Upendo, mshikamano, haki ,ukweli na umbele vinapaswa kuzingatiwa.
Viongozi Wa ATCL msilikwepe hili, Upendo miongoni mwenu uko kidogo saana, Mshikamano ni Wa mashakamashaka miongoni mwenu mnajua mnao marubani bora kabisa lkn mnabaniana.
Haki inapindishwa pindishwa ili kukatishana tamaa, Rais kanunua ndege, hakuweka uchoyo kwenu, katenda haki kwenu na kwa Watanzania wote, iweje nyie mbaguane msitendeane haki?
Ukweli miongoni mwenu ubaki kuwa ukweli, kwann, mnaongopeana ongopeana. Rais katoa kozi, jiulizeni mmetendeana haki, na ukweli umefanyika? Mko sawa kiviwango? Au mnaminyiana tu! Msije mkazalisha HUJUMA.
Peaneni umbele, bila kuathiri mtiririko mzima Wa mafunzo yenu, aliyeanza kwenda kozi azingatiwe haki zake za kimafunzo afuatie mwingine na mwingine vinginevyo mkienda mnavyoenda shaghalabagala mnakuwa mnalengo baya.
Hammfurahishi, baba wala watoto wake.mmeaminiwa tendeaneni niliyowashauri msipinge YAPO