Dr. Ngwazi
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 723
- 289
Pamoja na kutoshinda kwa Ndugu Edward Ngoyai Lowassa, bado kuna haja ya kufahamu kuwa Lowassa amemzidi na kumfunika Dr. Slaa aliyegombea mwaka 2010 kupitia CHADEMA. Mwaka 2010, kura zilizopigwa zilikuwa 8,398,394 na Dr. Slaa alipata kura milioni 2.2 ambazo ni sawa na asilimia 26.34 ya kura zote. Mwaka huu, zilipigwa kura 15,193,863 na Lowassa kupata kura milioni 6 na ushee sawa na asilimia 39.97.
Mshindi wa mwaka 2010,Rais Kikwete alipata asilimia 61 na wa mwaka huu amepata asilimia 58.46. Ukitazama kwa jicho kali, utaona na kujua kuwa Lowassa amemzidi kwa mbali sana Dr. Slaa. Pia, CCM imeendelea kupungua kwa asilimia za kura zake. Ni wazi sasa kuwa, Lowassa ameongeza hta majimbo ya uchaguzi kwa CHADEMA na CUF pamoja na vyama hivyo kupoteza baadhi ya majimbo yao.
Lowassa amesaidia kupoka ngome mbalimbali za CCM na kuzikabidhi CHADEMA na CUF. Mwaka huu, kwa uwiano wa kura za wagombea wa Urais wa Tanzania, CHADEMA itapata nafasi za viti maalum kwa wingi zaidi na kutoachwa mbali na CCM kama ilivyokuwa mwaka 2010. Haya pia ni mafanikio yaliyoletwa na Lowassa huko CHADEMA na kumzidi kwa mbali Dr. Slaa wa mwaka 2010. CHADEMA ilicheza karata zake vyema.
Kila la kheri watanzania!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Hivi mamlaka ya Kikwete mwaka huu haujayaona kwenye uchaguzi huu?Umesema kweli ndugu yangu! Dr.Slaa alipata 26% akipambana na Rais aliye mamlakani tena aliekuwa ana kibindoni na 80%, Chadema ilikuwa na Mgogoro wa ndani na Zitto, haikuwa na Backup wala fedha za kampeni leo baada ya kazi kubwa ya uhamasishaji 2010-2015, sapoti ya umoja wa Ukawa, ukwasi wa fedha zilizotumika, mpasuko uliotokea ccm watu kuhama, ccm kuleta mgombea mpya n.k Wamepunguza kura za urais ccm kutoka 61% ya Rais Kikwete mpaka 58% za Rais Mteule Dr.Magufuli i.e only 3% tena baada ya wazee na kina mama wengi kuogopa fujo kupiga kura, Dr.Slaa alisema Siasa ni Science Mbatia akapinga akasema ni Sanaa saaa kaona matokeo ya sanaa za mgombea wake!
Hii hoja haiwezekani. Ni kitu gani kinakuaminisha kwamba wapenzi wa Lipumba na Slaa walimpigia Kura Lowassa hasa baada ya Slaa na Lipumba wenyewe kujitokeza hadharani kumpinga Lowassa na, especially Dr. Slaa kuwashawishi wapenzi wake wamchague Magufuli?Mkuu kumbuka lowwasa aliingia akiwa na mtaji wa kura za lowassa26% na kura za lipumba12% hizo ndio kura walizopata ukawa 2010 sasa tathimini yako ianzie hapo lowassa ameongeza % ngapi je hizo % zinatija kiasi cha kumtupa dr na kubadilisha gea juu kwa juu na swali la kujiuliza kama dr na lipumba wangekuwepo na kundelea kuisimamia misingi walioijenga je ukawa wasingepata kura nyingi zaidi ya hizo? Na sasa lowassa ameshashindwa Urais je ule mshikamano wa wana ukawa utaendelea kuwepo na ile sologan ya chadema ya kupinga ufisadi itarejea baada ya kufa kifo cha mende pindi lowassa alipochaguliwa kuwa mgombea wa Urais kupitia Ukawa?
Slaa ni bora mara 200 kuliko Lowassa.Lowassa ni nguvu ya FEDHA na kumbuka kaanza kitambo 2008.Halafu Lowassa amekuwa "backed up" na UKAWA ambayo ni vyama vinne.Kwa vyama 4 plus Lowassa mwenye nguvu ya fedha 39% ni ndogo sana.SILAA WA 2010 WATU WALIMPENDA KUTOKA MOYONI KABISA NIKIWEMO MIMI SEMA CCM WALITUMIA UZOEZI WA MIAKA 50 NA NILIUMIA ALIVYOSHINDWA INGAWA ALINITOKA AKILINI ALIVYOANZA KUTUMIWA NA MBOWE-SAKATA LA ZZK.Lowassa kaua vyama 4 kwa mpigo.SUBIRI MTAFUTANO UANZE MAANA KUNA (TeamLowassa,4U Movement,CDM Asilia,NCCR Mageuzi,NLD na CUF).
Hii hoja haiwezekani. Ni kitu gani kinakuaminisha kwamba wapenzi wa Lipumba na Slaa walimpigia Kura Lowassa hasa baada ya Slaa na Lipumba wenyewe kujitokeza hadharani kumpinga Lowassa na, especially Dr. Slaa kuwashawishi wapenzi wake wamchague Magufuli?
Ok, kama ni nguvu ya pesa wewe ulipewa kiasi gani?.....ni kampeni gani tanzania utafanya bila kuwa na pesa?....kama ni nguvu ya ukawa unajua 2010 Prof. Lipumba alikiri kumsadia Rais Kikwete?
Nguvu kubwa ielekezwe kwenye kudai katiba mpya.
Hii hoja haiwezekani. Ni kitu gani kinakuaminisha kwamba wapenzi wa Lipumba na Slaa walimpigia Kura Lowassa hasa baada ya Slaa na Lipumba wenyewe kujitokeza hadharani kumpinga Lowassa na, especially Dr. Slaa kuwashawishi wapenzi wake wamchague Magufuli?
Angalia uwiano wa kura, siyo idadi ya kura...maana yake linganisha 26.34% za Slaa dhidi ya 39.97% za Lowassa.
Ni kura za Urais Mkuu. Mwaka huu, viti maalum vitapatikana kwa CCM na CHADEMA tu.
Mzee Tupatupa
sawa mkuu ila hatukushindwa katika box la kura tumeshindwa na ubabe wa jk &co.
Na unaonaje tukiweka factor ambayo ita-estimate kura zilizopungua kutokana na Dr. Slaa kuwaambia wale wanaomkubali wampigie kura magufuli? Plus za wapenzi wa Lipumba ambao kwa kuona mtu wao 'ameonewa' waliamua kutopiga kura kabisa au kumpigia kura magufuli?Usijumlishe % za slaa tu jumlisha za lipumba na za nccr jumla kuu ni % ngapi ndio ulinganishe na za lowassa hapo ndio utapata jibu kama lowassa amefanya vizuri au laa!!
Na unaonaje tukiweka factor ambayo ita-estimate kura zilizopungua kutokana na Dr. Slaa kuwaambia wale wanaomkubali wampigie kura magufuli? Plus za wapenzi wa Lipumba ambao kwa kuona mtu wao 'ameonewa' waliamua kutopiga kura kabisa au kumpigia kura magufuli?
Kila mmoja anao ushawishi, hapa suala ni nani mwenye ushawishi zaidi. In this case bado naona Lowassa alikuwa na ushawishi zaidi maana pamoja na Lipumba na Slaa kuhamishia kura za wapenzi wao CCM na ACT, bado Lowassa ameweza kupata 40% (assuming hizo ndizo alizopata kweli).Kwa hiyo tunakubaliana kuwa dr na lipumba walikuwa na ushawishi mkubwa na tulifanya kosa kubwa kubadili gea juu kwa juu na madhara yake ndio haya tunayoanza kuyaona sasa?