Tathmini: Dhamira ya "maandamano ya Mange" imefanikiwa

Tathmini: Dhamira ya "maandamano ya Mange" imefanikiwa

Tusifinye akili zetu,tufikiri kwa kina,kwa taifa au mataifa haya kutii maandamano mtandaoni uliona wapi? Wangapi wana access social media? Alijua itakuwa hivyo tu,sasa wewe unaesema anajuta,amejuta wapi! Alichokitarajia ndicho hicho. Wewe unalima kwenye kukoto utarajie uvune mazao mazuri,wapi na wapi!
 
Huwa nahofia zaidi PROCESS kuliko EVENT.
Tunaweza kusema kwa uhakika kabisa Kuwa EVENT haikutokea lakini je tunaweza kusema kwa uhakika kabisa Kuwa PROCESS imeshindwa?

Je Mange kapoteza BATTLE au kapoteza WAR?
Kula tano. Hiyo ni filosofia nzito sana.
 
mkuu kama una akili umeshajua watanzania wengi tunakubali kasi na utendaji wa magufuli hapa kazi tu
Akili zake kazitia mfukoni huyo. Anataka kulazimisha watanzania tuliomchagua Magufuli (ambao ndio wengi) tufikirie kama yeye. Ha ha ha.
 
Sijui kama ujumbe ulikuwa unawakilishwa bila ya support ya watu na ikaonekana hiyo ni hali mutual kwa watanzania wote. Mtu anaweza kuwa hampendi rais akaamua kuandaa maandamano ya kuwasemea watu ambao wao hawakuonyesha kwa lolote kukubaliana na hilo. Mimi najua London kuna watz kibao siyo wale saba tulio waona, Sweden ndiyo usiseme sasa huko ulaya watu hawafiki 100 waliogopa nini ?. Tanzania yenye 55 mil inasemewa na watu waliyopo out of the country less than one class la primary school. Madai yao yalikuwa watandamana non stop mpaka aondoke madarakani sasa leo mbona kimya. Sidhani kama nakubaliana na dhana ya kusema aondoke madarakani , hata ningeunga mkono maandamano nisinge taka hilo. Mimi nataka mjadala mkubwa wa rasimu ya katiba ya Warioba urudi na siyo hayo ya uhuru wa kusema ambao tunao. Watu wanakufa au wanapigwa risasi nani ametuonyesha proof kuwa ni serikali inawapiga? Huu upinzani wenyewe wa kichokoraa hakuna la maana wanalofanya wanakula pesa za kodi kuliko wata serikali unamkabidhi nani gurudumu la maendeleo watu hawawezi kuendeshwa kinyumbu wakaandamana kwa kitu kisicho wadhuru direct. Siyo watanzania tafuteni pengine sisi tunataka katiba mpya ili haya mema anayofanya Rais yaweze kuwa sustainable na mabaya yake tujaribu kuyapunguza kwa kupunguza mamlaka makubwa aliyowekewa hata yeye Rais atakuelewa kuliko mapinduzi ya Mange. Maana kusema kafikisha ujumbe kwani lengo ni ujumbe kufika au Rais kujiuzulu au umesahau lengo kuu la maandamano.

mkuu sijakuelewa unamaanisha mabaya yote yanayofanywa na prezidaa ni kwasababu amepewa mamlaka makubwa ? I think that nigger is evil and very selfish.....hilo la kwanza la pili unataka kusema watu wanaouliwa au kutekwa au kufanywa mambo hayaeleweki sio serikali ? we ni mtanzania wa wapi ? unataka proof gani ? jamaa mbona vitu viko obvious sana ? mtu akimsema magufuli kidogo tu ambayo sio kosa kikatiba anatengenezewa kesi wanaenda kumpiga brush mkunduni , these people are evil...kina roma wamepigwa brush mkunduni na kina bashite saivi wametulia kama nini...unataka proof gani ?
 
mkuu sijakuelewa unamaanisha mabaya yote yanayofanywa na prezidaa ni kwasababu amepewa mamlaka makubwa ? I think that nigger is evil and very selfish.....hilo la kwanza la pili unataka kusema watu wanaouliwa au kutekwa au kufanywa mambo hayaeleweki sio serikali ? we ni mtanzania wa wapi ? unataka proof gani ? jamaa mbona vitu viko obvious sana ? mtu akimsema magufuli kidogo tu ambayo sio kosa kikatiba anatengenezewa kesi wanaenda kumpiga brush mkunduni , these people are evil...kina roma wamepigwa brush mkunduni na kina bashite saivi wametulia kama nini...unataka proof gani ?
Halafu dada yenu Mange akiwaambia mtokee barabarani mnaufyata mkia na kujichimbia chini kwa uoga, ha ha ha.
 
Mange has succeeded to show the world that the government is oppressive, brutal and intolerant to free speach and expression against Tanzanian constitution. Furthermore it has shown that Tanzanians can protest outside the country peacefully but not in the country. Nomaaaa
 
Ndefu mno ndani imejaa takataka tu, zoezi lililo Shindwa linapambwa lionekane ushindi, ni mazuzu pekee watakubaliana na ujinga huu.
Mange mwenyewe anajuta, haamini mlichomtenda
kama hata kusoma hizo paragraph chache umeshindwa! utaweza kuelewa mantik wewe
 
ni busara kubwa iliotumika kwa watu kutojitokeza kuandamana. serikali imefaulu kuwahakikishia watu kuwa imaweza kuzuia maandamano. naamini ina takwimu ya idadi kubwa ya watu walio kuwa waandamane na kuepusha aibu hii imetumia gharama kubwa sana, matokeo yaliyo mpaisha mange.
 
Exactly! Hapa ndo ninaamini ule usemi kuwa Watanzania ni wavivu wa kusoma. Sasa makala ya kusoma under five minutes maximum mtu anaamua kuikacha ila ingekuwa stori za dhahania juu ya kisa cha mapenzi hata page 10 angesoma
Halafu cha kusikitisha zaidi ni kuwa mtu huyu anaweza kuwa ni kiongozi ambaye anategemewa kuwaongoza Watz kutoka kwenye maadui wakuu wa Mtz,au anaweza kuwa ni mlinzi aliyeaminiwa kulinda rasilimali,ulinzi na usalama wetu!
 
Kwanza nikiona mtu anataja taja miji ya huko ulaya na kuonyesha kuitukuza eti wameandamana huko Uskochi.sijui mnaona sifa?mtu kuponda nchi yake akiwa ndani ya nchi nyingine huko tena nchi za wanyonyaji ni ujinga tu.hao wote walioko huko ni watumwa wa fikla na wazungu watakua waliwadharau sana,mtatuijia humu na maneno ua kiswa-english mnadhani ndiyo tutawaona mnafaa msemayo kuliko mnaowashutumu?mburulaz kabisa
 
Maandamano yaliyopangwa kufanyika jana April 26, 2018 hayakutokea. Hilo halina mjadala.Na wala si la kushangaza. Kwa nguvu kubwa iliyoonyeshwa na vyombo vya dola juzi, ilihitaji zaidi ya ujasiri kwa mtu kujitokeza mtaani kuandamana.

Ni rahisi kuwalaumu Watanzania kuwa ni watu wa maneno zaidi kuliko vitendo. Japo hilo lina ukweli kwa kiasi flani — na lilipaswa kuzingatiwa wakati wa maandalizi ya maandamano hayo — lakini ukweli unabaki kuwa Magufuli alikuwa keshajiandaa “kunywa damu za waandamanaji.”

Sasa haihitaji uelewa japo mdogo wa tasnia ya mikakati kubaini kwamba kama unafahamu fika kwamba adui yako ametega mabomu njia flani, basi usipite njia hiyo.

Vita yoyote ile inahitaji mikakati. Na mikakati ya vita huwa flexible, kwa maana kwamba inaweza kubadilika muda wowote ule. Na mkakati hujumusha wapangaji wa mkakati husika na watekelezaji wa mkakati huo.

Katika suala la maandamano hayo, mhusika mkuu katika kupanga mikakati ya maandamano hayo alikuwa bloga wa Kitanzanian anayeishi nchini Marekani, Mange Kimambi.

Na watekelezaji wa mikakati ya maandamano hayo walikuwa Watanzania wote wanaoguswa na hali ilivyo huko nyumbani.

Na haijalishi jitihada kubwa kiasi gani zimetumika katika kuandaa mkakati, utekelezaji wake utategemea zaidi mazingira ya wakati husika. Na kubadili mwelekeo wa mkakati ni sehemu ya mafanikio ya mkakati husika.

Kwahiyo, uamuzi wa watu kutojitokeza mtaani kuandamana baada ya kuona kila dalili kuwa kuna mtu ana kiu ya damu zao ulikuwa uamuzi wa busara. Ulipaswa kuwa sehemu ya mikakati ya maandamano hayo.

Kwenye mikakati ya operesheni za kishushushu, kwa mfano, miongoni mwa masuala yanayoangaliwa wakati wa kuandaa operesheni ni “if things go wrong.” Yaani iwapo mambo yatakwenda kinyume na matarajio. Na hapo mkakati unazaa “mpango mbadala” (Plan B).

Muda huu ambapo baadhi ya watu wanaweza kuwa wamehitimisha kuwa wazo la maandamano halikufanikiwa, tungeweza kuwa tuna vilio vikubwa iwapo baadhi ya wenzetu wangeweka kando busara na kujiingiza mtaani na hatimaye kujeruhiwa au kuuwawa.

Haipaswi kulaumiana kuwa “watu wamemwangusha Mange” kwa sababu kimsingi maandamano hayo yalikuwa kwa ajili ya kila Mtanzania anayeitakia mema nchi yetu. Having said that, Mange anastahili pongezi nyingi kwa jitihada kubwa alizofanya kuja na wazo hilo na kulihamasisha kwa nguvu kubwa kabisa.

Kama kuna mapungufu katika mikakati ya maandalizi ya maandamano hayo basi ilikuwa huku ughaibuni. Nadhani kilichochangia kujitokeza kwa watu wachache ni kukosekana “uongozi” katika nchi husika.

Kwamba, watu walitarajiwa wajisukume wenyewe kwenda palipo na ubalozi wa Tanzania katika nchi husika. Kijiografia, mtu anayeishi Uskochi, kwa mfano, pengine ingemlazimu alale London ili aweze kushiriki maandamano hayo saa tatu asubuhi. Kwahiyo, laiti kungekuwa na “uongozi” basi labda ingekubaliwa kuwa badala ya waandamanaji wote kukutana London, ziwepo sehemu nyingine kwa Uskochi, Wales na Eire ya Kaskazini.

Nimeandika kwenye kichwa cha habari kuwa dhamira ya maandamano hayo imefanikiwa. Naam, imefanikiwa kwa sababu kuu mbili. Kwanza, ujumbe umemfikia Magufuli bila hata kuandamana. Na ikumbukwe kuwa ile nguvu kubwa iliyotumika kudhibiti maandamano hayo inamaanisha mabilioni ya shilingi yametumika katika kipindi hiki ambapo serikali ya kidikteta inakabiliwa na hali ngumu mno kifedha.

Pili, soma nukuu hii kutoka kwenye makala niliyoitafsiri kutoka gazeti la kimataifa la Africa Confidential [emoji117]Jarida Maarufu la Kimataifa Lachambua Ubabe wa Magufuli, Maandamano Na "Lamfagilia" Mange ~ Kulikoni Ughaibuni

Haitojalisha hata kama hakuna mtu atayejitokeza kuandamana Aprili 26. Kutoka umbali wa kilomita 26,000, Kimambi tayari ameweza kufanya zaidi ya kutikisa mkia wa chui kwa kutumia simu ya mkononi tu. Na laiti ikitokea asalimisha yeye mwenyewe, mara moja kukamatwa kwake kutakuwa tukio kubwa kabisa litakaloiweka Tanzania kwenye macho na masikio ya dunia nzima.

Naam, Mange amemudu “kumpelekesha” Magufuli na serikali yake nzima, sio kwa kutumia silaha, sio kwa kutumia vitisho, sio kwa kutumia kitu kingine chochote kile zaidi ya POSTS ZA INSTAGRAM. Yaani ni kama Mange ameua tembo kwa ubua. Kafanikiwa kumtetemesha Magufuli mpaka naambiwa huko Dodoma kwenye maadhimisho ya kashindwa kusalimia kwenye gari la wazi.

Sijasikia tathmini ya Mange kuhusu maandamano hayo lakini I hope hatoishia kudhani kuwa Watanzania wamemwangusha kwa vile hawakuingia mitaani kama ilivyokusudiwa.

Kadhalika natumaini hatokata tamaa hasa ikizingatiwa kuwa kwa sie wenye uelewa wa masuala haya, dhamira yake ya maandamano imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kamwe katika historia ya Tanzania hakujawahi kutokea mtu mmoja kuwa na nguvu alizonazo Mange muda huu kiasi kwamba “anamwendesha Magufuli kwa rimoti.” Kuna msemo mmoja kwamba “it is the first to act who controls the game.” The first to act alikuwa Mange na idea ya maandamano.Na kwa hakika amemudu kui-control hiyo game mpaka mwisho.

Naam, maandamano hayakutokea yalivyokusudiwa lakini ujumbe umefika. Magufuli ana hofu kubwa zaidi ya alivyokuwa kabla ya jana.

Itakuwa kosa kubwa sana kuachana na jitihada hizi. Nyerere na wenzake walipoanza mapambano dhidi ya mkoloni hawakufanikiwa kwa siku moja. Hata mtoto akizaliwa haanzi kutembea siku hiyohiyo. Ingekuwa miujiza kama maandamano yangefanyika nchi nzima na Magufuli kuamua kujiuzulu kwa hiari yake.Hii kitu inahitaji jitihada endelevu.

Lakini pengine kubwa zaidi ni haja ya ushirikiano miongoni mwa watu wenye nia ya dhati ya kuung’oa udikteta wa Magufuli. Kila mtu akifanya kivyake, sio tu itamwia rahisi dikteta huyo kuzima jitihada husika bali pia uwezekano wa mafanikio utakuwa mdogo. Umoja ni nguvu.

Nihitimishe makala hii kwa kumpongeza Mange kwa mafanikio ya kihistoria katika suala hili.Ujumbe umefika, and that’s all that matters. Maandamano yalipaswa kuwa symbolic tu, na nina uhakika kuwa mamilioni ya Watanzania wameandamana kimoyomoyo. Changamoto kubwa sasa ni kuhakikisha kuwa kiu ya Watanzania kuung’oa udikteta haipotei.

Naam, watadhihaki kuwa maandamano hayajatokea lakini kile ambacho hawatosema ni kwamba “badala ya wananchi kuandamana, polisi na jeshi ndo walioandamana” tena sio bure bali kwa gharama kubwa kwa serikali iliyo taaban kifedha.
View attachment 758277

Chanzo: “Tathmini: Dhamira Ya ‘Maandamano Ya Mange’ Imefanikiwa” @Chahali

Unapofanya Tathmini usichanganye na personal insinuation zako.

Sijui tathmini yako na wale wote mnaoshikilia bango juu ya gari la wazi, mnaongeleaje juu ya Raisi kushuka jukwaani na kwenda kuwasalimia wananchi kwa kuwasika mikono Na kuwapungia kwa ukaribu???

MAGUFULI sio Muoga Na hatetemeki kama alivyotetemeka Mange akiongea na VOA pale Embassy!
 
Unafikiri maandamano yaliyoratibiwa na da'Mange na chadema ndio yangetatua haya matatizo?

Serikali ndio isikilize hoja za wananchi...Mange hakusanyi kodi..Kilaza nini wewe?

TRA kila siku wanasema wamevuka lengo..kumbe wanaongeza sifuri mbele...

Serikali ya CCM na Jiwe lenu mmeuwa uchumi

Mnajibu hoja kwa bunduki?

Iko wapi 1.5 Trillioni wewe?

Unatetea mafisadi wa awamu ya 5?

Serikali inakusanya kodi....Itatue hayo matatizo....

Watu wanapaza sauti kwa njia ya mitandao ya Jamii na hata ikibidi maandamano

Eti anafungia mitandao ya jamii kama china, ila mafisadi wanakula bata mitaani...Shame on you
 
Back
Top Bottom