Taratibu za kuuziana gari mtaani kupitia KUPATANA/ZOOM Tz ili kuepuka kutapeliwa

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Salam wakuu.

Naomba kuuliza taratibu au njia sahihi ya kuuziana gari mtaani kupitia hii mitandao ya kijamii na blogs kama KUPATANA, ZOOM Tanzania jobs etc ili kuepuka kutapeliwa.

Unaanza kutoa pesa kwanza au gari kwanza?Pesa unalipa kwa mfumo gani?Benki au cash?Maana pia wengi wanakuwq na copy ya kadi ya gari na si original.Na mnakutania wapi, mbele ya ushahidi gani?

Nimekopa kahela fulani benki, nataka kuchukua ka PASSO niweke shida chini kiaina.

Naombeni ushauri wakuu ili nipate A,B,C za kununua gari mtaani kwa njia sahihi.

Asante sana.
 
mkuu yule msenegal aliyekutapeli vipi ushafanikiwa kumroga!?
 
Unakagua gari kwanza kupitia mechanic wako yaani nenda nae, na kuliendesha hata dk 10 au zaidi. Usitoe pesa hadi uone vyote na kadi za gari na kwa sasa kuwa haina madeni TRA n.k.
Kuandikishana muhimu kama ikitokea hivi au vile iweje, lipa kupitia benki uwe na kumbukumbu. Uliza maswali yote, usione aibu wewe ni mteja.

Sijawahi nunua gari kwa njia hii, ila nimedokeza tu machache.
 
Fata njia hizi!
1.ukiliona gari linalkufaa wasiliana n'a mmikili,na uende ukalikague na fundi wako
2.Kabla ya kununua gari Nenda TRA kahakiki Kadi ya gari kujua umiliki au kama gari linadaiwa au Labda lishaombewa mkopo..utajua huko
3.kwenye mauziano kuwepo na mkataba na mashahidi wawepo
4.mauziano ni vzuri kulipana kupittia bank kama hela ni ndefu,
5.kama hauna ukaribu na mtu au Huna imani na fulani ambaye unataka fanya naye biashara ya gari---usifanye biashara ya gari kuanzia Midas ya saa kumi na moja jioni na kuendeleaaa

Ukifata taratibu hzo hutoingia ktk maumivu ya kupigwa....

Ova
Salam wakuu.

Naomba kuuliza taratibu au njia sahihi ya kuuziana gari mtaani kupitia hii mitandao ya kijamii na blogs kama KUPATANA, ZOOM Tanzania jobs etc ili kuepuka kutapeliwa.

Unaanza kutoa pesa kwanza au gari kwanza?Pesa unalipa kwa mfumo gani?Benki au cash?Maana pia wengi wanakuwq na copy ya kadi ya gari na si original.Na mnakutania wapi, mbele ya ushahidi gani?

Nimekopa kahela fulani benki, nataka kuchukua ka PASSO niweke shida chini kiaina.

Naombeni ushauri wakuu ili nipate A,B,C za kununua gari mtaani kwa njia sahihi.

Asante sana.
 
We Baki kwenye siasa ujasiriamali tuachie wenyewe

Back
Top Bottom