Tatizo la circle cell limealibu penzi langu,msaada zaidi wa kimawazo!

Akagando

JF-Expert Member
May 24, 2012
533
116
Nilikuwa na Mpenzi ambaye tumekutana katika Somo lakini Mpenzi huyu anakuwa akijishitukia mara kwa mara kwa kuniambia hapendi kuumizwa kwa sababu alishakuwa na mpenzi ambaye alimtenda lakini nimejaribu kuulizia kwa Wenzangu wanao mfahamu wanadai ana ugojwa wa Sickle Cell ndio maana hapendi kuwa na Mpenzi na hivi juzi akanipigia simu nikiwa likizo na kudai hanitaki,nimejaribu kumuuliza sababu anadai hataki kuhumizwa katika Mapenzi.Jamani wana JF nisaidie msaada wa kimawazo kuhusu kuoa mwanamke mwenye ugojwa wa sickle Cell Anemia,
 
Pole sana kaka lakini mi cna mchango wa kimawazo maana nilikimbia masomo ya sayansi.
Napita TU.
 
Nilikuwa na Mpenzi ambaye tumekutana katika Somo lakini Mpenzi huyu anakuwa akijishitukia mara kwa mara kwa kuniambia hapendi kuumizwa kwa sababu alishakuwa na mpenzi ambaye alimtenda lakini nimejaribu kuulizia kwa Wenzangu wanao mfahamu wanadai ana ugojwa wa circle Cell ndio maana hapendi kuwa na Mpenzi na hivi juzi akanipigia simu nikiwa likizo na kudai hanitaki,nimejaribu kumuuliza sababu anadai hataki kuhumizwa katika Mapenzi.Jamani wana JF nisaidie msaada wa kimawazo kuhusu kuoa mwanamke mwenye ugojwa wa circle Cell Anemia,

Sahihisho kidogo: Ni Sickle cell or more of a technical notation HbS
 
Nilikuwa na Mpenzi ambaye tumekutana katika Somo lakini Mpenzi huyu anakuwa akijishitukia mara kwa mara kwa kuniambia hapendi kuumizwa kwa sababu alishakuwa na mpenzi ambaye alimtenda lakini nimejaribu kuulizia kwa Wenzangu wanao mfahamu wanadai ana ugojwa wa circle Cell ndio maana hapendi kuwa na Mpenzi na hivi juzi akanipigia simu nikiwa likizo na kudai hanitaki,nimejaribu kumuuliza sababu anadai hataki kuhumizwa katika Mapenzi.Jamani wana JF nisaidie msaada wa kimawazo kuhusu kuoa mwanamke mwenye ugojwa wa circle Cell Anemia,

Nenda mkapime, kama nyote ni HbSS basi msioane, kama mmoja ni HbS na mwingine ni normal, haina shida sana product zenu zitakuwa normal ingawa kunaweza kuwa na elements za HbS. Watawashauri zaidi na kwa undani zaidi!
 
mshauri mwende mkapime, ikigundulika ana half na wewe huna mnaweza kuendelea bila shida kwa watoto mtakao wapata.
 
Nenda mkapime, kama nyote ni HbSS basi msioane, kama mmoja ni HbS na mwingine ni normal, haina shida sana product zenu zitakuwa normal ingawa kunaweza kuwa na elements za HbS. Watawashauri zaidi na kwa undani zaidi!

Asante Mkuu.lakini suala la kuzaa wakati wa kujifungua kwa wa Sickle cell Mgojwa alina tatizo
 
Swala lako lipo sehemu mbili.
1. Kama alivyokuambia hataki tena mahusiano kwasababu alishaumizwa. Kisaikolojia ni kweli na si yeye tu watu wengi ambao ni 'majeruhi wa mapenzi' hujikuta katika hali kama hiyo.

2. Sickle cell, yaweza kuwa anafahamu ukubwa wa tatizo lake na pengine kuona kuwa hakuna mwanaume atakayekuwa tayari kukabiliana na tatizo pale linapojitokeza.Pengine experience yake ya mwanzo kuhusiano na hilo haikuwa nzuri

Ugonjwa wa sickle cell: Ni tatizo la mamubile ya chembe za damu. Huu ni ugonjwa wa kurithi.
Mtu anaweza kuwa nao na usijitokeze kama vinasaba vya urithi vimejificha ' recessive'.
Inapotokea wawili wenye hali hiyo wakapata mtoto, anaweza kuwa na maradhi yanayojitokeza kwavile vinasaba vimejidhihiri (dominant).Hii ni kwa uchache tu wa kuelewa lakini mada yenyewe inayohusu ugonjwa ni pana sana.

Kujibu swali, je, kuna tatizo. Jibu ni ndio au hapana. Itategemea hali yake na uwezekano wa kubeba mimba (mkijaaliwa).
Je, mtoto ni lazima awe na ugonjwa? Jibu ni hapana itategemea wewe una vinasaba vya aina gani,jibu linaweza kuwa ndio kama vinasaba vyako vitakuwa na chembe kama zake.

Lakini pia unaweza kuoa au kuolewa na mtu mwenye tatizo na kulitambua baadaye. Muhimu ni jinsi gani mna mapenzi, mapenzi yenu yapo kwa minajili gani na utayari wa kukabiliana na hali hiyo. Mapenzi hayana mpaka hata kama ni wa maradhi.
 
Hemu msaidie tu kujibu based on both; mwenzenu kaambiwa tu mtaa hii issue kwa hiyo hatutegemei atoe issue inatoeleweka Sana, msaidieni mwenzenu kapenda Jamani.

Ah, Au ngoja nikushauri, piga chini Tafuta mwingine, watu wakikosa Wapenzi wao Wanasema hawatapata mwingine Kama huyo ila Ni mindset, mi ninetoswa Mara 8 nikalia sana, wananipora kila Siku; Wa 9 sasa ambaye Ni Mama mtoto Mbona Safi kuliko Wote 8?

QUOTE=CHUAKACHARA;4637389]Sahihisho kidogo: Ni Sickle cell or more of a technical notation HbS[/QUOTE]
 
Hemu msaidie tu kujibu based on both; mwenzenu kaambiwa tu mtaa hii issue kwa hiyo hatutegemei atoe issue inatoeleweka Sana, msaidieni mwenzenu kapenda Jamani.

Ah, Au ngoja nikushauri, piga chini Tafuta mwingine, watu wakikosa Wapenzi wao Wanasema hawatapata mwingine Kama huyo ila Ni mindset, mi ninetoswa Mara 8 nikalia sana, wananipora kila Siku; Wa 9 sasa ambaye Ni Mama mtoto Mbona Safi kuliko Wote 8?

QUOTE=CHUAKACHARA;4637389]Sahihisho kidogo: Ni Sickle cell or more of a technical notation HbS
[/QUOTE]

Mkuu ilo sawa lipo lakini akiongea na Marafiki zangu usema Ananipenda ila anaogopa kuhumizwa pia mi siwezi kumuacha kirahisi sababu anaweza kuhisi kutengwa.
 
Hakuna tatizo hata kidogo. Kwani kuna theory gani unayoiogopa? Nahisi unahofia upungufu wa damu, sio kweli

kuna usemi kwamba mgojwa wa sickle cell uweza kupata matatizo wakati wa kujifungua ikiwemo kuvuja damu bila kikomo na hivyo kusababisha upungufu wa damu kwa Mgojwa.
 
kuna usemi kwamba mgojwa wa sickle cell uweza kupata matatizo wakati wa kujifungua ikiwemo kuvuja damu bila kikomo na hivyo kusababisha upungufu wa damu kwa Mgojwa.

Hapana, hiyo unayoisema ni hemophilia (lack of clotting factors in the blood). Tatizo la mchumba /mpenzi wako ni diminished oxygen carrying capacity of the blood (defective red cells in this case) due to sickle cell disease
 
Niliwahi kuwa na jirani nikiwa mtoto aliyekuwa na huo ugonjwa. Watu walikuwa wanasema wenye huo ugonjwa kuwa hawafiki miaka 18...imani za mitaani hizo.

Huyu dada alikuwa mkubwa, akapata kazi. Ila alikufa baada ya kuolewa. Alafu alikuwa hata ukimuona unajua kuwa yuko weak. Inatia huruma sana. Kama unampenda mpe matumaini na mwambie kuwa unajua anaumwa and you dont care.

Tatizo naona na wewe umeshaanza kuwa na wasiwasi. Inataka upendo wa dhati kuwa na uhusiano na mtu mwenye ugonjwa kama huo. Ni moja ya magonjwa ambayo familia za Kiafrika zilikuwa zinachunguza kabla ya kuoa au kuolewa na koo fulani.
 
Back
Top Bottom