a) Leta data na research inayoonyesha kwamba waislamu wanahitaji ajira zaidi kuliko wakristo?
b) Wewe ambaye si muislamu unajuaje umuhimu wa mahakama kama siyo ubinafsi na chuki zako..
c) Gharama ngapi serikali ime-finance miradi ambayo inahudumia dini moja (wakristo) waislamu hawakuja na hoja za kipuuzi kama hizi
d) You can postpnent the issue lakini lazima itakuwepo wakati huo itakuwa too late kujadili kwa busara kama sasa
Tumain
Mbona na wewe hutuwekei data za miradi ya wakristo wanaofadhiliwa na serikali.Chuki naiona kwako kwa jinsi ulivyoleta hoja yako.watanzania wote wawe waislamu au wakristo wanahitaji ajira hilo halina swali.
Katika hali ya jaziba unayoionyesha nina wasiwai kwamba huwezi kujenga hoja yoyote,tulia utafakari ujibu kwa hoja badala ya kujibu kwa jazba.
watu wengi hasa ambao si waislamu wangependa kujua faida na hasara za kuanzishwa mahakama hiyo.
Ikumbukwe kwamba tulifika mahala ambapo swala la udini halikuwapo,ninapoandika hivi ninaushahidi wa marafiki zangu na baadhi ya ndugu ambao wameoana wakiwa dini tofauti,hapa na maanisha dini siyo dhehebu,yaani mmoja mkristo na mwingine mwisilamu. Hata wengine walifikia mahala ambapo kila mmoja anabakia na dini yake je ikifikia mgogoro hao wataamuliwa na sheria gani? hayo ndo mambo tunatopenda kuyajadili,tuyajue kabla hatujajutia uamzi wetu kama wahenga walivyosema kuwa "majuto ni mjukuu".
Nina jua ndugu zangu tulivyo na msimamo tunapo shupalia jambo
hata ikibidi bila kulitafakari,lakini kuna busara pia kukaa chini na kutafakari
serikali haitawaliwi na wakristo tu wamo waislamu pia ambao wanaunga msimamo huo wa serikali, sasa basi hii mbinde inatokana na nini ndo maana wengine wanaanza kuwa na wasiwasi kuwa kuna ajenda ya siri ndani yake.
mnataka muanze kukatana mikono kama sharia inavyoagiza?angalieni mtapoteza waumini wakishaona sharia zingine za ajabuajabu,