TARURA wilaya ya Ubungo mmesinzia!

luirhu

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
800
412
Kulikoni TARURA WILAYA mpya ya ubungo mbona mmesinzia?!

Tangu billion 14 zilipo tolewa kwa wakandarasi Kwa ajili ya kuanza kazi ya ujenzi wa barabara ZA mitaa, wananchi wanaona kimya kimetanda! Kulikoni!

Maeneo ya pembezoni mwa mji kama vile maeneo ya Kiluvya POLISI GOGONI hadi HONDOGO barabara ni mbovu sana na wala hakuna dalili ya mkandarasi wala nini.

Maeneo ya pembezoni ni muhimu sana yakazingatiwa zaidi. Chondechonde msimuangushe Mhe. Rais wetu Samia ambaye amedhamiria.

Wizara ya TAMISEMI amkeni changamkeni, fuatilieni matumizi ya pesa hizi za watanzania Kwa karibu.
 
Kulikoni TARURA WILAYA mpya ya ubungo mbona mmesinzia?!
Tangu billion 14 zilipo tolewa kwa wakandarasi Kwa ajili ya kuanza kazi ya ujenzi wa barabara ZA mitaa, wananchi wanaona kimya kimetanda! Kulikoni!
Maeneo ya pembezoni mwa mji kama vile maeneo ya kiluvya POLISI GOGONI hadi HONDOGO barabara ni mbovu sana na wala hakuna dalili ya mkandarasi wala nini.
Maeneo ya pembezoni ni muhimu sana yakazingatiwa zaidi.
Chondechonde msimuangushe Mhe. Rais wetu Samia ambaye amedhamiria.
Wizara ya Tamiaemi amkeni changamkeni, fuatilieni matumizi ya pesa hizi ZA watanzania Kwa karibu
Kuna tatizo kwa watendaji wetu.
Yaani shida yetu mpka tusukumwe na kufuatiliwa nyuma!!

fedha zilishatoka kitambo lkn bado wanasuasua!! Je? lengo ni kutaka kuhujumu jitihada na dhamira ya mhe. Rais au nini?!

Naunga mkono 100% maeneo hayo barabara ni mbovu sana, nilifika maeneo ya kiluvya Polisi mpaka hondogo yaani hayafai!
Mbunge yupo na Diwani yupo.
 
Barabara ya kimara - kibaha imekwama tayari sidhani Kama huko mitaani zitakamilika...
nchi ya kikwete hii usitegemee maajabu yeyote kutoka kwao
unakosea sana mkuu.
Nchi hii inaongoza na Amiri Jeshi Mkuu, Samia sio Kikwete.
Hayati JPM alikuwa na msemo;
"maendeleo hayana chama"
barabara hizi tunapita sote, mkeka uliotandikwa kuanzia kimara mwisho hadi kibaha sote tunapita huku tukijidai....yaani gari zinateleza tu (asante hayati JPM).
sasa ni zamu Ya Mama yetu mpendwa.
 
TARURA Ubungo wanajitahidi sana. Kata ya Goba wanakarabati barabara ambazo hazikuwa zinapitika kabisa.

Huko Hondogo, Kiluvya njia zina afadhali kidogo. Bila shaka watakuja huko soon
 
hili ndio tatizo la wakandarasi wa Kibongo/wazawa, kwanza wanaizungusha pesa kwenye biashara nyingine, halafu wanavuta muda mvua zianze kunyesha kisha watoe sababu!
lkn sio kwa pesa hii ya walipa kodi! watazitapika kupitia puani.
 
TARURA Ubungo wanajitahidi sana. Kata ya Goba wanakarabati barabara ambazo hazikuwa zinapitika kabisa.

Huko Hondogo, Kiluvya njia zina afadhali kidogo. Bila shaka watakuja huko soon
kama hujui bora ukae kimya, mimi nimepita njia hiyo kuanzia Kutuo kikubwa cha Polisi Gogoni hadi zilipo shule za Sekondari Hondogo kama Km3.5 barabara mbovu sana, hakuna daladala inayo pita huko, wanafunzi wanakanyaga kwa miguu hadi huruma.
TARURA lazima waliangalie eneo hili ni muhimu sana.
inabidi sasa tuseme, kama Mbunge wala diwani haoni sawa. 2025 sio mbali sana.
 
Namtamani Sabaya asamehewe makosa yake halafu ateuliwe japo hata mtendaji mkuu wa TARURA apambane na wahandisi feki.
Bara bara nyingi za TARURA huwa ni za kiwango cha chini sana yaani mvua msimu mmoja barabara inapotea yote kwa maji ya mvua.
Mifano ipo mingi sana.
Mfani barabara ya mji mpya morogoro mjini ni mashimo tupu halafu mamlaka wanajenga lami juu ya lami.
TARURA Sio ubungo tu ni sehemu nyingi.
Ila SABAYA anaweza isaidia serikali hii kwa wakandarasi kama hao waliolipwa tayari.
 
Labda wanafanya kwingine ila kata ya Sinza sijaona chochote. Hata tenda hawatangazi, wakiopewa kazi hemna. Jamani hizi taasisi utadhani hawakupewa fungu?

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
 
Kwanini Sabaya na sio wewe ?
 
Siwezi kukaa kimya wakati unapotosha. TARURA Ubungo wanajitahidi sana. Ubungo ina Kata 14 na mitaa 89. Ukiona hawajafika Kata ya Kibamba, basi ujue wapo Goba. Barabara yako kuwa na changamoto haina maana kwamba TARURA Ubungo hawafanyi kazi
 
Labda wanafanya kwingine ila kata ya Sinza sijaona chochote. Hata tenda hawatangazi, wakiopewa kazi hemna. Jamani hizi taasisi utadhani hawakupewa fungu?

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
Kata ya Sinza barabara ya Igesa inayopita Law School, na ile inayotokea kwenye jengo refu Sinza Makaburini zimechongwa. Kwa hiyo TARURA Sinza wamefika.
 
Namtamani Sabaya asamehewe makosa yake halafu ateuliwe japo hata mtendaji mkuu wa TARURA apambane na wahandisi feki.
Bara bara nyingi za TARURA huwa ni za kiwango cha chini sana yaani mvua msimu mmoja barabara inapotea yote kwa maji ya mvua.
Mifano ipo mingi sana.
Mfani barabara ya mji mpya morogoro mjini ni mashimo tupu halafu mamlaka wanajenga lami juu ya lami.
TARURA Sio ubungo tu ni sehemu nyingi.
Ila SABAYA anaweza isaidia serikali hii kwa wakandarasi kama hao waliolipwa tayari.
Umenena Mkuu.
lkn TARURA kama sijakosea zipo chini ya Halmashauri.
na Halmashauri zetu zilizo nyingi ni wapigaji wa fedha za umma, sasa sijui ni nani wa kuwasimamia, LKN Waziri wa TAMISEMA wanayo dhamana ya kufuatilia.
Pamoja na mambo yote lkn JAFFO alikuwa anamudu sana ktk ufuatiliaji.
 
Siwezi kukaa kimya wakati unapotosha. TARURA Ubungo wanajitahidi sana. Ubungo ina Kata 14 na mitaa 89. Ukiona hawajafika Kata ya Kibamba, basi ujue wapo Goba. Barabara yako kuwa na changamoto haina maana kwamba TARURA Ubungo hawafanyi kazi
kwa hiyo huyo mkandarasi mmoja ndio kachukua tenda ya wilaya yote ya ubungo?!!
naamini sivyo kutokana na ukubwa wa wilaya ya Ubungo kamwe hawezi kupewa kandarasi mmoja,
lazima kuna kandarasi zaidi ya mmoja au kuna subcontract.
lazima kazi ionekane inafanyika kila kona za wilaya, sio wajibanze huko ndanindani Goba halafu wanajifanya eti wapo kazini kumbe wametafuta kichaka cha kupigia.
wanasubiria mvua zianze kunyesha halafu iwe sababu.
 
TARURA Ubungo wanajitahidi sana. Kata ya Goba wanakarabati barabara ambazo hazikuwa zinapitika kabisa.

Huko Hondogo, Kiluvya njia zina afadhali kidogo. Bila shaka watakuja huko soon
Huku goba ndani barabara bado sana, acha kuwapa sifa wasizostahili, ujenzi wa barabara za mitaani ulishashika kasi kipindi cha magu......tumerudi kulekule shimoni.
 
kwa hiyo huyo mkandarasi mmoja ndio kachukua tenda ya wilaya yote ya ubungo?!!
naamini sivyo kutokana na ukubwa wa wilaya ya Ubungo kamwe hawezi kupewa kandarasi mmoja,
lazima kuna kandarasi zaidi ya mmoja au kuna subcontract.
lazima kazi ionekane inafanyika kila kona za wilaya, sio wajibanze huko ndanindani Goba halafu wanajifanya eti wapo kazini kumbe wametafuta kichaka cha kupigia.
wanasubiria mvua zianze kunyesha halafu iwe sababu.
Mkuu achana na fix za huyo jamaa, aje atuonyeshe barabara zinazojengwa goba ni zipi kabla ya kuleta matango pori hapa...
 
Back
Top Bottom