Tarifa kwa Umma: Imba Ukombozi

Tarifa kwa Umma: Imba Ukombozi

Chademakwanza

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
6,346
Reaction score
1,872
Taarifa kwa Umma.....

Idara ya sanaa Chadema Taifa kwa sasa iko ziarani nyanda za juu kusini mikoa ya Njombe Mbeya Songea, ziara hii imepewa jina la

"IMBA UKOMBOZI".

Ieleweke idara ya sanaa ya Chadema inawasanii wengi karibu kila mkoa.

Ziara hii ya idara ya sanaa inamalengo ya kuhamasisha vijana kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la wapiga kura punde zoezi litakapoanza, lengo la pili kuwahamasisha kuimba nyimbo za ukombozi.

Imetolewa na idara ya sanaa Chadema Taifa
 
Asante taarifa hiyo imepokelewa.
 
Sasa mkuu hamkuendanae Njombe na Makambako ? mnaona mumeacha na njaa huku wenzenu wamekuja nakumchukua na kumpa cheo
 
Asante Sana Makamanda tuko pamoja, mkitoka huko mje mtuimbishe kanda ya kati ikiwezekana... chilihamonga muno wawaha!
 
Asante sana. Idara makini kwa kazi makini chini ya watu makini.

Sisi watanzania tutaisapoti chama hiki kwa sababu haijawahi kuchoka au 'kususa' kutoa elimu ya uraia iwe kwa njia ya mikutano ya hadhara ama njia ya sanaa kama hivi.

Big up sana CHADEMA na mmalizapo nyanda za juu kusini karibuni na huku kwetu pwani
 
Siasa za Tanzania zimegubikwa na gilba ya maslahi kiasi kwamba mwanachama wa CHADEMA anaweza kuhamia CCM ikiwa malengo yake fulani ya yatatimia. Anaweza kuhama CUF kuhamia ACT ikiwa kuna fursa ya kupata madaraka na sehemu aliko wamesheheni watu wengi hivyo kupata cheo mtiti wake sio kitoto.

Ndio maana tukahitaji MGOMBEA BINAFSI ihuhishwe kusudi kuepusha unafiki wakutumikia chama cha kibepari miaka 10 ukilipwa mishahara na posho, na unaamia chama cha kijamaa nakudai sasa upo chama kinachoendana na mtazamo wako.

Hizi RUZUKU sharti masharti yaongezwe au zipungue, nasikia hata chama cha Dovutwa kila mwezi anapokea kalaki tisa kutokana na KODI ZETU WANANCHI
 
Wasanii wanapatikana vipi mkuu, je nikitaka nifanye hiyo kazi naipataje
 
Ahsante nadhani hapo Pr.J na kundambandamba atakuwepo,mbele mbele hakuna kurudi nyuma,wamaoshuka njiani watatukuta nyumbani
 
Siasa za Tanzania zimegubikwa na gilba ya maslahi kiasi kwamba mwanachama wa CHADEMA anaweza kuhamia CCM ikiwa malengo yake fulani ya yatatimia. Anaweza kuhama CUF kuhamia ACT ikiwa kuna fursa ya kupata madaraka na sehemu aliko wamesheheni watu wengi hivyo kupata cheo mtiti wake sio kitoto.

Ndio maana tukahitaji MGOMBEA BINAFSI ihuhishwe kusudi kuepusha unafiki wakutumikia chama cha kibepari miaka 10 ukilipwa mishahara na posho, na unaamia chama cha kijamaa nakudai sasa upo chama kinachoendana na mtazamo wako.

Hizi RUZUKU sharti masharti yaongezwe au zipungue, nasikia hata chama cha Dovutwa kila mwezi anapokea kalaki tisa kutokana na KODI ZETU WANANCHI

Mkuu sina uhakika unasimamia hoja ipi lakini kilicho muhimu ni umma wa watanzania kupata elimu ya uraia.

Ideally elimu ya uraia kwanza afu sera za chama zinafuata. TATIZO ktk nchi ambayo serikali haitaki wananchi kupata elimu ya uraia inabaki kwamba vikundi kama hivi vyenye kuhamasisha, kuburudisha na kuelimisha inapewa umuhimu na kipaumbele
 
Safi sana makamanda wa idara ya Sanaa.

Huu ni wakati wa kutumia silaha zote kuleta ukombozi
 
Back
Top Bottom