TASAF kumuingiza Wassira Ikulu 2015

TASAF kumuingiza Wassira Ikulu 2015

SDP_TZ_Mpya

Senior Member
Joined
Jun 21, 2013
Posts
166
Reaction score
77
Taarifa za kwenye CCM zilithibisha kuwa Wassira yuko 'very serious' kwenye kusaka Urais 2015. Hoja yake ni kuwa yeye ni msafi kuliko akina Lowassa. Kura alizopata NEC na kumfanya aongoze zinamtia wazimu. Anadai Ikulu ya sasa inamkubali na anaweza kutumika ku-neutralise uhasama wa akina Sitta, Membe na Lowassa.

Hata hivyo, imefahamika kuwa kwa sasa ameamua kuikumbatia TASAF iliyo chini ya uratibu wake kuhakikisha inamwingiza Ikulu. Ikumbukwe kuwa TASAF imefika kila kona ya nchi na mbunge na mjumbe wa CCM wilaya lazima ajitahidi kumuunga mkono ndipo mradi wa TASAF uje kwenye eneo lake. Na yeye baadae hutembelea miradi hiyo huku akipokea kiapo cha mpokea mradi cha kumuunga mkono yeye Wassira 2015.

Inajulikana wazi kuwa ni mtindo huu ndio uliompa Wassira kura nyingi wakati wa uchaguzi wa NEC mwaka jana Dodoma. Ukiangalia kutoka pembeni, hakuna tofauti na ufisadi mwingine wowote.
 
maccm bana........hata mfuu anaweza kuwa rais dan ya ccm.
 
Nawaoomba sana CCM msimamisheni Wasira, he..hee.
 
Wassira akiwa rais unakuwa mwisho wa watoto kulia lia bila sababu za msingi (sababu kapuni)
 
ukisoma mpango wa TASAF #3 unatoa fedha za matibabu,chakula kwa wasiojiweza na karo kwa ajili ya Elimu,na mpango unaanzia kaya 3078 zilizopo Bagamoyo na zitafuata kaya zote kabla ya 2015...hapo walenga ni wajumbe wa mkutano mkuu wa C C M na sijui Lowasa hapo atachomokea wapi hahahahaha chezeya wasira weye,zee la Mahusiano leny mvuto kwa wanachama
 
Itabidi asisafiri ili watalii waje kwa wingi kumwangalia kabla hawajaenda kuangalia ndugu zake kule kwenye pori la kigoma
 
Watawala wa TZ hawana mipango shirikishi ya kuleta maendeleo ya kweli, lakini kwenye mambo ya kutaka uongozi ni mabingwa wa kimikakati.
 
Mbona hata sasa yuko Ikulu kiofisi,,,, au hukumsikia wakati anachimba mkwara kuwa wapinzani kamwe hawatakaribishwa Ikulu.

Huyu Mzee wa Gombe hata ubunge wa Bunda hawezi kupambana na Esther Bulaya sasa huo urais atapataje? Lakini kwa CCM wameona mchovu kama JK kawa rais ndio maana akina Nape, Mwigulu Nchemba, January Makamba, Lusinde, William Malecela na wengi tu wameishatangaza nia ya kujitosa urais. But 2015 hata wakigombea wote kwa pamoja wataishia kuisoma namba tu, watanzania hatutarudia makosa ya kukumbatia umaskini kwa kuchagua CCM
 
Com'on men,

Of all the people, you mean Steven Wassira Tyson gonna be a presida of the United Republic of Tanzania???
Kweli dunia na hata Sokwe wa Gombe watatucheka Watanzania ile mbaya!

Kwamba Wassira awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania????Bila shaka hii itakuwa ni ndoto tamu sana kwa Bwana Wassira!

Hivi kwa Wana-CCM wanafikiri kwa akili zao finyu Wassira anaweza kutawala Tanzania kwa sifa zipi hasa alizonazo?
Huyu mwendawazimuambaye juzi amepingwa na Rais na Mwenyekiti wake kuhusu madai yake kuwa MILANGO YA IKULU IMEFUNGENGWA KWA WAPINZANI KWA HIYO WASITEGEMEE KUITWA KUJA KUNYWA JUICE NA MAJI!!!!

Hivi hawa ma-CCM wanategemea nini kwa Rais mwenye matamushi ya kipuuzi kama haya???Wassira hafai,hafai,hafai,hafai na hana sifa za kuongoza nchi kama Rais. Kama kweli Wassira ana ndoto za kuwa Rais wa nji hii basi tutashuhudia Mahoka,Vihoja na Vituko vya kucheka na kusikitisha!!!

Najua kwa nchi hii chini ya uongozi wa CCM lolote au chochote kinaweza kutokea.

Tusubiri tuone hatima yake.
 
ukisoma mpango wa TASAF #3 unatoa fedha za matibabu,chakula kwa wasiojiweza na karo kwa ajili ya Elimu,na mpango unaanzia kaya 3078 zilizopo Bagamoyo na zitafuata kaya zote kabla ya 2015...hapo walenga ni wajumbe wa mkutano mkuu wa C C M na sijui Lowasa hapo atachomokea wapi hahahahaha chezeya wasira weye,zee la Mahusiano leny mvuto kwa wanachama

Kama ilivyo mipango karibu yote ya serikali awamu ya 4, either inaanzia au inajumuisha Bagamoyo. Si kwamba Bagamoyo ndio wilaya pekee inayohitaji maendeleo kwa haraka lkn yanafanyika kumpendeza mwenye kaya ili akuunge mkono(km kwa Wassira na TASAF) au kulimia TUMBO.

Wagombea u-Rais 2015 lazima waje na definition na demarcations za ufisadi maana to this regime, ufisadi ni kuunga mkono upinzani, kuishutumu serikali, kutomkubali jk, kuandamana, kugoma, ufujaji wa fedha wa maafisa wa idara za serikali za mitaa na manesi nk.
 
Wassira is a compromise candidate in CCM no matter what you kids talk about, The man is capable,energetic,and intelligent to lead the country.
Wassira gooo you deserve it!
 
Com'on men,

Of all the people, you mean Steven Wassira Tyson gonna be a presida of the United Republic of Tanzania???
Kweli dunia na hata Sokwe wa Gombe watatucheka Watanzania ile mbaya!

Kwamba Wassira awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania????Bila shaka hii itakuwa ni ndoto tamu sana kwa Bwana Wassira!

Hivi kwa Wana-CCM wanafikiri kwa akili zao finyu Wassira anaweza kutawala Tanzania kwa sifa zipi hasa alizonazo?
Huyu mwendawazimuambaye juzi amepingwa na Rais na Mwenyekiti wake kuhusu madai yake kuwa MILANGO YA IKULU IMEFUNGENGWA KWA WAPINZANI KWA HIYO WASITEGEMEE KUITWA KUJA KUNYWA JUICE NA MAJI!!!!

Hivi hawa ma-CCM wanategemea nini kwa Rais mwenye matamushi ya kipuuzi kama haya???Wassira hafai,hafai,hafai,hafai na hana sifa za kuongoza nchi kama Rais. Kama kweli Wassira ana ndoto za kuwa Rais wa nji hii basi tutashuhudia Mahoka,Vihoja na Vituko vya kucheka na kusikitisha!!!

Najua kwa nchi hii chini ya uongozi wa CCM lolote au chochote kinaweza kutokea.

Tusubiri tuone hatima yake.

Hii dharau ulionayo nadhani unamzungumzia Slaa ambae sidhani kama watanzania watampa kura tena, maana ni mnafiki,mzandiki na mtetea tumbo badala ya wanyonge.
Wassira atakuwa kama Mungu akimbariki wewe mwenye hila huwezi zuia mafuriko
 
Itabidi asisafiri ili watalii waje kwa wingi kumwangalia kabla hawajaenda kuangalia ndugu zake kule kwenye pori la kigoma

Nyota ya Wassira inazidi kung'aa kila kukicha, yeye hajasema lakini wapiga debe naona mnazidi kuongezeka.
 
Wassira anazo sifa nyingi za kumfanya kuwa Rais na si TASAF peke yake

1. Uadilifu
2. Uzalendo
3. Uchapakazi
4. Ujasiri
5. Ukweli na uwazi
6. Uzoefu.
 
Back
Top Bottom