TARURA wilaya ya Ubungo mmesinzia!

TARURA wilaya ya Ubungo mmesinzia!

unakosea sana mkuu.
Nchi hii inaongoza na Amiri Jeshi Mkuu, Samia sio Kikwete.
Hayati JPM alikuwa na msemo;
"maendeleo hayana chama"
barabara hizi tunapita sote, mkeka uliotandikwa kuanzia kimara mwisho hadi kibaha sote tunapita huku tukijidai....yaani gari zinateleza tu (asante hayati JPM).
sasa ni zamu Ya Mama yetu mpendwa.
Mtamkumbuka JPM 😅 wacha hela ziendelee kuishilia wilayani tu kwa mkurugenzi
 
Huku goba ndani barabara bado sana, acha kuwapa sifa wasizostahili, ujenzi wa barabara za mitaani ulishashika kasi kipindi cha magu......tumerudi kulekule shimoni.
Kipindi cha magu barabara za Mtaa wa Tegeta A, Kata ya Goba zilisahaulika.

Sasa hivi ukarabati unendelea. Ninazungumza nikionacho. Barabara itokayo Njia-Panda Tegeta A hadi mpakani mwa Madale na Kulangwa, na barabara ya kutokea Njia Nne hadi Kwa Abedui zinaendelea kuchongwa na daraja la Kwa Katunzi limekamilika. Mimi siyo muimba pambio. Nasema ukweli
 
Kata ya Sinza barabara ya Igesa inayopita Law School, na ile inayotokea kwenye jengo refu Sinza Makaburini zimechongwa. Kwa hiyo TARURA Sinza wamefika.
Hiyo ambapo hawakumaliza kazi? Sasa hivi madimbwi yapo katika maeneo yale ambayo maji yanayotoka chuo cha sheria yanavuka hiyo barabara. Zipo drift zaidi ya 10 na zote hazikuchongwa. Mbomba linalokatiza batabara limekatwa na linavuja na limeshatengeneza shimo.
Sasa wanapita au wanachonga na kurekebisha?
TULIZENI AKILI. KAMA MNATAKA PICHA SEMENI

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
 
Wananchi wa wilaya ya ubungo kata ya kiluvya gogoni/polisi/hondogo wanataka kuona barabara zinatengenezwa sio maneno.
Kuna mchepuko wa barabara ya TANROAD unatokea Kiluvya Gogoni/POLISI unapitia Kwa Kawawa unatokea Kiluvya Kwa Komba, huo ni mchepuko muhimu sana na upo chini ya TANROAD.
ZIlizobaki TARURA wanaweza kuendelea nazo na wananchi wa eneo hilo pia wakaondokana na kero ZA barabara mbovu.
Inawezekana.
 
kwa hiyo huyo mkandarasi mmoja ndio kachukua tenda ya wilaya yote ya ubungo?!!
naamini sivyo kutokana na ukubwa wa wilaya ya Ubungo kamwe hawezi kupewa kandarasi mmoja,
lazima kuna kandarasi zaidi ya mmoja au kuna subcontract.
lazima kazi ionekane inafanyika kila kona za wilaya, sio wajibanze huko ndanindani Goba halafu wanajifanya eti wapo kazini kumbe wametafuta kichaka cha kupigia.
wanasubiria mvua zianze kunyesha halafu iwe sababu.
Viongozi wetu wabunge, Madiwani pamoja na wenyeviti wa mitaa wanapaswa wawe imara na Makini sana.
Kuna hatari au kuna uwezekano kabisa kuwa ujenzi wa barabara hizi ZA mitaani zikajengwa maeneo ambayo kuna viongozi wenye ushawishi na maeneo yasiyo na mtu au watu muhimu basi yakaachwa solemba.
Nakubaliana na hoja yako mkuu.
 
kulikoni TARURA wilaya ya Ubungo kuhusu ujenzi ya barabara za pembezoni?
naongelea barabara za Kiluvya Polisi (kituo kikuu) hadi Kiluvya Hondogo, wananchi wa maeneo hayo wanalalamika kuwa waliahidiwa kuwa ujenzi utaanza mwezi huu wa Novemba lakin kimyaaa hadi leo.
Mhe. Rais Mama Samia kamwaga zaidi ya 14Billioni sasa tatizo ni nini?
Je Uongozi wa TARURA Wilaya ya Ubungo wana hujumu jitihada za Rais?!
 
Swali kwa TARURA wilaya ya Ubungo.
Je?hii barabara ya mchepuko kutoka kiluvya gogoni(kituo kikuu cha Polisi) na kitokezea Kiluvya kwa Komba inajengwa na TARURA au TANROAD?

kama ni TANROAD basi TARURA wanapaswa na wao waipokee ujenzi kutoka TANROAD wanapo achia hadi shule za Msingi Hondogo ambapo itarahisisha usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo haswa watoto wetu wanao soma ktk shule hizo.
 
Back
Top Bottom