Tathimini: Siku 10 za kampeni ya Dr. John Magufuli

Tathimini: Siku 10 za kampeni ya Dr. John Magufuli

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Posts
1,644
Reaction score
709
COEGxgzUYAAUWwc.jpg


TATHMINI; siku 10 za Kampeni ya Dr John Magufuli.

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Pombe Magufuli amehitimisha mzunguko wa Kwanza wa Kampeni yake kwa mikoa 6 ya kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kusini ambayo ni KATAVI, RUKWA, MBEYA, NJOMBE, RUVUMA na MTWARA.

Katika kampeni zake Dr Magufuli amefanya mikutano ya hadhara takribani 49 pamoja na mikutano midogo ya kusalimia wananchi zaidi ya 126 ambapo katika mikutano yote wananchi walijitokeza kwa Maelfu kumsikiliza akiwasilisha Ilani ya CCM ya 2015-2020.

Dr Magufuli ametembea takribani Kilometa 5,900 kwa kutumia gari na maeneo mengine akitembea kwa miguu ili kukutana na Wananchi wa Makundi mbalimbali akinadi sera za CCM.

Tafiti za awali za Mashirika mbalimbali ya nje na ndani ya nchi yalionyesha kuwa CCM itashinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa zaidi ya asilimia 60, lakini baada ya kuanza kwa Kampeni na mgombea kuzunguka akifanya mikutano mikubwa ya hadhara ambayo imekuwa ikirushwa moja kwa moja (live) kupitia vituo mbalimbali vya televisheni, magazeti, redio pamoja na mitandao ya kijamii na kuwafikia watanzania takribani milioni 30, Umaarufu wa CCM na uwezekano wa kushinda umeongezeka kufikia asilimia 85 (tafiti za ndani)

Mambo yaliyopelekea CCM kuongeza umaarufu wake ni pamoja na rekodi nzuri ya uadilifu na uchapakazi aliyonayo mgombea wake, pamoja na uwezo mkubwa wa mgombea (Dr Magufuli) katika kutambua na kutoa suluhu ya matatizo yanayowakabili wananchi wa kada zote na maeneo yote ya Mijini na Vijijini.

Ilani ya CCM na namna mgombea anavyoinadi (Body language) imeongeza imani ya wananchi kwa CCM, mfano Dr Magufuli akisema anaichukia rushwa, mwili, haiba na sura yake vinaonyesha kuwa anamaanisha anachokizungumza. Ilani ya CCM imejikita katika kuleta mabadiliko kwa kuondoa Umasikini na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa Vijana, kuendeleza Vita dhidi ya Rushwa na Ubadhirifu, Kuboresha huduma za jamii na kuendeleza Umoja wa Kitaifa pamoja na kudumisha Ulinzi na usalama.

Wakati Umaarufu na kukubalika kwa CCM kunaongezeka, bado inapata upinzani hafifu ktk kampeni zake. Rekodi zenye mashaka za wagombea wao zinazohusisha kashfa za rushwa, ufisadi, utendaji mbovu na uzembe. Hali tete na migogoro ya ndani ya vyama vya Upinzani ambayo imeshika kasi ktk kipindi hiki hasa kuhusu wagombea kwa nafasi ya Urais na baadhi ya majimbo. Hali ya Afya za wagombea wao ambazo zimewafanya kutoweza kufika katika baadhi ya maeneo waliyopanga kufanya mikutano mfano Ludewa na Tunduru ambapo wananchi walishakusanyika na mgombea akashindwa kutokea. Vyama vya upinzani kukosa Ilani madhubuti na hivyo wananchi kupunguza imani yao kwao.

NB;
Katika moja ya utaratibu bora kabisa wa Chama Cha Mapinduzi ni ule wa kujifanyia tathmini katika kila hatua ya mpango ama jambo lake lolote, utaratibu huu umeiwezesha CCM kubaki kuwa relevant na kuendelea kuaminiwa na kupendwa na watanzania walio wengi.
 
​ccm ingekuwa ni mwili wa binaadamu tungesha sema figo na ini vimekufa hakuna matumaini ya kupona tena!
 
Eti utafiti unafanywa na UVCCM
 

Attachments

  • 1441434884837.jpg
    1441434884837.jpg
    48.5 KB · Views: 748
Eti utafiti unafanywa na UVCCM
UVCCM like any other organization inacho kitengo imara na bora kinachoshughulika na tafiti za kisiasa ili kujua muelekeo wa siasa za ndani na nje ya nchi. Ni kitengo chenye wataalamu wenye kuaminika na wanaotumainiwa hata na taasisi kubwa za kitaaluma kama University of Dar es salaam.
 
​ccm ingekuwa ni mwili wa binaadamu tungesha sema figo na ini vimekufa hakuna matumaini ya kupona tena!

ukiwa na mawazo finyu lazima utasema tu hivo ila wenye akili zao timamau wanatambua umuhimu wa ccm na magufuli ndani ya taifa la tanzania hao figo na ini waliokufa ni lowassa na sumaye ambao mmewachukua nyinyi na sisi kubadilisha figo mpya ya magufuli ambayo ni safi sana sasa ccm imebaki imara na inasonga mbele kwa kishindo
 
Wakati wa kutangaza nia ulipofika, niliwaambia watu kuwa huyo mnayemuona ana watu wengi na kufanya kampeni kabla ya kampeni kuruhusiwa ni mtu hafai na CCM itasimamisha mtu mwema na si huyo, watu wakanibishia, lakini CCM ilifanya maamuzi ya busara na kumsimamisha Magufuli kama mgombea wa urais kwa hakika walifaulu, na hivi sasa nawaambia watu CCM itashinda kwa kishindo, lakini wanabisha, tusubiri 0ct 25.
 
kama watanzania tutaendele kufwata mikumbo, kukubali kupandikizwa fitna za uongo, basi hatunabudi kujifananisha na wale wapiganaji vita wa maji maji , waliolaghaliwa huku wakifa wakisema maji, tunajichimbi kaburi wenyewe huku tunajiona, ytuzinduke tufanye maamuzi sahihi tusijutie hapo baadae #hapakazitu
 
TandaleOne

Pole baba Kwa kazi nzito...Nina imani na na wewe sanaaa...Kazi unaiweza. Hongera sanaaaa
 
Last edited by a moderator:
sina shaka na uadilifu wa magufuli na utendaji wake pia
 
TandaleOne

Kwa heshima na taadhima napenda kusema magufuli ni hodari wa kila jambo linalohusu maendeleo sina mengi ila nawasihi wakazi wa morogoro tukutane leo tukamsikilize mh sera zake na tumuunge mkono
11659364_423602097827066_5754281488131590984_n.jpg
 
Last edited by a moderator:
kama UKAWA ingekua gari, basi ningesema pia matairi yote yameshapata pancha,hivyo gari limebeki kusukumwa tuu ilimradi liende

Gari siku zote inahitaji service, na ndivyo ilivyo. Huwa tunabadili oil ya engine kwa kutoa oil chafu na kuweka safi, tunabadili matairi yaliyochoka na kuweka mapya, safari hii CCM imekuwa kama gari, imetoa oil chafu imeweka mpya na matair mabovu yaliyochoka yametupwa na kuwekwa mapya, sasa UKAWA eti wakayachukua matairi yaliyochoka na oil chafu na kwenda kuviweka kwenye gari yao ambayo tangu awali ilikuwa mbovu, sasa hapo unategemea nini kama si kuua gari, matokeo yake kondakta kaondoka, dereva haeleweki, mkata tiketi naye hayupo, abiria wamebaki hawajielewi na hawajui pa kwenda, na ndiyo maana wakaiita safari ya matumaini, maana yake ni kwamba, safari ya matumaini kuna kufika au kuishia njiani, sasa naona wameishia njiani na imekuwa safari ya UKIWA.
 
Utafit mzuri sana huu. Unatupa picha kamili ya kile kitakachotokea baada ya tarehe 25. CCM oyeee
 
​ccm ingekuwa ni mwili wa binaadamu tungesha sema figo na ini vimekufa hakuna matumaini ya kupona tena!

CCM Imetoa ini na figo na kufanya transplant kwa kuweka ini na figo mpya, ila kuna watu wamechukua figo na ini lililotoka CCM na kwenda kuharibu miili yao,
 
Ninachoona ni maendeleo yanakuja ndani ya Magufuli #hapakazitu
 
Back
Top Bottom