Tarehe 31 Machi, 2022 TTCL wanapandisha bei ya vifurushi

Status
Not open for further replies.
Noma sana wakuu, tarehe tajwa hapo juu 31.03.2022, shirika la serikali la mawasiliano litatupiga na kitu kizito sana kichwani, wanapandisha vifurushi.

Bufee inaweza kuondolewa maana inawatia hasara tu. Toboa night HAIRUDISHWI ng'o

Si mnakumbuka tuliambiwa tuhamie Burundi tukaanza kuleta mapozi?

Sasa nyumbani kunafuka moshi.

Tujiandae kisaikolojia.
acha uongo
kesho tar 31 hakuna kitakachopandishwa

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Watanzania tunalalamika saaaaaana. Ila kiukweli ni moja ya nchi chache DUNIANI ambazo unapata bando la uhakika chini ya USD 1. Ni nchi chache sana zina kiwango hiko. Tuwe na shukrani.
Jua kwanza gharama ya kitu chochote hutegemea uchumi wa nchi, chip kavu za bongo usidhani ukienda marekani 🇺🇸 utanunua kwa buku jero.
 
Well said. Hoja ambayo wengi hawaielewi. Hata ukivuka hapo Kenya bei ya chips au hata sahani ya ugali kwa maharage iko juu kuliko huku kwetu.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom