Ameshindwa kuishauri na kuisimamia serikali itekeleze ahadi zake alizotuahidi kama kutatua kero ya maji, barabara, elimu, nk. Umenielewa?Kwanza kaa ukitambua kwamba kama ni ugonjwa kila mmoja anaweza kuugua ukiwemo na wewe,kwa hiyo usimnyanyapae kwa hili lake la ugonjwa,pili suala la ujenzi wa barabara na hayo mengine meengi uliyoyaleta sio kazi ya Mbunge,ni kazi ya serikali,nambie mbunge ambaye ameweza kuwajengea wananchi barabara hata kilomita tano tu kwa pesa zake,kwa hiyo huwezi kufanya tathmini kubwa kama hiyo kwa hivi vigezo ulivyovitoa,nenda kajipange urudi humu ndani vizuri.
Ahsante kwa taarifa hii mkuu. Nimefarijika sana na chembechembe za mabadiliko zinazoanza kujitokeza huko Tabora hasa ikizingatiwa Tabora ilikuwa ngome kuu ya CCM.Kutoka Sikonge-CDM inahimarika sana tokea kushinda udiwani-ipole,vijana wanachukua kadi,magwanda n.k... heko CDM!
Nenda pale Ubungo Msewe ukaulize wananchi, ua Baruti. Na kuanzia mwezi ujao, subiri uone rangi ya ubungo. Kaangalie matawi ya msingi yanavyojengwa. Tumechukua mabalozi kibao wa CCM. Nenda mwenyewe, au piga simu kwa Mbepela.Tuthibitishie maneno yako. Inamaana Mnyika kazitekeleza ahadi zake kwa ufasaha au ni kwamba wananchi hawaitaki tu CCM?
Wakuu, nadhani tuanze kupima upepo wa kisiasa wa CHADEMA ukoje majimboni mwetu. Je kama uchaguzi ungefanyika leo CHADEMA ingeshinda jimboni kwako leo?. Kwa kuanzia jimboni kwangu Iramba mashariki dalili zinaonesha dhahiri ya kwamba kama uchaguzi ungefanyika leo CHADEMA ingeshinda katika nafasi ya ubunge kutokana na kupwaya sana kwa mbunge aliyepo madarakani, Salome D Mwambu [ CCM ]. Mbunge wa sasa ameshindwa kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi kama tatizo sugu la maji, barabara mbovu, huduma mbovu za afya, ukosefu wa walimu na vitabu mashuleni, nk. Mbunge wa sasa haongei na wananchi, ni mbaguzi wa kimaeneo na pia ni mgonjwa. Hajatimiza ahadi zake hata moja. Katika nafasi ya udiwani na urais bado shughuli ni pevu kwani tathimini inaonyesha CCM na CHADEMA watagawana kura kwa usawa. Je hali ikoje jimboni kwako kama uchaguzi ungefanyika leo?
Wakuu, nadhani tuanze
kupima upepo wa kisiasa wa CHADEMA ukoje majimboni mwetu. Je kama
uchaguzi ungefanyika leo CHADEMA ingeshinda jimboni kwako leo?. Kwa
kuanzia jimboni kwangu Iramba mashariki dalili zinaonesha dhahiri ya
kwamba kama uchaguzi ungefanyika leo CHADEMA ingeshinda katika nafasi ya
ubunge kutokana na kupwaya sana kwa mbunge aliyepo madarakani, Salome D
Mwambu [ CCM ]. Mbunge wa sasa ameshindwa kutatua kero mbalimbali
zinazowakabili wananchi kama tatizo sugu la maji, barabara mbovu, huduma
mbovu za afya, ukosefu wa walimu na vitabu mashuleni, nk. Mbunge wa
sasa haongei na wananchi, ni mbaguzi wa kimaeneo na pia ni mgonjwa.
Hajatimiza ahadi zake hata moja. Katika nafasi ya udiwani na urais bado
shughuli ni pevu kwani tathimini inaonyesha CCM na CHADEMA watagawana
kura kwa usawa. Je hali ikoje jimboni kwako kama uchaguzi ungefanyika
leo?
Nimemwangalia Salome kama kielelezo cha CCM jimboni. Serikali ya CCM imeshindwa kutekeleza ahadi zake. Mbunge wake amepoteza popularity jimboni. Kuhusu Msindai, Hollela, Dr Msengi na wengineo pia hawakubaliki kwa wananchi. Msindai alishaipata nafasi ya kuwatumikia wananchi kwa awamu tatu lakini hakuna cha maana alicho-deliver. Dr Msengi na Hollela wamegombea mara kadhaa na wananchi wamewakataa. Hawakubaliki. In general CCM ipo ICU Iramba mashariki.We unamwangalia Salome Mwambu ama CCM kwa ujumla wake kwa nafasi ya ubunge? Msindai na wengineo watakaotokeza umewasahau?
Tutajie japo kidogo mafanikio ya kichama yaliyopatikana kutokana na hizo operation. Je uongozi wa CHADEMA kwenye manispaa ya Tabora upo imara?katika jimbo la Tabora manispaa mambo ni mazuri kwani baraza la vijana(BAVICHA) wakishirikiana na vijana wa saut tabora wamefanya operesheni katika kata 23 za manispaa na kubakiza kata 3 tu,ambazo muda si mrefu zitamaliziwa
Nimekupata mkuu. Vipi Hawa Ghasia hajaanza kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao?Nenda pale Ubungo Msewe ukaulize wananchi, ua Baruti. Na kuanzia mwezi ujao, subiri uone rangi ya ubungo. Kaangalie matawi ya msingi yanavyojengwa. Tumechukua mabalozi kibao wa CCM. Nenda mwenyewe, au piga simu kwa Mbepela.
Ahsante kwa taarifa mkuu. Je unaweza kutuambia Halima Mdee ametekeleza ahadi zake kwa kiasi gani huko Kawe? Je wananchi wana maoni gani?. Kwa upande wa Rombo sina mashaka na wana Rombo kwa sababu ni wana mabadiliko wa muda mrefu. Pia wana uelewa sana.Kwa hapa Dar, Jimbo la Kawe CDM bado iko juu. Japo kazi ya ziada inatakiwa ifanyike CCM hawachelewi kuchakachua kama uchaguzi uliopita.
Kule Mkoani: Jimbo la ROMBO linafahamika kuwa ni nguzo kuu ya CDM. Hata kipindi kile cha Mrema na NCCR yake, CCM na dola yake bado Rombo ilimchagua mbunge wa CDM bwana Salakana.
Hawa ngumbi mkuu, aaaa huyo atafute vijijini, labda udiwani, kiwango chake kwa ubunge wa ubungo mmmm? Lile jimbo kichwa kweli.Nimekupata mkuu. Vipi Hawa Ghasia hajaanza kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao?
Ahsante mkuu kwa correction. Nilikuwa namaanisha Hawa Ng'umbi. Mshindani wa Mnyika 2010. Kero ya maji Ubungo Mnyika ameitatua kwa kiasi gani?Hawa ngumbi mkuu, aaaa huyo atafute vijijini, labda udiwani, kiwango chake kwa ubunge wa ubungo mmmm? Lile jimbo kichwa kweli.