Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,015
- 2,191
Uongozi na wanachama wa Umoja wa Waendeshaji wa Vituo vya Mafuta ya Petroli nchini (Tanzania Petrol Stations Operators - TAPSOA), umepokea kwa furaha kubwa uamuzi wa busara na wa kishujaa uliofikiwa na viongozi wetu wakuu wa Tanzania na Uganda, Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa kuamua kujenga bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Uganda.
Tunaamini kuwa uamuzi huo umefikiwa katika wakati muafaka, hasa kipindi hiki wakati mataifa haya mawili yakilenga kukuza uchumi wake, huku Tanzania ikipania kuwa nchi yenye kipato cha kati na uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.
Dk. Magufuli na Museveni walifanya mazungumzo walipokutana kwenye Ikulu Ndogo jijiji Arusha katikati ya wiki, ambapo wamekubaliana kufanyika kwa ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta kutoka Bandari ya Tanga nchini Tanzania hadi Uganda, litakalopita kaskazini mwa Tanzania, hivyo kuinganisha Uganda na dunia.
Museveni alimtembelea Rais Magufuli Jumanne wiki hii mara tu baada ya kuwasili nchini, siku chache baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu nchini mwake, kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Hoteli ya Ngurudoto nje ya Jiji la Arusha.
Taarifa iliyotolewa baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo ya faragha ilisema kwamba viongozi hao wakuu wan chi mbili wanachama wa EAC wamekubaliamna kutekeleza mradi huo wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili na nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa ujumla.
Bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1,120 na kwamba mradi huo utazalisha ajira za watu zaidi ya 15,000 kutoka Uganda na Tanzania, kitendo ambacho sisi TAPSOA kinatupa imani kwamba kitakuwa chachu ya maendeo ya mtu mmoja mmoja na jamii nzima.
Mbali na ujenzi wa bomba hilo muhimu kwa maendeleo ya Tanzania na Uganda, viongozi hao pia walizungumzia kuongeza biashara ndani ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kujenga viwanda na kuzalisha ajira zaidi kupitia sekta mbalimbali za uzalishaji mali.
TAPSOA tunakubaliana kwa moyo mmoja na ujenzi wa mradi huo utakaowapa fursa wafanyabishara wa mafuta kutoka Tanzania na Uganda kupanua wigo wao na kulifikia soko kubwa la EAC lenye takriban watu milioni 150, hivyo kupata manufaa makubwa kama wafanyabiashara, huku pia wakizinufaisha serikali zao kwa njia ya kodi.
Kwa hakika hatua hii iliyochukuliwa na marais hawa wawili haiwezi pupita bila kuungwa mkono kwani imeonyesha ni namna gani viongozi hawa wamepania kuwatumika wananchi wao bila woga na sisi TAPSOA tunawaahidi kuwaunga mkono katika kila jema walilopanga kulifanya kwa manufaa ya mataifa yetu mawili na EAC nzima.