JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,327
- 9,328
Hii kitu nimekutana nayo sana kwenye familia tatu za engine za toyota
NZ engines[1NZ-FE, 2NZ-FE]
AZ engines[1AZ, 2AZ]
na ZZ engines [1ZZ sanasana]
Sitotaja gari zinazotumia hizo engine sababu hata nikianza kuzitaja ni nyingi sitamaliza, lakini huenda zaidi ya 50% ya gari ndogo ambazo watu wanatumia zinaangukia kwenye hizo engine family nilizotaja hapo juu.
Hasa nimekutana nayo kwenye Rav 4 na IST lakini huenda ipo kwenye gari nyingi sana sababu toyota gari nyingi zinashare engines.
Okay ishu yenyewe ipo hivi,
Gari inachemsha, inaweza hata ikaunguza cylinder head gasket na kupindisha cylinder head.
Unarudishia kila kitu fresh, ila ukija kuwasha gari, engine inakaa Idling vizuri kabisa ila changamoto inakuja ukikanyaga accelerator.
Ukikanyaga tu accelerator inakuja misi kubwa yaani gari inaweza hata kuzima. Ukiikanyaga taratibu na kwa kwa kuibembeleza ndio mshale wa RPM unapanda vizuri kabisa.
Ila ukikanyaga kawaida au haraka basi lazima imisi. Na ukiwa barabarani ndio ile unakanyaga gari haitembei. Na kibaya zaidi kwenye Diagnostic mashine huwa haioneshi chochote.
Sasa hiyo ishu unaweza ukabadilisha spea mpaka kichwa kikauma ila in real sense sababu kubwa huwa ni Kuharibika kwa Ignition Coil Pack Zote.
Nimeshakutana na Case 6 mtindo huo na mara zote ilikuwa ni Ignition coils.
Ukifunga coil pack zingine ishu inapotea kabisa.