Tathmini ya Chaguzi za CCM (Kizota, Dodoma 2012)

Tathmini ya Chaguzi za CCM (Kizota, Dodoma 2012)

MARIRE

Nafurahi kwamba umefurahia tathmini yangu. January makamba hawezi kugombea 2015 kwasababu mbalimbali 1. Bado mdogo na Katiba haimruhusu-huwezikujua kama wananchi watabadili hicho kipengele, 2. Ajitoe kundi la EDWARD NGOYAI LO-RUSHWA kwani tunajua fika aliyemsaidia hadi akaibuka wa pili NEC.
 
Hatimaye chaguzi za CCM katika ngazi mbalimbali ndio umemalizika, Idodomya. Ifuatayo ni tathmini yangu:

1. MAAMUZI MAGUMU
Kwa utaratibu ulioanza mwaka huu, kundi la kifo la NEC lilipunguzwa toka 20 na kubaki 10 huku wagombea wakiwa ni 31. Kutokana na woga wa viongozi wengi waliamua kukimbilia mawilayani ambako kupita ni almost guaranteed labda uwe na mpinzani wa haja kama ilivyokua kwa Mh Sumaye.

Wale WOTE 20 walioshinda NEC 2007 walikimbilia huko mfano Laighwanan, Chenge, Sumaye etc kasoro B. Membe PEKE YAKE. Katika uchaguzi wa 2007 nafasi nne za juu zilikua
1. Chenge
2. Lowassa
3. Makamba Sr
4. Membe

Membe alifanya uamuzi MGUMU, NA WA HATARI wa kujipima ubavu kama alioufanya Mwl JK Nyerere tar 12.7.1955 kuamua kuendelea kuwa Mwalimu au Siasa. Membe angeshindwa ingekuwa tabu sana kuibuka tena.Kwahiyo MH YOU DESERVE A MASSIVE PAT ON THE BACK! HATS OFF, SIR!

2. MAKUNDI
Uchaguzi umedhihirisha kuana makundi mawili. Kundi la Kwanza ni la MAFISADI ambao ni wazee wa kupiga dili za mjini na wana pesa nyingi linaongozwa na DON LA KIMASAI LAIGHWANAN TEDDY LOWASA. Kundi la pili ni la WAPINGA UFISADI likiongozwa na Mwanadiplomasia Bernard Membe. CCM ina kazi ya ziada kuyaunganisha makundi haya baada ya uchaguzi huu maana kuna chuki kali baina yao.


3. RUSHWA
Rushwa ilitawala SANA katika chaguzi hizi. Kundi la mafisadi lilitumia hela nyingi mno na kufanikiwa kujaza watu wao mawilayani pamoja na kwenye Jumuia zile 3. Hii inaonyesha kwamba kwa kiasi fulani bado kuna watu wanakubali kuuza utu wao na kununuliwa ili kumchagua kiongozi.

4. PCCB
Licha ya rushwa kugawiwa WAZIWAZI maeneo mengi eg Mahotelini, guest, ukumbini, vyooni, kwa mama ntilie, kwa wauza vocha. Kinachosikitisha SANA ni kwamba licha ya Rushwa kugawiwa WAZIWAZI lakini hakuna mtu aliyekamatwa na kushitakiwa wakati hata vyombo vya habari viliandika bila kificho kua kiwango kilikua 40,000, 70,000 na 100,000. Ipo haja kubwa ya PCCB kufumuliwa maana IMESHINDWA KAZI.

5. MAGAZETI
Katika kipindi chote hiki waandishi wengi waliweka pembeni ethics zao na kuamua kwa makusudi kabisa kumpamba LAIGHWANAN na haihitaji kua na Rocket scientist kujua kilichopelekea waandishi ambao wengine wanaheshimika sana katika jamii kumnadi TEDDY kiasi kile ndo maana vichwa vya habari vilikua "Lowasa awatimulia vumbi ccm(kana kwamba yeye si ccm), "Lowasa amtimulia vumbi Membe", 'Lowasa ni maji marefu" "Lowasa hashikiki" etc. Waandishi tuwe wazalendo jamani!

6. KUMPINGA JK KWA VIPEPERUSHI
Kundi la TEDDY kwa kuwatumia akina BASHE lilitengeneza vipeperushi ili kutaka JK asichaguliwe kua Mwenyekiti na abaki kua Rais. Hili lilifanywa kwakua kundi hilo linaamini JK yuko kwa Membe hivyo lilitaka "Mtu wao" ndie aikwae nafasi hiyo. Matokeo yake ni kuaibika kwani JK ameshinda kwa KISHINDO!

7. MANGULA
Mafisadi ambao walikua wanataka S. Wasira ndie awe M/Mwenyekiti walipigwa butwaa kuona mpinga ufisadi hodari Mh Philip Japhet Mangula ndie aliechaguliwa. Kwa hakika uteuzi huu uliwaduwaza sana akina Bashe!

8. KURA ZA ITIFAKI
Poroja kwamba chaguzi za CCM zina kura za Itifaki zilizikwa rasmi Kizota. M/Mwenyekiti mstaafu alitangaza na wote tulimuona katika runinga zetu akisema wagombea wote 31 wa kundi la kifo wanaruhusiwa kwenda kushuhudia kura kuhesabiwa au kutuma wawakilishi wao. Wagombea 25 kati ya 31 walienda wenyewe na 6 walituma wawakilishi na kura zilihesabiwa chini ya Spika Mh. A. makinda.

9. KURA 1,455 ZA MEMBE
Suala kubwa la kujiuliza ni wapi zilitoka kura hizi. Teddy kwa kumtumia Bashe alieleza wazi kua juhudi yao kubwa ni kumchinjia baharini Membe ili asiwemo kwenye TOP TEN kwa hali yoyote. Walitumia kila njia waliyoijua na kila hila na pesa nyingi lakini Membe, kama alivyoahidi kabla ya uchaguzi kua atawashangaza, akaibuka kidedea! Je hoja kwamba TEDDY ana watu wengi vikao vya ccm ni porojo tu? Je watu walikula hela na kumpigia Membe? Bashe baada ya kuona Membe KAWATIMULIA VUMBI bila aibu akabadili "goal posts" na kudai eti "Membe mwenyewe kashinda kwa kura kiduuuuchu, hakuwemo tatu bora wala tano bora na kwanza kashindwa na watoto eg January, Nchemba ".

Membe hakusema atakuwa wa kwanza wala tano bora ila alisema atawashangaza wabaya wake na kweli amewashangaza na kubaki WAMEDUWAA! Kua wa kwanza au wa mwisho haina impact yoyote kwenye kuteuliwa na chama kupeperusha bendera. 2002 kundi la akina Sumaye lilolkua likimwogopa sana JK lilimfanyia mizengwe SANA JK ili asifanye vizuri kundi la kifo NEC la wagombea 20. Matokeo yake JK akawa wa 18 kati ya 20 ambapo akina Sumaye, Malecela walingara. JK ndiye akaja kuwa mgombea wa ccm 2005 licha ya kuibuka wa 18 NEC!!!

10. KUBADILISHWA SIKU YA UCHAGUZI WA TOP TEN NEC
Uchaguzi wa wajumbe 10 wa kundi la kifo ulikua ufanyike sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti na M/Mwenyekiti siku ya tarehe 13.11.2012. Baada ya kushtukia kwamba LAIGHWANA na kundi lake la mafisadi wameandaa dina jumapili ili kugawa mikwanja kwa wajumbe, CCM ilibadili na Mh Msekwa akatangaza kwamba uchaguzi huo utafanyika mapema. Kitendo hiki kilikua ni pigo kwa Mafisadi. CCM INA WENYEWE!!

11. THINKTANKS WA MAFISADI
Ni dhahiri mafisadi wana mbumba za kufa mtu but tatizo washauri wanaomzunguka TEDDY ni waganga njaa wasio na mikakati kwani kwao wanadhani ukiwa na hela kila kitu kinawezekana mf M. Mahanga, P. Serukamba, Bashe, etc. Lazma mjue mikakati.

USHAURI KWA TEAM LAIGHWANAN:

"Mgombea" wenu ana madoa makubwa SANA mawili ie 1. Mwalimu Nyerere alimkataa 2. Fisadi. Haya ni madoa makubwa sana ambayo yanahitaji JIKI special ili kumsafisha na sidhani kama itawezekana. Suala la kwanza ni Nyerere PEKEE ndie angemsafisha but sasa hayupo. Mwaka 2005 wakati Malecela anagombea niliandika makala kwenye RAI kua Malecela hatapita kwenye CC maana Nyerere alimkataa. Nilibezwa na kutukanwa sana na wapambe wake waliokua na uchu wa kwenda magogoni, THE REST IS HISTORY! Suala la pili nalo ni gumu mno maana migao ya pesa inayoenda miskitini, makanisani, etc vyote ni hongo tu.
Sasa nashauri MJIPANGE vinginevyo itakula kwenu.

MATOKEO YA UCHAGUZI YAMEDHIHIRISHAPASINA SHAKA KUWA
1. HAMUMUWEZI MEMBE
2. KUWA NA PESA BILA MIKAKATI THABITI NI KUPOTEZA MUDA.

Great thinkers manonaje?

du kwa CCM kila kitu kinawezekana.....shida ni kuwa huko ccm siasa ni biashara.......si unakumbuka ile tiki taka ya genda aliyopigwa nayo sita kuvuliwa uspika?????

ila wanadai kuna makundi manne......yale mawili yalienda wapi???
 
BUSHO

Umedai mimi sina lolote bali ni mtoto wa Membe. Assuming kweli naitwa GALIYA BERNARD CAMILIUS MEMBE je hoja zangu mbona umeshindwa kujibu hata moja? Nilidhani kwamba Great Thinkers jukumu letu ni kubishana kwa hoja au????
 
Kuna tofauti. Kikwete hakukataliwa, ila aliambiwa bd mdogo, akue kwanza.
LOWASA NA MALECELA ndiyo walikataliwa live na Nyerere.

Jk bado mdogo kivipi ndugu ilhali alikua na miaka 43 by then na katiba inahitaji 40yrs pekee? Nyerere alimaanisha ana mawazo ya kitoto bado hivyo hafai kwa urais na for bad luck hadi leo bado hajakua..
 
I'm beginning to think hili swala la makundi ni bullshit ..Yani lowasa na camp Yake inatosemwa sanaaa wampinge JK kwa kura mbili tuu?? Izi propaganda tuu Nape anatulisha so his party can stay relevant.
 
Wakuu, nchi hii na ccm ina watu wengi tu wazuri na wasio walarushwa
 
Wote Mafisadi

Membe alitaka Kuuza Nchi kwa Libya leo Unamwita Mpinga Ufisadi? Naona CCM wanataka kututengenezea Mwanasesere Membe na Kumfanya Kuwa ni Msafi sana

Lowasa ni Mwizi wa EPA akatumia Pesa za EPA kufanikisha Ushindi wa akina Membe 2005

Narudia tena Hakuna Msafi Ndani ya CCM. Wote ni Wezi Mkuu umesahau List of Shame ya Dr. Slaa

Nakubaliana na wewe kwa asilimia 101 kwamba katika wapinga ufisadi Tanzania MEMBE sio moja wao. Alikuwa anaunga mkono waziwazi utapeli wa dhahiri uliyotaka kufanywa wa kuchote fedha za wa-Libya zilizoifadhiwa TIB kwa kisingizio cha eti kutaka kujenga Kiwanda cha Cement . Membe ni fisadi full STOP
 
BUSHO

Umedai mimi sina lolote bali ni mtoto wa Membe. Assuming kweli naitwa GALIYA BERNARD CAMILIUS MEMBE je hoja zangu mbona umeshindwa kujibu hata moja? Nilidhani kwamba Great Thinkers jukumu letu ni kubishana kwa hoja au????

Kaka hizi ni sindano za moto na zimewachoma vilivyo, ndo maana wanafura kwa hasira na kupambana na mtu badala ya hoja. Hakika umepiga ikulu na sasa naweza kuona kwamba Ted Rushwa amezungukwa na novices wa siasa na ambao wamegeuza jamaa kuwa ATM. Sasa kwa lineup ya Sekretarieti jamaa ndo keshaelekezwa kibla!
 
JUMATANO, NOVEMBA 14, 2012 04:18 BAKARI KIMWANGA NA DEBORA SANJA, DODOMA

*Awaonya wanaotaka kutenganisha nafasi ya rais na chama
*Aeleza alivyochukiwa ndani ya chama kwa kusema ukweli
*Asema baadhi ya mawaziri wakipigiwa simu usiku hawapokei

KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, amewashukia wanachama wa chama hicho waliokuwa na lengo la kutaka kumpunguzia madaraka Rais Jakaya Kikwete kwa kutenganisha nafasi za urais na uenyekiti wa chama.

Amesema kwamba, wanaotaka mabadiliko ni wale wasiokuwa na kazi na ambao wameshindwa kutimiza wajibu kikazi.

Makamba alitoa kauli hiyo mjini hapa jana, katika Mkutano wa Mkuu wa CCM uliohitimishwa jana ambapo alikuwa akimuombea kura Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa amepitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama ngazi ya taifa.

"Ndugu zangu, Wakwere na Wasambaa huwa wanatumia methali isemayo kuwa, hata siku moja tembo hawezi kuelemewa na mkonga wake, leo hii mtu anakuja eti tumpunguzie rais kazi, huyo anayesema hayo anayo kazi moja kwa sababu hata aliyonayo imeshamshinda.

"Anayesema Rais Kikwete apunguziwe kazi hasemi hiyo kazi nyingine tumpe nani," alisema Makamba huku akishangiliwa na wajumbe wa mkutano huo.

Suala la urais 2015

Katika mazungumzo yake, Makamba ambaye alijizolea sifa katika kipindi chake cha uongozi kwa kukariri mistari ya vitabu vya dini, alisema hivi sasa kuna watu wamekuwa wakipita na kujiaminisha kuwa wana sifa za kuwania urais wakati wa uchaguzi mkuu, mwaka 2015.

Alisema kwamba, watu hao wasijidanganye kwamba wanajulikana, kwani kipimo sahihi cha kujulikana na jamii katika kuwania nafasi hiyo ni kikao katika mkutano mkuu taifa wa CCM.

"Kuna watu ambao sasa hivi wanajiona wanajulikana kumbe wanajijua wenyewe sisi hatuwaoni. Ili uwe rais, lazima ujulikane mara tatu, yaani ujijue wewe, wajumbe wakujue na Mungu pia akujue kama ilivyo kwa Dk. Jakaya Kikwete.

"Moja ya sifa ya mgombea wa nafasi hiyo ya uenyekiti wa taifa wa CCM ni Rais Kikwete kuwa karibu na watu wa rika zote, sambamba na kujitoa pale yanapotokea matatizo.

"Hakika, leo kila mtu anajua mkataba baina yetu na Dk. Kikwete ni ilani ya uchaguzi, kwani hakuna asiyejua kuwa wewe umekuwa mtu wa watu, kila siku tunakuona kwenye misiba, tunakuona Muhimbili, wapo humu viongozi wenzako hatuwaoni kwenye maziko na baadhi ya mawaziri ukiwapigia simu usiku, anapokea mkewe na anakwambia mzee amelala.

"Mimi huwa nasema ukweli hata kama mkikasirika, tabia hii ya kuwa mkweli ndiyo ilinipa matatizo wakati nikiwa Katibu Mkuu.

"Nilijengewa chuki lakini bado itabaki ukweli ni ukweli kwa maslahi ya CCM na nchi yetu kwa ujumla," alisema Makamba.

"Nayasema haya kwa sababu katika chaguzi zilizopita za chama na jumuiya za CCM kwa ngazi zote za matawi hadi mkoa, zilikuwa zinapanga safu ya wachezaji kwa ajili ya ushindi na leo tunachagua kocha na baada ya hapo tutaunda ‘benchi la ufundi' ambalo ndiyo sekretarieti ya chama.

"Mimi ni shabiki wa timu ya Simba. Timu ya Yanga walifanya usajili mzuri wa wachezaji, lakini wakachagua kocha mbaya, baadaye rafiki yangu Manji akashtuka akabadilisha kocha, sasa wanaipeleka puta Simba, hivyo leo hii tumchague kocha bora ambaye ni Jakaya Kikwete.

"Wale wenye nia ya kupiga kura za maruhani washindwe, Mungu asimame katikati yenu mumchague Dk. Kikwete, msiwe na hiana katika hili.

"Ni vema wajumbe mkatambua kuwa, Rais Kikwete naye ni binadamu kama wengine, hivyo mkataba wake na CCM ni utekelezaji wa ilani na kwamba asihukumiwe kwa matendo ya kibinadamu," alisema Makamba.

Hotuba hiyo ya Makamba, ilionekana kuwafurahisha wajumbe wa mkutano huo, kwani baadhi yao walishindwa kujizuia na kujikuta wakienda kumtuza fedha na kusababisha hotuba kusimama kwa muda.

Utaratibu wa kupiga kura wabadilika

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida, utaratibu wa kupiga kura kwa nafasi hiyo ya uenyekiti ulibadilishwa na kusababisha taharuki miongoni mwa wajumbe.

Utaratibu huo ulitangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Spika wa Bunge, Anne Makinda. Chini ya utaratibu huo, wajumbe waligawiwa karatasi za kupiga kura kwa kufuata mikoa yao badala ya kutumia utaratibu uliozoeleka kugawiwa karatasi kwa kila mjumbe.

Utaratibu huo ulionekana kama njia ya kuzuia uvumi wa kuwepo kwa kura za maruhani, kwani makatibu wa mikoa walipewa jukumu la kugawa na kukusanya karatasi za kura kutoka kwa wajumbe wa mikoa yao.

Katika uchaguzi huo, Rais Kikwete alikuwa akitetea nafasi yake ya uenyekiti kwa kipindi cha pili na wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Katibu Mkuu wa zamani, Philip Mangula na kwa upande wa Zanzibar mgombea alikuwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
 
Uh... Kikwete atakuwa na MAKATIBU waKUU 3 toka ashike Madaraka ya URAIS???
 
Sidhani kama mwenye akili timamu anaweza kumfurahia Makamba. Yaani utumbo wote alioufanya akiwa katibu ndo anaita ukweli? Sioni tofauti yake na wachumia tumbo wengine waliopo ndani ya chama
 
It was a mistake, big mistake kumpa Makamba nafasi ya ukatibu mkuu. Anaweza kufaa kwenye mambo mengi lakini sio ukatibu mkuu wa chama.
 
STEVE umesema ccm hawaaminiki wanawezakumpendekeza Lowasa kugombe..Je mbona hujatupa ushahidi au hata sababu za wao kumpendekeza? Hivi jitihada anazofanya Mwenyekiti za kuweka watu safi we unazionaje?
 
galiya,asante kwa uchambuzi wa kina uliojaa vina,laighwanan ana strategies za hatari sana ikiwemo hata ya kuondoa uhai na ndo maana wanatumia nguvu nyingi sana kumpinga,jamaa ana mawe,kwa jinsi ulivyomfumbua si ameshakalasuka sasa na atakuja kivingine,au we unaonaje mkuu
 
Last edited by a moderator:
LAIGHWANAN kama atakuja kivingine anajua mwenyewe. Cha msingi Watanzania wamemshtukia hivyo inabidi AJIPANGE. TENA AJIPANGE SANA
 
Namkubali sana kinana!Ni msema kweli na muungwana!Ndio maana huwa naamini kuna Waislamu safi na Waislamu Feki!Shein ni mfano mwingine mzuri wa watu makini waislamu wanaoweza kuweka kando dini na kuongoza nchi isioyokuwa na dini na yenye machanganyiko wa dini kama yetu!Hakika kwa safu hii EL ana kazi!
 
mwanawe sana ataanza jiona anaweza kuwa Amir Jeshi Mkuu.
 
Nyumba haiungui kwa mwanga wa tochi.
Huu ndo moto aliowasha??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom