Nimerudi Halotel na Vodacom baada ya TTCL kupandisha bei ya vifurushi

Buza Kwa Mpalange

Senior Member
Apr 15, 2020
139
150
Moja kwa moja kwenye mada,

Hii kampuni ya kuitwa TTCL Customer Care imekuwa hawajali kabisa wananchi wa kipato cha chini kabisa.

Mwanzo walikuwa na vifurushi rafiki sana, Watanzania tukaanza kuwaamini tukaona ndio wanatutoa kwenye mikono ya utawala wa kinyonyaji wa mabeberu akina VodaCom, Airtel, Halotel, Tigo, Smart na Smile.

Tukaanza kuambiwa TURUDI NYUMBANI KUMENOGA, tukaamua kurudi, tukarudi kweli. Tarehe kama ya 27 Julai 2020 unajua kilichotokea? Watu bado tupo kwenye majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu Rais Mstaafu Mkapa na TTCL si wakaamua kutuongezea kilio zaidi

Ile tumetoka kuzika tukaona tujifariji hata kuingia mtandaoni kupata habari, tunajaribu kupiga *148*30#
TOBOA NIGHT hakuna
BANDUKA BANDUA holaa
Tukapiga *150*71# kucheki BANDO TAMTAM ndio hakuna kitu
Nikasema ngoja nikachungulie UNI PACK kule ndio kabisaaa.

Kuanzia leo mimi sitatumia tena mtandao wa TTCL, kama mkataa kwao ni mtumwa bora niende ugenini niwe mtumwa ila nipate huduma nzuri.

Hawana SMS za kuchombeza wateja, yaani hata kutuma sms ya kumkumbushia kama kuna huduma mpya.

Costomer Care wana lugha mbovu, majibu ya nyodo na dharau juu mpaka unapata hasira.

Wanaosajili laini mitaaani ndio hatuwaoni kabisa.

Muda wa kurudi HALOTEL na VodaCom ndiyo huu.

Halotel, VodaCom, Tigo na Zantel nisameheni sana shetani alinishawishi nirudi nyumbani kumenoga kumbe alinidanganya.
Ulaaniwe sana shetani.
 

TOHATO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,047
2,000
Sifagilii tccl ila naona nyuzi zako unakitu moyoni na hili shirika kana kwamba limekutimua kazi vile Mana hi ni nyuzi ya piliau zaidi inayohusu kulia lia na tccl
 

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,600
2,000
Sifagilii tccl ila naona nyuzi zako unakitu moyoni na hili shirika kana kwamba limekutimua kazi vile Mana hi ni nyuzi ya piliau zaidi inayohusu kulia lia na tccl
Jiunge na mtandao bora wa TTCL ufurahie huduma zenye bei nafuu na kasi ya intaneti ya 4.5G.

#RudiNyumbaniKumenoga
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom