Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,116
- 4,773
Maandamano yaliyopangwa kufanyika jana April 26, 2018 hayakutokea. Hilo halina mjadala.Na wala si la kushangaza. Kwa nguvu kubwa iliyoonyeshwa na vyombo vya dola juzi, ilihitaji zaidi ya ujasiri kwa mtu kujitokeza mtaani kuandamana.
Ni rahisi kuwalaumu Watanzania kuwa ni watu wa maneno zaidi kuliko vitendo. Japo hilo lina ukweli kwa kiasi flani — na lilipaswa kuzingatiwa wakati wa maandalizi ya maandamano hayo — lakini ukweli unabaki kuwa Magufuli alikuwa keshajiandaa “kunywa damu za waandamanaji.”
Sasa haihitaji uelewa japo mdogo wa tasnia ya mikakati kubaini kwamba kama unafahamu fika kwamba adui yako ametega mabomu njia flani, basi usipite njia hiyo.
Vita yoyote ile inahitaji mikakati. Na mikakati ya vita huwa flexible, kwa maana kwamba inaweza kubadilika muda wowote ule. Na mkakati hujumusha wapangaji wa mkakati husika na watekelezaji wa mkakati huo.
Katika suala la maandamano hayo, mhusika mkuu katika kupanga mikakati ya maandamano hayo alikuwa bloga wa Kitanzanian anayeishi nchini Marekani, Mange Kimambi.
Na watekelezaji wa mikakati ya maandamano hayo walikuwa Watanzania wote wanaoguswa na hali ilivyo huko nyumbani.
Na haijalishi jitihada kubwa kiasi gani zimetumika katika kuandaa mkakati, utekelezaji wake utategemea zaidi mazingira ya wakati husika. Na kubadili mwelekeo wa mkakati ni sehemu ya mafanikio ya mkakati husika.
Kwahiyo, uamuzi wa watu kutojitokeza mtaani kuandamana baada ya kuona kila dalili kuwa kuna mtu ana kiu ya damu zao ulikuwa uamuzi wa busara. Ulipaswa kuwa sehemu ya mikakati ya maandamano hayo.
Kwenye mikakati ya operesheni za kishushushu, kwa mfano, miongoni mwa masuala yanayoangaliwa wakati wa kuandaa operesheni ni “if things go wrong.” Yaani iwapo mambo yatakwenda kinyume na matarajio. Na hapo mkakati unazaa “mpango mbadala” (Plan B).
Muda huu ambapo baadhi ya watu wanaweza kuwa wamehitimisha kuwa wazo la maandamano halikufanikiwa, tungeweza kuwa tuna vilio vikubwa iwapo baadhi ya wenzetu wangeweka kando busara na kujiingiza mtaani na hatimaye kujeruhiwa au kuuwawa.
Haipaswi kulaumiana kuwa “watu wamemwangusha Mange” kwa sababu kimsingi maandamano hayo yalikuwa kwa ajili ya kila Mtanzania anayeitakia mema nchi yetu. Having said that, Mange anastahili pongezi nyingi kwa jitihada kubwa alizofanya kuja na wazo hilo na kulihamasisha kwa nguvu kubwa kabisa.
Kama kuna mapungufu katika mikakati ya maandalizi ya maandamano hayo basi ilikuwa huku ughaibuni. Nadhani kilichochangia kujitokeza kwa watu wachache ni kukosekana “uongozi” katika nchi husika.
Kwamba, watu walitarajiwa wajisukume wenyewe kwenda palipo na ubalozi wa Tanzania katika nchi husika. Kijiografia, mtu anayeishi Uskochi, kwa mfano, pengine ingemlazimu alale London ili aweze kushiriki maandamano hayo saa tatu asubuhi. Kwahiyo, laiti kungekuwa na “uongozi” basi labda ingekubaliwa kuwa badala ya waandamanaji wote kukutana London, ziwepo sehemu nyingine kwa Uskochi, Wales na Eire ya Kaskazini.
Nimeandika kwenye kichwa cha habari kuwa dhamira ya maandamano hayo imefanikiwa. Naam, imefanikiwa kwa sababu kuu mbili. Kwanza, ujumbe umemfikia Magufuli bila hata kuandamana. Na ikumbukwe kuwa ile nguvu kubwa iliyotumika kudhibiti maandamano hayo inamaanisha mabilioni ya shilingi yametumika katika kipindi hiki ambapo serikali ya kidikteta inakabiliwa na hali ngumu mno kifedha.
Pili, soma nukuu hii kutoka kwenye makala niliyoitafsiri kutoka gazeti la kimataifa la Africa Confidential [emoji117]Jarida Maarufu la Kimataifa Lachambua Ubabe wa Magufuli, Maandamano Na "Lamfagilia" Mange ~ Kulikoni Ughaibuni
Haitojalisha hata kama hakuna mtu atayejitokeza kuandamana Aprili 26. Kutoka umbali wa kilomita 26,000, Kimambi tayari ameweza kufanya zaidi ya kutikisa mkia wa chui kwa kutumia simu ya mkononi tu. Na laiti ikitokea asalimisha yeye mwenyewe, mara moja kukamatwa kwake kutakuwa tukio kubwa kabisa litakaloiweka Tanzania kwenye macho na masikio ya dunia nzima.
Naam, Mange amemudu “kumpelekesha” Magufuli na serikali yake nzima, sio kwa kutumia silaha, sio kwa kutumia vitisho, sio kwa kutumia kitu kingine chochote kile zaidi ya POSTS ZA INSTAGRAM. Yaani ni kama Mange ameua tembo kwa ubua. Kafanikiwa kumtetemesha Magufuli mpaka naambiwa huko Dodoma kwenye maadhimisho ya kashindwa kusalimia kwenye gari la wazi.
Sijasikia tathmini ya Mange kuhusu maandamano hayo lakini I hope hatoishia kudhani kuwa Watanzania wamemwangusha kwa vile hawakuingia mitaani kama ilivyokusudiwa.
Kadhalika natumaini hatokata tamaa hasa ikizingatiwa kuwa kwa sie wenye uelewa wa masuala haya, dhamira yake ya maandamano imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kamwe katika historia ya Tanzania hakujawahi kutokea mtu mmoja kuwa na nguvu alizonazo Mange muda huu kiasi kwamba “anamwendesha Magufuli kwa rimoti.” Kuna msemo mmoja kwamba “it is the first to act who controls the game.” The first to act alikuwa Mange na idea ya maandamano.Na kwa hakika amemudu kui-control hiyo game mpaka mwisho.
Naam, maandamano hayakutokea yalivyokusudiwa lakini ujumbe umefika. Magufuli ana hofu kubwa zaidi ya alivyokuwa kabla ya jana.
Itakuwa kosa kubwa sana kuachana na jitihada hizi. Nyerere na wenzake walipoanza mapambano dhidi ya mkoloni hawakufanikiwa kwa siku moja. Hata mtoto akizaliwa haanzi kutembea siku hiyohiyo. Ingekuwa miujiza kama maandamano yangefanyika nchi nzima na Magufuli kuamua kujiuzulu kwa hiari yake.Hii kitu inahitaji jitihada endelevu.
Lakini pengine kubwa zaidi ni haja ya ushirikiano miongoni mwa watu wenye nia ya dhati ya kuung’oa udikteta wa Magufuli. Kila mtu akifanya kivyake, sio tu itamwia rahisi dikteta huyo kuzima jitihada husika bali pia uwezekano wa mafanikio utakuwa mdogo. Umoja ni nguvu.
Nihitimishe makala hii kwa kumpongeza Mange kwa mafanikio ya kihistoria katika suala hili.Ujumbe umefika, and that’s all that matters. Maandamano yalipaswa kuwa symbolic tu, na nina uhakika kuwa mamilioni ya Watanzania wameandamana kimoyomoyo. Changamoto kubwa sasa ni kuhakikisha kuwa kiu ya Watanzania kuung’oa udikteta haipotei.
Naam, watadhihaki kuwa maandamano hayajatokea lakini kile ambacho hawatosema ni kwamba “badala ya wananchi kuandamana, polisi na jeshi ndo walioandamana” tena sio bure bali kwa gharama kubwa kwa serikali iliyo taaban kifedha.
Chanzo: “Tathmini: Dhamira Ya ‘Maandamano Ya Mange’ Imefanikiwa” @Chahali