Mwaka 2013 umeanza kwa kuporomoka kwa CHADEMA kisiasa kutokana kwa kushindwa kwa uongozi wa chama husika kuanzisha hoja zenye mshiko kwa maendeleo ya TZ. CHADEMA imejikuta ikijikita katika siasa za majungu, uzushi, manung'uniko,kufukuzana, uwongo, uzandiki pasipo kuonyesha dalili zozote za kumkomboa mtanzania kifikra na kimaendeleo.
Hali ya CHADEMA kisiasa imezidi kuwa mbaya katika ngazi za serikali za mitaa kutokana na tabia ya wabunge na madiwani wao kususia vikao vya mabaraza ya madiwani katika maeneo husika.
Hivyo wananchi wa kata zinazowakilishwa na CHADEMA wamekuwa ni wapweke kwa vile mawazo yao na vipaumbele vyao vimeshindwa kuwekwa katika mipango ya halmashauri kwani madiwani wao wameshindwa kushiriki katika vikao vya maendeleo. Pia wabunge wa CHADEMA wameshindwa kutetea na kulinda maslahi ya wananchi waliowachangua wawapo bungeni kwa vile wamekuwa ni vinara wa kuleta fujo na kususia bunge BADALA ya kuwakilisha vipaumbele vya wapiga kura wao.
Mfano halisi ni Mbunge Tundu Lissu atokaye katika eneo lenye shida kubwa ya maji, ameshindwa kuhudhuria siku ..za uwasilishaji wa bajeti husika, pia mbunge huyu amekuwa ni kinara wa kuwatia ujinga wapiga kura wa jimboni mwake ili wasusie kutoa michango na kushiriki katika shughuli za ujenzi wa taifa. Hizo zote ni kielelezo cha siasa uchwara ndani ya CHADEMA.
Yote kwa yote, matukio yanayofanywa na wawakilishi na viongozi wa CHADEMA imekuwa ni kaburi kwa chama chao kwani siku zinavyokwenda mbele CHADEMA imekosa mashiko kwa wananchi. Viashiria vya kutosha vinajionyesha kuwa CHADEMA itaambualia patupu uchaguzi wa 2014!