Tathmini: Dhamira ya "maandamano ya Mange" imefanikiwa

Tathmini: Dhamira ya "maandamano ya Mange" imefanikiwa

Kwa mwenye akili kibàmia ndiyo ataona zoezi limeshindwa.
Kiukweli maandamano yameshindwa vibaya, mpende msipende, Mange pia Kakiri.
Nzuri zaidi msimamo wa Amiri jeshi mkuu uko palepale, watu wafanye kazi, siasa Majitaka hazitakiwi, watanzania wanajua na ,dunia inajua.
Endeleeni na propaganda za kuchafua taifa, labda wakoloni watawaelewa
 
Kiukweli maandamano yameshindwa vibaya, mpende msipende, Mange pia Kakiri.
Nzuri zaidi msimamo wa Amiri jeshi mkuu uko palepale, watu wafanye kazi, siasa Majitaka hazitakiwi, watanzania wanajua na ,dunia inajua.
Endeleeni na propaganda za kuchafua taifa, labda wakoloni watawaelewa
Ndiyo maana nimesema mwenye akili ndogo hatalielewa hili , ishu siyo watu kuandamana ila jee dunia imeona nini kuhusu hayo maandamano.
 
Uko hapa ili "uonyeshwe"? Bahati mbaya sina hiyo hulka. Siko hapa "kujionyesha".
Kama ndio hivyo, usidhihaki wenzako ambao ni wajanja kweli kweli na wanajukwaa wa JF ikiwemo wewe mnafuatilia maandiko yao.
 
Maandamano yaliyopangwa kufanyika jana April 26, 2018 hayakutokea. Hilo halina mjadala.Na wala si la kushangaza. Kwa nguvu kubwa iliyoonyeshwa na vyombo vya dola juzi, ilihitaji zaidi ya ujasiri kwa mtu kujitokeza mtaani kuandamana.

Ni rahisi kuwalaumu Watanzania kuwa ni watu wa maneno zaidi kuliko vitendo. Japo hilo lina ukweli kwa kiasi flani — na lilipaswa kuzingatiwa wakati wa maandalizi ya maandamano hayo — lakini ukweli unabaki kuwa Magufuli alikuwa keshajiandaa “kunywa damu za waandamanaji.”

Sasa haihitaji uelewa japo mdogo wa tasnia ya mikakati kubaini kwamba kama unafahamu fika kwamba adui yako ametega mabomu njia flani, basi usipite njia hiyo.

Vita yoyote ile inahitaji mikakati. Na mikakati ya vita huwa flexible, kwa maana kwamba inaweza kubadilika muda wowote ule. Na mkakati hujumusha wapangaji wa mkakati husika na watekelezaji wa mkakati huo.

Katika suala la maandamano hayo, mhusika mkuu katika kupanga mikakati ya maandamano hayo alikuwa bloga wa Kitanzanian anayeishi nchini Marekani, Mange Kimambi.

Na watekelezaji wa mikakati ya maandamano hayo walikuwa Watanzania wote wanaoguswa na hali ilivyo huko nyumbani.

Na haijalishi jitihada kubwa kiasi gani zimetumika katika kuandaa mkakati, utekelezaji wake utategemea zaidi mazingira ya wakati husika. Na kubadili mwelekeo wa mkakati ni sehemu ya mafanikio ya mkakati husika.

Kwahiyo, uamuzi wa watu kutojitokeza mtaani kuandamana baada ya kuona kila dalili kuwa kuna mtu ana kiu ya damu zao ulikuwa uamuzi wa busara. Ulipaswa kuwa sehemu ya mikakati ya maandamano hayo.

Kwenye mikakati ya operesheni za kishushushu, kwa mfano, miongoni mwa masuala yanayoangaliwa wakati wa kuandaa operesheni ni “if things go wrong.” Yaani iwapo mambo yatakwenda kinyume na matarajio. Na hapo mkakati unazaa “mpango mbadala” (Plan B).

Muda huu ambapo baadhi ya watu wanaweza kuwa wamehitimisha kuwa wazo la maandamano halikufanikiwa, tungeweza kuwa tuna vilio vikubwa iwapo baadhi ya wenzetu wangeweka kando busara na kujiingiza mtaani na hatimaye kujeruhiwa au kuuwawa.

Haipaswi kulaumiana kuwa “watu wamemwangusha Mange” kwa sababu kimsingi maandamano hayo yalikuwa kwa ajili ya kila Mtanzania anayeitakia mema nchi yetu. Having said that, Mange anastahili pongezi nyingi kwa jitihada kubwa alizofanya kuja na wazo hilo na kulihamasisha kwa nguvu kubwa kabisa.

Kama kuna mapungufu katika mikakati ya maandalizi ya maandamano hayo basi ilikuwa huku ughaibuni. Nadhani kilichochangia kujitokeza kwa watu wachache ni kukosekana “uongozi” katika nchi husika.

Kwamba, watu walitarajiwa wajisukume wenyewe kwenda palipo na ubalozi wa Tanzania katika nchi husika. Kijiografia, mtu anayeishi Uskochi, kwa mfano, pengine ingemlazimu alale London ili aweze kushiriki maandamano hayo saa tatu asubuhi. Kwahiyo, laiti kungekuwa na “uongozi” basi labda ingekubaliwa kuwa badala ya waandamanaji wote kukutana London, ziwepo sehemu nyingine kwa Uskochi, Wales na Eire ya Kaskazini.

Nimeandika kwenye kichwa cha habari kuwa dhamira ya maandamano hayo imefanikiwa. Naam, imefanikiwa kwa sababu kuu mbili. Kwanza, ujumbe umemfikia Magufuli bila hata kuandamana. Na ikumbukwe kuwa ile nguvu kubwa iliyotumika kudhibiti maandamano hayo inamaanisha mabilioni ya shilingi yametumika katika kipindi hiki ambapo serikali ya kidikteta inakabiliwa na hali ngumu mno kifedha.

Pili, soma nukuu hii kutoka kwenye makala niliyoitafsiri kutoka gazeti la kimataifa la Africa Confidential [emoji117]Jarida Maarufu la Kimataifa Lachambua Ubabe wa Magufuli, Maandamano Na "Lamfagilia" Mange ~ Kulikoni Ughaibuni

Haitojalisha hata kama hakuna mtu atayejitokeza kuandamana Aprili 26. Kutoka umbali wa kilomita 26,000, Kimambi tayari ameweza kufanya zaidi ya kutikisa mkia wa chui kwa kutumia simu ya mkononi tu. Na laiti ikitokea asalimisha yeye mwenyewe, mara moja kukamatwa kwake kutakuwa tukio kubwa kabisa litakaloiweka Tanzania kwenye macho na masikio ya dunia nzima.

Naam, Mange amemudu “kumpelekesha” Magufuli na serikali yake nzima, sio kwa kutumia silaha, sio kwa kutumia vitisho, sio kwa kutumia kitu kingine chochote kile zaidi ya POSTS ZA INSTAGRAM. Yaani ni kama Mange ameua tembo kwa ubua. Kafanikiwa kumtetemesha Magufuli mpaka naambiwa huko Dodoma kwenye maadhimisho ya kashindwa kusalimia kwenye gari la wazi.

Sijasikia tathmini ya Mange kuhusu maandamano hayo lakini I hope hatoishia kudhani kuwa Watanzania wamemwangusha kwa vile hawakuingia mitaani kama ilivyokusudiwa.

Kadhalika natumaini hatokata tamaa hasa ikizingatiwa kuwa kwa sie wenye uelewa wa masuala haya, dhamira yake ya maandamano imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kamwe katika historia ya Tanzania hakujawahi kutokea mtu mmoja kuwa na nguvu alizonazo Mange muda huu kiasi kwamba “anamwendesha Magufuli kwa rimoti.” Kuna msemo mmoja kwamba “it is the first to act who controls the game.” The first to act alikuwa Mange na idea ya maandamano.Na kwa hakika amemudu kui-control hiyo game mpaka mwisho.

Naam, maandamano hayakutokea yalivyokusudiwa lakini ujumbe umefika. Magufuli ana hofu kubwa zaidi ya alivyokuwa kabla ya jana.

Itakuwa kosa kubwa sana kuachana na jitihada hizi. Nyerere na wenzake walipoanza mapambano dhidi ya mkoloni hawakufanikiwa kwa siku moja. Hata mtoto akizaliwa haanzi kutembea siku hiyohiyo. Ingekuwa miujiza kama maandamano yangefanyika nchi nzima na Magufuli kuamua kujiuzulu kwa hiari yake.Hii kitu inahitaji jitihada endelevu.

Lakini pengine kubwa zaidi ni haja ya ushirikiano miongoni mwa watu wenye nia ya dhati ya kuung’oa udikteta wa Magufuli. Kila mtu akifanya kivyake, sio tu itamwia rahisi dikteta huyo kuzima jitihada husika bali pia uwezekano wa mafanikio utakuwa mdogo. Umoja ni nguvu.

Nihitimishe makala hii kwa kumpongeza Mange kwa mafanikio ya kihistoria katika suala hili.Ujumbe umefika, and that’s all that matters. Maandamano yalipaswa kuwa symbolic tu, na nina uhakika kuwa mamilioni ya Watanzania wameandamana kimoyomoyo. Changamoto kubwa sasa ni kuhakikisha kuwa kiu ya Watanzania kuung’oa udikteta haipotei.

Naam, watadhihaki kuwa maandamano hayajatokea lakini kile ambacho hawatosema ni kwamba “badala ya wananchi kuandamana, polisi na jeshi ndo walioandamana” tena sio bure bali kwa gharama kubwa kwa serikali iliyo taaban kifedha.
View attachment 758277

Chanzo: “Tathmini: Dhamira Ya ‘Maandamano Ya Mange’ Imefanikiwa” @Chahali

Yeyote anaeamini mange ni shujaaa na amefanikiwa kutimiza azma ya maandamano ya tarehe 26/4/2018 basi mtu huyo ukiwemo rafiki yangu na classmate wangu Chahali, atakua na mapungufu katika bongo lake. Nakushangaa zaidi Chahali kwa sababu, kama ulivyojitangaza kuwa wewe ni "shushushu" (nasikia huwa kwenu hakuna kustaafu always mko kazini), taratibu za kiusalama unazielewa kama kweli ulitumikia idara husika. Tishio lolote la usalama bila kujali limetolewa na nani, kwa kutumia means gani, akiwa eneo gani nk. litachuliwa kwa uzito wake. Ndio mana naamini ulipoanza kazi ya ushushushu kabla hujapewa eneo na wafuasi ulianza kwa kukusanya taarifa hata za udaku ambazo mabosi wako walizifanyia tathmini kabla ya kuzifanyia kazi. Hivyo hivyo, tishio la mange lisingechukuliwa kirahisi kama wengi wenu diaspora mlivyotegemea. Na bahati nzuri mange kutoka na kukosa maarifa katika kupanga strategy alitoa muda mpana wa kufanya risk analysis ya tishio lake la kuhamasisha mapinduzi ya kumoundoa rais aliyechaguliwa kidemokrasia na watanzania. Risks analysis ilitoa taswira ya scale of impact kama maandamano hayo yangefanyika na kutimiza lengo lake kusudiwa. Katika hali kama hiyo, ni wapambe na washabiki wa mange tu kama wewe Chahali pamoja na vyombo vya habari vya magharibi ambavyo sisi wenye upeo wa uandishi tunaelewa "what makes news" and "what makes the headlines", ambao wangefurahia mapinduzi ya mange yafanikiwe. Law enforcement walitimiza wajibu wao na response yao ilitokana na tathmini ya tishio husika. Inaeleweka nyuma ya mange wapo akina chahali na baadhi ya nchi ambazo mmejificha diaspora. Swali dogo tu, mapinduzi yangetimia, jee, ni mange angekua kiongozi wa nchi ya Tanzania? Kinachosikitisha ni kuona watu aina ya Chahali mnamchukulia mange kama shujaa. Hamasa inawafanya mpoteze fahamu kwa muda, katika hali ya kawaida hakuna mwenye akili timamu na busara angekuwa tayari kuji-associate na mange kutokana na namna alivyotumia matusi, kejeli n.k kwa watanzania wakiwemo viongozi wa serikali na madhehebu mbali mbali ya kidini. Historia haijatuonyesha wanaharakati waliotumia matusi kuleta ukombozi mlioutarajia kutoka kwa mange. Historia inatuonyesha harakati za wanaharakati waliofanya mambo makubwa bila kutumia matusi miongoni mwao ni Martin Luther, Nelson Mandela, Fredric Douglas, Che Guevara, Mao Zedong, Mahatma Ghandhi na wengine wengi waliosadia kufanyika mabadiliko katika nchi zao. Wapo waliopata umaarufu mkubwa just for 'long march' (Mao), waliopata umarufu na kuleta mabadiliko makubwa kwa kutumia kalamu zao (Fredric Douglas - USA), walioleta mabadiliko kwa kugoma kula (Bagat Sing - India) na waliotumia non-violence kama Mahtma Gandhi. Hawa wote ukisoma historia zao hawakutumia matusi dhidi ya watawala na viongozi wa kidini kuwaunganisha watu ili kuondoa tawala zilizokuwepo kwanye nchi zao. So katika hali kama hiyo ni type ya akina Chahali na wengine wenye upeo finyu wa kuchambua mambo na wenye mihemko ndio wanaweza kusimama na mange kimambi kwenye mambo ya msingi hasa yenye maslahi mapana kwa taifa na vizazi vya leo na kesho. Ndio hao hao ambao wanaamini mange kafanikiwa katika hili - MNAJIPOTOSHA NA KUPOTOSHA WANAOWASHABIKIA KATIKA HILI - TRY TO BE HONEST KWA KUWAAMBIA WAFUASI WENU MKAE CHINI KUREKEBISHA MLIPO MESS UP ILI MJIPANGE VIZURI MFANIKIWE NEXT TIME.
 
Kitengo cha Mtukufu malaika toka chato kuogopa kivuli cha mange ambaye yupo Mbali USA ni Dalili kuwa Mtukufu sasa ametambua Udhaifu wake na ubaya wake pia atazinduka toka kwenye Dimbwi la kutekwa Akili na Maliyamungu Bashite ambaye ni mshauri wake mkuu wa mambo ya hovyo hovyo ikiwemo kuchukua pesa Hazina kupiga Dili hovyo hovyo zisizo na tija kwa Taifa.
 
Hii tathmini naona kama haijazingatia malengo ya tukio husika.
Malengo ya maandamano yalikua ni kumtoa rais madarakani hili halijafanikiwa na kama ndilo lengo kuu maana yake maandamano hayajafanikiwa.
Tukisema yamefanikiwa tutakua tunawaaminisha watanzania kwamba maandamano yoyote yakiitishwa wakae tu nyumbani halafu yatakua yamefanikiwa na watakua wamepata wanachokitaka.
Mimi naona maandamano hayakufanikiwa kabisa na yanaweza kusababisha kusiwe na maandamano kabisa siku zijazo.
Yakiitishwa maandamano tena tutakaanyumbani halafu kesho yake tutakuja na tathmini maandamano yamefanikiwa sana.
Mungu atufungue akili tuwaze sawasawa na akili zetu.
 
Utaandika mpaka vidole viote sugu na hamtafanikiwa kivunja amani ya nchi hii. Endeleeni kutumika hivyohvyo
 
Serikali ndio isikilize hoja za wananchi...Mange hakusanyi kodi..Kilaza nini wewe?

TRA kila siku wanasema wamevuka lengo..kumbe wanaongeza sifuri mbele...

Serikali ya CCM na Jiwe lenu mmeuwa uchumi

Mnajibu hoja kwa bunduki?

Iko wapi 1.5 Trillioni wewe?

Unatetea mafisadi wa awamu ya 5?

Serikali inakusanya kodi....Itatue hayo matatizo....

Watu wanapaza sauti kwa njia ya mitandao ya Jamii na hata ikibidi maandamano

Eti anafungia mitandao ya jamii kama china, ila mafisadi wanakula bata mitaani...Shame on you
Sasa na wewe maneno mengii ya nini? Ukiambiwa na da'Mange utokee mtaani unaufyata. Afande Muroto keshawapiga mkwara nyie.
 


Hata kama Mange hakufanikiwa kwenye lengo lake ila madhara aliyo sababisha kwa kuchafua taswira ya utawala wa Magufuli kwenye media za nje ni kubwa sana! Hapo hujaweka hesabu ya rasilimali watu, fedha, muda nk vilivyotumika kudhibiti maandamano "hewa"!
 
Ndefu mno ndani imejaa takataka tu, zoezi lililo Shindwa linapambwa lionekane ushindi, ni mazuzu pekee watakubaliana na ujinga huu.
Mange mwenyewe anajuta, haamini mlichomtenda
Well said walahi
Watu wa nyuzi za namna hii haya huwa kisogoni walahi
 


Hata kama Mange hakufanikiwa kwenye lengo lake ila madhara aliyo sababisha kwa kuchafua taswira ya utawala wa Magufuli kwenye media za nje ni kubwa sana! Hapo hujaweka hesabu ya rasilimali watu, fedha, muda nk vilivyotumika kudhibiti maandamano "hewa"!

Hahahaha
Umesahau ya MWAMSHO naona, na rais bado akaendelea!
Jamani dunia haina muda na kuhangaika na vinyago vichache visivyo na kazi na kubangaiza ili kuweka mkono kinywani DUH WALAHI! Someni alama za nyakati!
 


Hata kama Mange hakufanikiwa kwenye lengo lake ila madhara aliyo sababisha kwa kuchafua taswira ya utawala wa Magufuli kwenye media za nje ni kubwa sana! Hapo hujaweka hesabu ya rasilimali watu, fedha, muda nk vilivyotumika kudhibiti maandamano "hewa"!
chadema jaribuni kuratibu maandamano mengine tena. Haya, kama ilivyokuwa kwa ukuta yameangukia pua. Mtajifariji kutwa nzima lakini haisaidii. 2020 inakaribia.
 
Kwani dhamira ilikuwa ujumbe au kumtoa Rais ikulu? Mbona mnabadili topic baada ya kushindwa? Kwani huko Marekani aliko huyo mzaa na babake kuna watz wawili tu? Mbona hata hakuweza kuwashawishi hata wa huko kumuunga mkono? Acheni kubadili topic, hii kiki imeshindwa kuwasha pikipiki.
 
Back
Top Bottom