TAPP (Tanzania AIDS Prevention Program) kulikoni?

chhatbhai

Member
Apr 12, 2016
8
1
Majipu ni mengi sana, na mengine ndiyo yanasababisha wahisani kutunyima pesa, mfano ni hili shirika la TAPP (TANZANIA AIDS PREVENTION PROGRAM), linapokea fedha za miradi na kuzitumia isivyo.Wanapata miradi, wanapatia kazi asasi zingine, asasi zinafanya kazi, ikifika katikati uongozi wa TAPP wanadai kluwa hawajapokea pesa toka kwa wafadhili, na hiyo inafanyika katikati ya mradi kabla ya mkataba kuisha.

TAPP inadaiwa na asasi nne pesa za miezi miatatu ya mwaka 2014 (Jan, February an March 2014), wakidaiwa wanazungusha kuwa hawajapesa hizo pesa. Kweli CDC yaweza ingia mkataba na shirika ikawa idai idadi ya wateja waliyofikiwa kwa miezi mitatu mfululizo bila kulipa pesa?

Kumbuka kila asasi ina wafanyakazi wanaotakiwa kulipwa kila mwisho wa mwezi.Pale kuna mtindo wa ajabu, mwaka wa 2013 zilikuja pesa za GBV, asasi zikaelezwa kuwa pesa zimekuja ila zinasubiriwa zingine zifike ndipo asasi ziweze kupewa kwa pamoja, baadae kiswahili kikabadilika, mara pesa zimetumika kununulia maji ya kunywa kwa watu wanaopata huduma ya METHADONE, wakati hela ililenga kwenda kwenye asasi ambao ndiyo watendaji wa mradi huo.

Uongozi wa TAPP wameendeleza udanganyifu hata wakadanganya asasi iitwayo OPEN SOCIETY FOUNDATION ya Marekani na hata wawakirishi wao kuwa ilitumia pesa zaidi ya dolla laki 3 kuendesha mradi wa HARM REDUCTION kwa kutumia asasi iitwayo YOVARIBE, kitu ambacho si kweli. Walinunua mabomba na sindano (yote yapo yamejaa vumbi ofisi ya YOVARIBE na mengine yapo kwenye ofisi ya mratibu wa mradi huo huko TAPP Muhimbili).

Maofisa toka Nairobi na Marekani walikuja kutaka kujua kama mradi huo umefanyika, majibu waliyopata toka YOVARIBE yanakatisha tamaa. Pesa haziwahi kutumwa YOVARIBE, ni khasibu wa TAPP na Mratibu wa TAPP na kushirikiana na afisa mmoja wa YOVARIBE ndiyo wanafahamu wapi pesa hizo zilikokwenda. Kawaida kama asasi inakuwa imepewa mradi, basi pesa za mradi huo huwa zinatumwa kwenye akaunti ya asasi husika, hicho hakikufanyika. KUNANI??

Haya ni majipu TAKUKURU iingie pia hapo, ione jinsi walafi wanavyoaibisha nchi yetu.

Nawasilisha.
 
hivi inawezekana kweli kutumbua majipu yaliyopo kwenye miradi inayofadhiliwa na wahisani??maana saiivi hela zinapigwa huko watu wamepiga hela ndefu na wananendelea..NACP,TACAIDS,TAPPand the like ni majipuuuu
 
Ni majipu, TAKUKURU yaweza fika hu
hivi inawezekana kweli kutumbua majipu yaliyopo kwenye miradi inayofadhiliwa na wahisani??maana saiivi hela zinapigwa huko watu wamepiga hela ndefu na wananendelea..NACP,TACAIDS,TAPPand the like ni majipuuuu

TAKUKURU haina mipaka lazima iingie huko TAPP, hukusikia kuhusu zile za PANAMA PAPERS kuwa watafuatilia kuona kama kuna watanzania waliyoficha michuzi huko?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom