Kuna vitu vingine umetia ushabiki usio na maana eti watu wanachangia wembe! Husituingize kwenye umburula wako hapa.....hivi mbagala utalinganisha na vingunguti, buguruni kwa mnyamani, msasani bonde la mpunga, kinondoni mkwajuni nk,,,,unapewa story za kijiweni unaleta jf...sijui unaaishi wapi lkn kama ni sinza sipati tabu kwani ndiyo wale mnaohamka asubuhi na kutafuta poda kwanza kabla ya pesa na kwenda vijiweni kuzungumzia mbagala.....hawa ndiyo wale wanalala buguruni anashinda masaki
10.napia ndo waasisi wa vigodoro , mchiriku .
sinza kivp mbona unampa manyota!anakaa msasani bonde la mpunga akiwasikiaga mamlaka ya hali ya hewa huwa mavi yanamtoka
11.Bila kuwa baunsa hupandi daladala za mbagala!
si kweliWiki hii nilipata fursa ya kupita mbagala na kuzungukia mitaa michache na hiki ndio nilichokiona;
1.Kwa wenyeji Mbagala hujulikana zaid kama "Mbajala"
2.Mbagala ina watu wengi sana na pilikapilika ni nyingi sana.
3.Nyumba nyingi zimetenganishwa na njia na vipenyo finyu sana lakini ndani kuna sofa! sijui hata hizo sofa zinapitaje
4.Kuna ujamaa sana watu bado wanachangia matumiz ya vitu mbalimbali nimekuta jamaa watano wamejipanga kwa kinyozi wanahudumiwa kwa wembe mmoja!
5.Kuna ukaribu baina ya watu kiasi kwamba watu wanafahamiana, kama ni mgeni utajulikana tu.
6.Kuna biashara kubwa ya vitu feki / pirated hasa cd, tv n.k
7.Ofisi ya imamu ni moja ya ofisi muhimu sana pengine kuliko hata ya mjumbe wa mtaa
8.Kuna uwingi wa ofisi za wataalam wa tiba asili pengine kuliko hata maduka ya madawa.
9.Wakazi wa huko hupendelea sana sherehe zinazokwenda kwa majina mbalimbali kama kumtoa mwali, maulidi n.k, sherehe husherekewa kwa shangwe na vigelegele na akina dada na akina mama ambao wengi wao huvalia nguo nyepesi za kuangaza almuradi kila kitu burudani!
Jaman hii ndio Mbagala niliyoiona mimi, Je Mbagala yako ikoje?
si kweli
si kweli
11. Ma VX ya masaki na kwingineko yanapaki kwenye hivyo vichochoro kwa waganga
Unaposema Mbagala unaamanisha eneo gani?.......maana kuna Kijichi, chamazi, mbande, Mbagala Kuu, Mbagala Rangi Tatu Mzinga etc. , Mbagala ni jina la Tarafa
Ni kweli kabisa mbajala ukipita na rav4 mtaani watoto watakushangaa kweli tena kwa vigeregere, ukiwa na elf10 mtaa mzima utaitwa milionea.
Kama cha kula ni 1500 basi maisha ya huko mbagala ni ghali sana...
Maana huku kwetu 1000 unapata wali ndondo, mchicha,nyama vipande viwili yani unakula hadi unaomba mfuko ubebee mwingine utaobakiza..
Kuna vitu vingine umetia ushabiki usio na maana eti watu wanachangia wembe! Husituingize kwenye umburula wako hapa.....hivi mbagala utalinganisha na vingunguti, buguruni kwa mnyamani, msasani bonde la mpunga, kinondoni mkwajuni nk,,,,unapewa story za kijiweni unaleta jf...sijui unaaishi wapi lkn kama ni sinza sipati tabu kwani ndiyo wale mnaohamka asubuhi na kutafuta poda kwanza kabla ya pesa na kwenda vijiweni kuzungumzia mbagala.....hawa ndiyo wale wanalala buguruni anashinda masaki
sinza kivp mbona unampa manyota!anakaa msasani bonde la mpunga akiwasikiaga mamlaka ya hali ya hewa huwa mavi yanamtoka
Unajua watu wengi wamejenga taswira unapotaja Mbagala au hata wilaya ya Temeke, wao huona kama sehemu isiyo na maendeleo, sehemu ya hovyo hovyo tu..........kwa wale msiofahamu Wilaya ya Temeke ni moja kati ya wilaya zenye miundombinu bora zaidi kuliko wilaya nyingi sana hapa nchini. Tarafa ya Mbagala ni moja ya maeneo yenye nyumba za kisasa sana, miundo mbinu bora zaidi kuliko sehemu nyingine. Tuna vyanzo vya maji vya kwetu Biasi na Azimio maji safi ya bomba 24/7.
Hivi sasa ujenzi wa barabara za lami za mitaa unaeendelea, barabara toka rangi 3 kwenda Mbagala kuu inajengwa kiwango cha lami, hivyo hivyo Rangi kwenda Chamazi. Nenda huko Kigamboni, Toangoma nk....hii yote ni Temeke
Katika tarafa ya Mbagala tu acha wilaya ya Temeke kuna zaidi ya mabenki nane na taasisi zote za fedha unazozijua wewe hapa Dar.
Nimeandika haya ili kuwafahamisha watu wengine kuwa ile picha hasi inayoelezwa kuhusu tarafa ya Mbagala na wilaya ya Temeke sio kweli kabisa, huku watu wana enjoy maisha kuliko sehemu kibao hapa Dar. Watu wanasafiri masaa manne kufika posta umbali wa 15kms tu halafu hao hao utawasikia ''Mbagala mbali sana'' wakati Chamazi kwenda Posta ni saa moja tu. Karibuni tarafa ya Mbagala karibuni Wilaya ya Temeke..............