na hivyo sukari hiyo kutoka nje ya mwili wa mgonjwa kupitia njia ya mkojo. Ugonjwa huu pia huitwa Diabetes Mellitus, maneno yanayotokana na kigiriki na kilatini. Diabetes linatokana na kigiriki likimaanisha kijibomba kinachonyonya maji na mellitus linatokana na neno la kilatini “Mel” lenye maana ya asali, hivyo diabetes mellitus ni “kunyonya maji yenye utamu kama asali” baada ya madaktari wa enzi hizo kugundua kuwa mkojo na damu ya mgonjwa wa kisukari vilikuwa na glucose kwa wingi sana.

Wachina wa zamani nao waligundua kuwa mchwa walijaa kwa kwingi kwenye eneo la mkojo wa mtu mwenye kisukari kutokana na mkojo huo kuwa mtamu na wakatoa neno “Sweet Urine Disease” -Ugonjwa wa kutoa mkojo mtamu.

Insulin Na Kongosho

Insulin ni homoni inayotoa ishara kwa seli za mwili ili ziweze kuchukua glucose kotoka kwenye damu na kuitumia katika kuupa mwili nguvu na kuujenga. Kama kiwango cha insulin mwilini ni kidogo au hakuna insulin kabisa katika mwili, glucose haitachukuliwa na seli za mwili hivyo kusababisha mwili kuyeyusha mafuta yaliyomo mwilini ili upate nguvu.

Insulin karibu za wanyama wote hufanana, tofauti ni katika nguvu ya ufanyaji wake wa kazi. Kwa mfano, insulin ya nguruwe “Porcine insulin”, inafanana sana na insulin ya binadamu, hii ikiwa na maana kuwa binadamu anaweza kutumia insulin ya wanyama. Lakini kwa bahati nzuri, insulin inaweza kutengenezwa kwenye maabara.

Kongosho ni sehemu ya viungo vilivyo katika mfumo wa uyeyushaji (mmeng’enyo) wa chakula na kinapatikana sehemu ambapo mbavu hukutana kwa chini. Kongosho lina umbo la jani na lina urefu upatao kama nchi sita. Kongosho ina kazi ya kutengenza insulin na homoni zingine za kusaidia uyeyushaji wa chakula.

Dalili Za Kisukari Ni Zipi?

Baada ya kujikumbusha hayo, sasa tutazame mambo ambayo yakikutokea ujue kwamba ni dalili za kuwa na ugonjwa huu wa kisukari. Watu wengi wanakuwa na ugonjwa huu bila kujijua kwa sababu dalili za awali za ugonjwa huu hazimsababishii mtu kushindwa kuendelea na shughuli zake za kawaida, lakini ni vizuri kuugundua ugonjwa huu katika hatua zake za awali ili kuepukana na madhara makubwa yanayoweza kutokea baadaye. Tutaorodhesha hapa dalili zinazojionyesha mara nyingi zaidi:

Kukojoa mara kwa mara: Jee, umekuwa na tabia ya kwenda kupata haja ndogo mara kwa mara? Kama jibu ni ndiyo, basi figo zako sasa haziwezi kuirudisha glucose kwenye mfumo wa damu na badala yake zinachukua maji kutoka kwenye damu na kusababisha kibofu kijae mara kwa mara.

Kiu Isiyoisha: Kama unakojoa mara kwa mara, utapata kiu isoisha kwa sababu mwili unahitaji kurudisha maji uliyopoteza kwenye mkojo.

Njaa Kali: Kama isulin yako haifanyi kazi au kama huna insulin, mwili wako unakosa glucose ya kuupa nguvu. Katika kutafuta njia nyingine ya kupata nguvu, mwili utakuwa na njaa ili uupatie chakula.

Kuongezeka kwa uzito (unene): Hii inatokana na dalili ya kusikia njaa kali.

Kupungua uzito kusiko kawaida: Hili huwatokea zaidi wagonjwa waType 1 Diabetes kwa sababu kwa kukosa insulin na seli kukosa chanzo cha kupata nguvu, mwili huanza kuvunjavunja misuli na kuyeyusha mafuta ya mwili ili upate nguvu hiyo hali inayochangiwa zaidi na tabia ya kisukari cha aina hiyo kujitokeza kwa ghafla.

Uchovu wa mwili: Mwili unapokosa glucose ya kuzipa seli nguvu, uchovu hutokea.



dalili-za-kisukari.png




Hasira: Hasira zinaweza kuwa ni sababu ya mwili kukosa nguvu.

Kutoona vizuri: Ugonjwa huu husababisha mtu kushindwa kuviona vitu vizuri. Tatizo hili hutibika lakini mara nyingine hali huweza kuwa mbaya kiasi cha kuwa na tatizo la kudumu au kupata upofu.

Vidonda kutopona vizuri au haraka: Unapokuwa na sukari nyingi katika damu, uwezo wa mwili kuponya vidonda hupungua.

Magonjwa ya ngozi: Mwili wenye sukari nyingi ndani ya damu huwa na uwezo mdogo sana wa kujiponya kutokana na maambukizi ya wadudu. Wanawake wenye kisukari huwa na maambukizi zaidi na hupata shida kubwa ya kuponya maambukizi ya sehemu nyeti za miili yao.

Kuwashwa kwa ngozi: Kuwashwa kwa ngozi mara nyingine ni dfalili ya kuwa na kisukari.

Kuwa na fizi nyekundu au zilizovimba: Fizi nyekundu na/au zilizovimba huweza kuwa kuwa ni dalili ya kuwa na ugonjwa wa kisukari, mara nyingine meno hulegea.

Uwezo mdogo wa kushiriki tendo la ndoa: Hili ni tatizo hasa la wanaume wenye umri unaozidi miaka 50, ambapo mara nyingi watakosa uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kikamilifu au uwezo wao wa kufanya tendo hilo kufa kabisa (Erectile Dysfunction).

Ganzi mikononi au miguuni: Uzidifu wa sukari mwilini huweza kuharibu neva au mishipa midogo ya damu inayolisha neva, hivyo kusababisha hali ya ganzi mikononi au miguuni.


kisukari-four.jpg




Madhara Ya Kisukari

Kama ugonjwa wa kisukari hautadhibitiwa ipasavyo, madhara makubwa huweza kutokea. Baadhi ya madhara ambayo yamehusishwa na ugonjwa huu ni kama ifuatavyo:
  • Matatizo ya macho-glucoma, cataracts na mengineyo.
  • Matatizo ya miguu-vidonda na gangrene ambavyo mara nyingine husababishwa miguu ikatwe.
  • Matatizo ya moyo-pamoja na upungufu wa damu inayoelekea kwenye misuli ya moyo.
  • Hypertension-ambayo huweza kulsababisha figo kushindwa kufanya kazi, matatizo ya macho, magonjwa ya moyo na kiharusi.
  • Matatizo ya kusikia-kisukari husababisho tatizo la kushindwa kusikia vizuri.
  • Gastroparesis-misuli ya tumbo kushindwa kufanya kazi yake vizuri.
  • Kiharusi (Stroke)-endapo blood pressure, cholesterol na sukari havitadhibitiwa, uwezekano wa kupatwa na kiharusi huwa ni mkubwa sana.
  • Ugumba-kisukari humfanya mgonjwa ashindwe kufanya tendo la ndoa.
VIPI UNAWEZA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU?
Ikiwa unayo historia katika familia sio lazima kwamba utapata ugonjwa huu. Lakini kwa wale ambao wanaweza kuupata wanaweza kuuchelewesha kwa kujitahidi kuishi maisha ya afya nzuri kwa kula chakula bora, mazoezi, kula mboga mboga kwa wingi na kujiepusha na uzito wa mwili. Pia kupima damu baada ya kila muda ikiwa una historia katika ukoo au una wasi wasi kutokana na dalili zilizotajwa hapo juu.

JEE KUNA MATIBAU YA MARA MOJA KUONDOA UGONJWA HUU?
Kwa dawa za hospitali mpaka sasa hakuna dawa ya kuondoa moja kwa moja ingawa hasa kwa aina ya 2 watu baada ya kurekebisha vyakula wanaweza kujiweka katika hali hali ambayo mwili unaweza kutumia insulin yake kidogo bila ya kula vidonge au sindano. Kuna utafiti wa kufanya transplant ili kuongeza insulin mwilini kwa kutumia sehemu (pancreas) ya mtu mwengine lakini bado haujafanikiwa kuweza kutumika kama ni matibabu.
 
Back
Top Bottom