Tatizo la constipation kwa mtoto

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,023
Nina mjukuu wangu wa kiume ana umri wa miaka 4 na wiki 2.
Ana tatizo la kufunga choo anaweza kaa wiki nzima bila kwenda haja kubwa pamoja na kumpa matunda kama mapapai.

Hili jambo linanitisha sana. Mtoto ana uzito mkubwa usio wa kawaida. Alishawahi kulazwa discharge summary yake iliandikwa hivi
admitted due to C/c

-DIB
-fever
Diagnosed with
1.CHD
R/s s.PNA
2.Hypothyrodism

Tx for PNA and get relief
Baada ya kutoka hospitali report iliandikwa hivyi.
Discharged Diagnosis
1.CHD.
2.PNA.
3.Hypothyrodism.
Naomba wataalamu mbalimbali mnisaidie pengine endocrinologist kutokana na hilo neno hypothyrodism.
Je constipation inasababishwa na yaliyoandikwa juu? na nifanyeje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole kwa madhila.
Ni kweli kuwa hypothyroidism inaweza kusababisha choo kigumu.
Je ulielezwa chochote juu ya ufuatiliaji wa tiba ya hiyo hypothyroidism au ilikuwa bado haijathibitishwa?
Ilithibitishwa na ndio maana discharge report yake inaonyesha hivyo imepita miaka miwili na hatukuambiwa chochote ila kipindi hiki ndio tunashangaa hali hiyo ya kufunga choo mda mrefu.

Kuna wakati tunamwekea maji ya sabuni kwa bomba la sindano ndio anakwenda choo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilithibitishwa na ndio maana discharge report yake inaonyesha hivyo imepita miaka miwili na hatukuambiwa chochote ila kipindi hiki ndio tunashangaa hali hiyo ya kufunga choo mda mrefu.
Kuna wakati tunamwekea maji ya sabuni kwa bomba la sindano ndio anakwenda choo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama imethibitishwa ni muhimu kufuatilia matibabu yake. Kwani huo msingi wa tatizo husika. Lakini pia hii inaweza kuleta shida kwenye ukuaji na maendeleo ya mtoto kwa ujumla. Hata hilo suala la uzito uliopitiliza, uwezo wa nguvu za mtoto na mapigo ya moyo.

Wakati mwingine huwa tunasau kujadili na wagonjwa kuhusu nini kinamsibu mgonjwa na nini kimefanyika au nini kitahitajika kufanyika zaidi kwajili ya mwendelezo wa tiba za wagonjwa wetu.
Hii inaweza kuwa kwa sababu ya kutokuwa na utaratibu madhubuti au kazi nyingi au kupitiwa.

Huwa inahitaji team approach.
Wahusishe watu wafuatao:
1: Endocrinologist/daktari bingwa wa vichocheo vya mwili
2: Pediatrician/daktari bingwa wa watoto
3: Pediatric surgeon kama atahitajika.
 
Ahsante sana umeongea kweli kabisa mimi nilikuwa kikazi porini muda mrefu.
Alivyotoka hospitali akaonekana mzima na huu unene watu wanaona ni afya shauri ya maziwa tunayompa ya ng'ombe niko nyumbani sasa machale yakanicheza hasa baada ya kuona discharge summary yake.Aise naku inbox tuwe tunawasiliana separately umekuwa msaada kwangu kitaalam . nimeona wewe ni Dr by profession

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom