uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 2,085
- 2,996
Habari zenu wanajamvi,
kama habari inavyosomeka
nitangulize samahani huwenda nimekosea
herufi za taasisi husika(Tarura) nilitaka kumaanisha
ile idara inayoshughulika na barabara inayofanya kazi
kama TANROAD.Naisikia taasisi hii ila sielewi majukumu yake.
Mimi ni mkazi wa kisukuru migombani njia ya kwenda
makokoka,tupo kwenye jimbo la uchaguzi la segerea
Mbunge wetu ni wa ccm anaitwa Bona .
mwanzoni barabara zetu mtaani zikiwa na hali
mbaya tulikuwa tukimwendea diwani wetu
naye anafanya linalowezekana ili kutusaidia.
Baadaye nikasikia kwamba majukumu haya ya barabara
za mitaa yetu yanashughulikiwa na taasisi inayoitwa tarura.
sasa tangia jukumu hili lihamishiwe
tarura,hata gereda lililokuwa likipita kufukia makolongo
hatulioni tena.Mbaya Zaidi ni hili daraja linalounganisha
barabara ya kutokea migombani kwenda makoka
kupitia kwa mama Mushka,mvua zilizoisha liliponea chupuchupu
kukatika na ni juhudi zetu wananchi ziliokoa hili daraja
kwa kuweka matairi na viroba. Kinachonisikitisha zaidi
ni kuona karibia mwaka unaisha na tunakaribia
kuingia kipindi kingine cha mvua za masika ambapo
lazima daraja hili halitahimili mikiki ya mkondo mkubwa wa maji
yanayopita kwa kutegemea matairi na viroba vya cement.
Nadhani gharama iliyojenga hili daraja ni kubwa
kuliko ya kurepair,tukisubiri likatike kabisa
tutakuwa tunaharibu fedha nyingi bila sababu
nadhani hawa tarura wafanye mpango
wa kujazia kifusi eneo lililokatika kwani makaravati bado yapo imara.
Watu wa tarura kama mpo humu naomba mpitie eneo hili
kujionea hali halisi na kutoa ushauri au kutujulisha nini mpango wenu
wa sasa au baadaye juu ya hili daraja,Nimeambatanisha picha walau za upande mmoja.
asanteni.