Tatizo la Corona: Wa kulaumiwa ni Serikali kwa asilimia 100%

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Tatizo la Corona wa kulaumiwa ni serikali kwa asilimia 100% nitawalaani mpaka kaburini

Nina sababu ya kusema serikali ndo ya kulaumiwa kwa sababu zifuatazo

KWANZA kabisa kipindi mwezi wa pili na wa tatu Corona ilivyoanza kuwa serious ninyi mliendelea kuwapokea watalii na wachina tena bila kificho mkisema kuwa hamtaki kupoteza mapato na watalii kwa sababu ya Corona

PILI ni kwamba mliendelea kuruhusu wageni na safari zikiendelea bila kujali watu wetu watakaoambukizwa mkijimwambafai kwamba mmejizatiti kwa kuwapima watu Airports

TATU mlikua mnaidharau Corona Rais na Makonda walikua wakidharau Corona wakiita kuwa ni kaugonjwa kadogo tu hako na kasiwatishe watanzania huku mkisema ni kaugonjwa kadogo mngekua basi hata mmejiandaa kufanya tafiti ya dawa za asili na kuandaa mazingira ya kukabiliana na Corona. Halafu sasa hivi mnasema tuombe my dear government maombi hayatosaidia chochote mungu hadhihakiwi na wala hapendi unafiki!

NNE hamkufunga mipaka hata mpaka sasa sidhani kama mmefunga sijui mnataka tufe wote?

TANO mliwapa wanasiasa nafasi mkaingiza siasa kwenye ugonjwa mara polepole aite wapinzani Corona mara makonda atoe matamko ya hovyo hovyo sasa hivi mambo yamekua magumu mnasema tuombe maombi hayatosaidia chochote kile nawaambia maana mlikufuru mkasema korona ni kaugonjwa kadogo sana.Mmesahau suala la bashite kumtangaza mtoto wa mbowe kuwa ana Corona na kwamba ni mungu kaleta Corona kwa familia ya Mbowe

SITA hili ni kosa kubwa sana mlificha data za ugonjwa wa Corona sijui mlikua mnamaanisha nini mfano tu mdogo kulipotiwa Corona Zanzibar na mgonjwa mkabisha lakini baadae ikaja kuonekana ni kweli,mlificha sana na sasa mmeona hali ni mbaya hadi waziri anakiri alikua anaficha ficha lakini sasa ameamua kuwa muwazi mmepika data na mnaendelea kuficha maana watu wanakufa wengine ni ndugu zetu kabisa na tena wanakufa kwa Corona mnawazika lakini cha ajabu hairipotiwi

Sasa hivi mmeona hali ni mbaya Mloganzila imejaa ndio mnakumbuka shuka kumekucha watu wameathirika wengi mnoo Corona inatembea mtaani kama nzi mmekumbuka shuka kumekucha watanzania wengi wanaenda kupoteza maisha kwasababu ya uzembe wenu

Wa kulaumiwa ni serikali ya awamu ya tano kwa asilimia 100 na nitawalaani mpaka kaburini
 
Hatari sana hii serikali walisema utalii utakufa sasa makampuni yanakufa na mamia ya watu washapoteza ajira, jiwe alisema miradi ya sgr itasimama tukifunga mipaka lakini hii corona ikituchapa hao wanaojenga watachapwa na miradi itasimama, jiwe hana akili yule

ntawalaani kamati ya 2015 kwa kutuletea huyu mtu hafai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwasasa Wananchi waliowengi wamemchukia kiasi cha kutisha kwa kweli waliobaki wanampenda ni Mapolisi tu kwa sababu amekuwa akiwaongezea mishahara kila wanapowapiga na kuwadhalilisha Chadema ila Zitto hawamgusi
Wanainchi wanaomchukia ni kikundi Cha wahuni wa ufipa ila mamilioni ya watanzania watakupa jibu kwenye sanduku la kura uchaguzi ujao
 
Hatari sana hii serikali walisema utalii utakufa sasa makampuni yanakufa na mamia ya watu washapoteza ajira, jiwe alisema miradi ya sgr itasimama tukifunga mipaka lakini hii corona ikituchapa hao wanaojenga watachapwa na miradi itasimama, jiwe hana akili yule

ntawalaani kamati ya 2015 kwa kutuletea huyu mtu hafai

Sent using Jamii Forums mobile app
Its a matter of common sense that prevention is better than cure.We lost such an opportunity when WHO warned us that Covid-19 is pandemic.

Utalii utashuka kwani uchumi wa dunia upo ICU na utaendelea kushuka kwani nchi watokapo watalii zipo duniani na dunia nzima imekumbwa na Corona.

Hivi vita ni vita kama vita nyingine tuungane pammoja kwa kutumia nguvu na akili zetu.

Sisi kama taifa tufungue macho,hatuna mjomba tuko peke yetu ndio ukweli.Kinyume chake tutateketea sote kwa ujinga wa watu wachache.
 
Serikali za nchi nyingine unazizungumziaje mkuu? Ilikua ni halali kwa nchi nyingine kupata maambukizi?

Unazungumza kanakwamba serikali yetu ya imezembea MNO.

Huu si muda wa kulaumiana. Endelea kusambaza elimu kwenye jamii tuzidi kujikinga.

- Satan -
 
Namtafakari Magufuli nakosa majibu wazee...

Hivi anawaza nini!??
Unakumbuka uongo wake mwingine wa Uchumi wa kati wakati wakati Watanzania wanaishi kwenye hizi nyumba
Mud-Home-1.jpg
 
Its a matter of common sense that prevention is better than cure.We lost such an opportunity when WHO warned us that Covid-19 is pandemic.
Utalii utashuka kwani uchumi wa dunia upo ICU na utaendelea kushuka kwani nchi watokapo watalii zipo duniani na dunia nzima imekumbwa na Corona.
Hivi vita ni vita kama vita nyingine tuungane pammoja kwa kutumia nguvu na akili zetu.
Sisi kama taifa tufungue macho,hatuna mjomba tuko peke yetu ndio ukweli.Kinyume chake tutateketea sote kwa ujinga wa watu wachache.
Kuna wakati inakuwa vigumu kuelewa viongozi wetu wanatumia nini kufikiri. Unakataa kuzuia wageni kuingia nchini mwako eti kwa kuhofia kukosa watalii ambao wameelemewa na corona huko kwao?
 
Tatizo la Corona wa kulaumiwa ni serikali kwa asilimia 100%nitawalaani mpaka kaburini

Nina sababu ya kusema serikali ndo ya kulaumiwa kwa sababu zifuatazo

KWANZA kabisa kipindi mwezi wa pili na wa tatu Corona ilivyoanza kuwa serious ninyi mliendelea kuwapokea watalii na wachina tena bila kificho mkisema kuwa hamtaki kupoteza mapato na watalii kwa sababu ya Corona

PILI ni kwamba mliendelea kuruhusu wageni na safari zikiendelea bila kujali watu wetu watakaoambukizwa mkijimwambafai kwamba mmejizatiti kwa kuwapima watu airports

TATU mlikua mnaidharau Corona rais na makonda walikua wakidharau Corona wakiita kuwa ni kaugonjwa kadogo tu hako na kasiwatishe watanzania huku mkisema ni kaugonjwa kadogo mngekua basi hata mmejiandaa kufanya tafiti ya dawa za asili na kuandaa mazingira ya kukabiliana na Corona.Halafu sasa hivi mnasema tuombe my dear government maombi hayatosaidia chochote mungu hadhihakiwi na wala hapendi unafiki!

NNE hamkufunga mipaka hata mpaka sasa sidhani kama mmefunga sijui mnataka tufe wote?

TANO mliwapa wanasiasa nafasi mkaingiza siasa kwenye ugonjwa mara polepole aite wapinzani Corona mara makonda atoe matamko ya hovyo hovyo sasa hivi mambo yamekua magumu mnasema tuombe maombi hayatosaidia chochote kile nawaambia maana mlikufuru mkasema korona ni kaugonjwa kadogo sana.Mmesahau suala la bashite kumtangaza mtoto wa mbowe kuwa ana Corona na kwamba ni mungu kaleta Corona kwa familia ya Mbowe

SITA hili ni kosa kubwa sana mlificha data za ugonjwa wa Corona sijui mlikua mnamaanisha nini mfano tu mdogo kulipotiwa Corona Zanzibar na mgonjwa mkabisha lakini baadae ikaja kuonekana ni kweli,mlificha sana na sasa mmeona hali ni mbaya hadi waziri anakiri alikua anaficha ficha lakini sasa ameamua kuwa muwazi mmepika data na mnaendelea kuficha maana watu wanakufa wengine ni ndugu zetu kabisa na tena wanakufa kwa Corona mnawazika lakini cha ajabu hairipotiwi

Sasa hivi mmeona hali ni mbaya mloganzila imejaa ndo mnakumbuka shuka kumekucha watu wameathirika wengi mnoo Corona inatembea mtaani kama nzi mmekumbuka shuka kumekucha watanzania wengi wanaenda kupoteza maisha kwasababu ya uzembe wenu

wa kulaumiwa ni serikali ya awamu ya tano kwa asilimia 100 na nitawalaani mpaka kaburini

Sent using Jamii Forums mobile app
Hadi sasa, ukiacha Zanzibar ambako wagonjwa bado wanaongezeka, Tanzania bara, kwa kiasi kikubwa umedhibitiwa. Sababu kubwa ya kudhibitiwa ni wananchi kuzingatia ushauri wa wataalamu, na usimamizi makini wa Serikali.

Baadhi ya Mikoa imwxhukua hatua zaidi ya kuhakikisha vyombo vya usafiri na maeneo ya mikusanyiko ya watu km hospitali, masoko, nk yanapuliziwa dawa.
 
Kuna wakati inakuwa vigumu kuelewa viongozi wetu wanatumia nini kufikiri. Unakataa kuzuia wageni kuingia nchini mwako eti kwa kuhofia kukosa watalii ambao wameelemewa na corona huko kwao?
Mkuu nafikiri kwa sasa hivi hakuna ubishi kuwa Covid-19 ni janga kubwa la kitaifa na dunia nzima.
Hao viongozi wabishi muda haupo upande wao,walifanya makosa makubwa ya kupenda pesa za watalii kuliko uhai wananchi watanzania.Leo nashangaa tunapomtania Mungu kwa maombi.Kwanini hawakutumia madaraka yao kufunga mipaka mapema?
 
Back
Top Bottom