TANZIA: Sheikh Muhammad Bakari

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,805
31,819
20160308_175155.jpg

Sheikh Muhammad Bakari

Kila aliposimama kuzungumza watu walinasa maneno yake katika vinasa sauti
kama darsa tosha kusikizwa siku za usoni

Sheikh Muhammad Bakari amefariki usiku wa tarehe 26 Mfungu nane 1437 (sawa na tarehe 7 March 2016) na hadi kufikia afajir taarifa zikawa zimeshafika Tanga. Ghafla mji mzima ukawa umejiinamia. Mbuyu mkubwa ulikokuwa katikati ya mji uliokuwa ukitoa kivuli ulikuwa umeanguka. Sheikh Muhammad Bakari alikuwa mwanafuzi wa mwanazuoni mkubwa wa Afrika ya Mashariki na Kati marehemu Sheikh Muhammad Ayub muasisi wa Shamsiyya na mwalimu wa masheikh wengi.

Haukupita muda watu wakawa wamekusanyika uwanja wa ndege wa Tanga kusubiri mwili wa Sheikh Muhammad Bakari uliowasili majira ya saa nane. Tanga ilikuwa imeondokewa na msomi wake mkubwa ambae kabla ya kifo chake Sheikh Muhammad Ayub alipatapo kusema kuwa mwanafunzi wake Muhammad Bakari ni mwanazuoni.

Katika kumueleza Sheikh Muhammad Bakari Sheikh Suleiman Amrani Kilemile akizungumza kwenye msiba Dar es Salaam kabla ya mwili haujapelekwa uwanja wa ndege alisema kuwa Sheikh Muhammad Bakari kwao wao walipokuwa wanasoma kwa Sheikh Muhammad Ayub alikuwa ‘’kaka’’ na ‘’mwalimu.’’ Alimsifia Sheikh Muhammad Bakari kwa kusema kuwa alikuwa mtu wa subira ya hali ya juu wakati wa kusoma kwani wakati ule hali ilikuwa ngumu. Aliongeza na kusema kuwa Sheikh Muhammad Bakari alikuwa msomi wa sifa na alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kusoma vitabu. Akaendelea na kusema kuwa Sheikh Muhammad Bakari alikuwa na tabia ya kuweka sahihi yake kwenye kurasa ya mwisho ya kila kitabu alichomaliza kusoma.

Baada ya kifo cha Sheikh Muhammad Ayub Sheikh Muhammad Bakari alifundisha Shamsiyya kwa muda akishika nafasi ya mwalimu wake. Sheikh Muhammad Bakari aliondoka Shamsiyya na kwenda Magomeni kwenye msikiti mdogo na hapo akaendelea kusomesha chini ya taasisi yake mpya aliyoiita Shams Maarif akisaidiwa na walimu wachache waliomfuata kutoka Shamsiyya mmojawao akiwa Mwalimu Miraj na Sheikh Said Makata.

20160308_182002%252520%2525282%252529.jpg

Maalim Miraji

Hiki kilikuwa kipindi kigumu sana kwake na kwa wanafunzi waliomfuata kwani alijaza wanafunzi wengi katika mahali finyu. Watu wengi hawakupenda kuona hali ile lakini hawakuwa na la kufanya. Sheikh Muhammad Ayub aliendelea kusomaesha na mara kwa mara alikuwa akisema kuwa ile hali iliyokuwa ikimkabili katika kusomesha ilikuwa ni qadar ya Allah.

20160308_175301.jpg

Sheikh Muhammad Bakari katika uhai wake akihadhiri na wasikilizaji wakinasa
nasaha zake katika vinasa sauti

IMG-20160308-WA0206.jpg

Sheikh Muhammad Bakari akiozesha

20160308_164110.jpg

Kushoto Sharif Khitami na Sheikh Muhammad Bakari Nyuma ni Sharif
Mundhari Khitami siku ya ufunguzi wa Msikiti na Madrasa ya Shams Maarif

IMG-20160309-WA0112.jpg

Sheikh Muhammad Bakari Iddi Simba na Bakari Mwapachu siku ya ufunguzi

Kushoto Salim Bajaber, Sharif Khitami na Sheikh Muhammad Bakari
wakielekea msikitini kwenda kufanya ufunguzi wa msikiti na madras 2 May 2004

IMG-20160308-WA0188.jpg

IMG-20160308-WA0202.jpg

Kulia: Sheikh Muhammad Bakari, Salim Kisauji, Sheikh Muhammad Hariri
Mudir wa Maawal Islamiyya katika Maulid ya Bandari ya Tanga

IMG-20160308-WA0216%252520%2525281%252529.jpg

Umma ukiomba dua siku ya ufunguzi wa Msikiti na Madrasa ya Shams Maarif

IMG-20160309-WA0123.jpg

Katikati Salim Bajaber Meneja Mkuu wa Pembe Flour Mills Tanga

IMG-20160309-WA0126.jpg

Sheikh Alhad Omar akisoma Qur'an tukufu siku ya ufunguzi

20160308_172715.jpg

Kulia: Salim Bajaber wa Mombasa na Salim Bajaber wa Nairobi wakurugenzi
wa Pembe Flour Mills waliojenga msikiti na madrasa

DSCN0414.JPG

DSCN0416.JPG

Sheikh Salim Mtambo akiwa Uwanja wa Ndege akiratibu usafiri wa wazishi na maiti
kwenda Tanga

DSCN0415.JPG

Sheikh Burhani Bakari mdogo wa Sheikh Muhammad Bakari Uwanja wa
Ndege Dar es Salaam

IMG-20160309-WA0200.jpg

Mazikoni Duga

Umati uliojotokeza kumzika Sheikh Muhammad Bakari haujapatapo kuonekana Tanga. Barabara ya Mombasa ilifurika magari watu na waliokuwa wakitembea kwa miguu wakija Tanga mjini mazikoni. Vijiji vyote vya pembezoni mwa Tanga vilitoa watu walioingia mjini kwa maelfu.

Duga ilikuwa haiingiliki.

Screenshot_2016-03-09-23-12-01.jpg

Shams Maarif ilikuwa imezingirwa kila upande na wale waliopata nafasi ya kuingia msikitini ni wale ambao walifika pale asubuhi na mapema. Mji wa Tanga ulijiinamia.

Maziko haya yatazungumzwa kwa miaka mingi sana ijayo In Shaallah.
Kwa hakika haya maziko yamemueleza Sheikh Muhammad Bakari alikuwa nani.​

IMG-20160310-WA0127.jpg

Khitma

Maziko haya yamethibitisha kuwa silsila yake kama alivyopata kuieleza mwenyewe siku moja kuwa kapokea ilm kutoka kwa mwalimu wake Sheikh Muhammad Ayub na inakwenda nyuma hadi kufikia kwa Mtume SAW na kumalizikia kwa JIbril AS ambae alipokea kutoka kwa Allah SW.

IMG-20160310-WA0140.jpg

Ningependa kumaliza kwa kusema lini kwa mara ya kwanza nilipata kulisikia jina la Sheikh Muhammad Bakari.

Ilikuwa siku moja Msikiti wa Mtoro katika miaka ya 1970. Sheikh Kassim Juma alikuwa anamueleza Sheikh Muhammad Ayub.

Alipomaliza akaeleza maajabu aliyoyaona kwa Sheikh Muhammad Bakari.

Wakati ule Sheikh Muhammad Bakari alikuwa bado kijana mdogo mwanafunzi. Sheikh Kassim alisema kubwa aliloliona kwake Sheikh Muhammad Bakari ni ahklaki njema.

Kisha Sheikh Kassim Juma akaeleza umahiri wa Sheikh Muhammad Bakari katika ilm.

Ilipita miaka mingi hadi mimi kuja kujuana na Sheikh Muhammad Bakari wakati huo sasa Sheikh Muhammad Bakari alikuwa tayari ni sheikh na Mudir wa Shamsiyya chuo alichoasisi mwalimu wake Sheikh Muhammad Ayub.

IMG-20160308-WA0231.jpg

Kushoto: Sheikh Muhammad Hariri Mudir wa Maawal Islamiyya, Sheikh Muhammad
Bakari Mudir wa Shams Maarif na Mwandishi Tanga

Ahsante sana mwandishi wa makala hii,nilisoma TAMTA miaka 70,na umetupa historia nzuri sana.Nilipomaliza kusoma kwa Al marhum Mwalim Awadhi,nikaenda kusoma na TAMTA,Mwalimu wangu ninayemkumbuka Sharif Hashim,sijajuwa mpaka leo kwa nini hajiiti Sheikh,kigogo huyu wa Elimu,aliyewahi kuwa Mwalimu wa shule ya Secondary.
 
Samahani Maalim! U Sheikh Ni mtu Tu anaamua kujiita?
 
Moto wa jehanum unamsubiri

Kwa mujibu wa Imani yako uko sahihi, ila kwa Imani yake ya dini aliefia haupo sahihi!. Ila pia kwa mujibu wa desturi za Kiafrika na kibinadamu hapakuwa na ulazima wa kuandika ulichoandika.
 
Juha kama hilo ni la kupuuzwa tu mkuu!!
 
20160308_175155.jpg

Sheikh Muhammad Bakari

Kila aliposimama kuzungumza watu walinasa maneno yake katika vinasa sauti
kama darsa tosha kusikizwa siku za usoni

Sheikh Muhammad Bakari amefariki usiku wa tarehe 26 Mfungu nane 1437 (sawa na tarehe 7 March 2016) na hadi kufikia afajir taarifa zikawa zimeshafika Tanga. Ghafla mji mzima ukawa umejiinamia. Mbuyu mkubwa ulikokuwa katikati ya mji uliokuwa ukitoa kivuli ulikuwa umeanguka. Sheikh Muhammad Bakari alikuwa mwanafuzi wa mwanazuoni mkubwa wa Afrika ya Mashariki na Kati marehemu Sheikh Muhammad Ayub muasisi wa Shamsiyya na mwalimu wa masheikh wengi.

Haukupita muda watu wakawa wamekusanyika uwanja wa ndege wa Tanga kusubiri mwili wa Sheikh Muhammad Bakari uliowasili majira ya saa nane. Tanga ilikuwa imeondokewa na msomi wake mkubwa ambae kabla ya kifo chake Sheikh Muhammad Ayub alipatapo kusema kuwa mwanafunzi wake Muhammad Bakari ni mwanazuoni.

Katika kumueleza Sheikh Muhammad Bakari Sheikh Suleiman Amrani Kilemile akizungumza kwenye msiba Dar es Salaam kabla ya mwili haujapelekwa uwanja wa ndege alisema kuwa Sheikh Muhammad Bakari kwao wao walipokuwa wanasoma kwa Sheikh Muhammad Ayub alikuwa ‘’kaka’’ na ‘’mwalimu.’’ Alimsifia Sheikh Muhammad Bakari kwa kusema kuwa alikuwa mtu wa subira ya hali ya juu wakati wa kusoma kwani wakati ule hali ilikuwa ngumu. Aliongeza na kusema kuwa Sheikh Muhammad Bakari alikuwa msomi wa sifa na alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kusoma vitabu. Akaendelea na kusema kuwa Sheikh Muhammad Bakari alikuwa na tabia ya kuweka sahihi yake kwenye kurasa ya mwisho ya kila kitabu alichomaliza kusoma.

Baada ya kifo cha Sheikh Muhammad Ayub Sheikh Muhammad Bakari alifundisha Shamsiyya kwa muda akishika nafasi ya mwalimu wake. Sheikh Muhammad Bakari aliondoka Shamsiyya na kwenda Magomeni kwenye msikiti mdogo na hapo akaendelea kusomesha chini ya taasisi yake mpya aliyoiita Shams Maarif akisaidiwa na walimu wachache waliomfuata kutoka Shamsiyya mmojawao akiwa Mwalimu Miraj na Sheikh Said Makata.

20160308_182002%252520%2525282%252529.jpg

Maalim Miraji

Hiki kilikuwa kipindi kigumu sana kwake na kwa wanafunzi waliomfuata kwani alijaza wanafunzi wengi katika mahali finyu. Watu wengi hawakupenda kuona hali ile lakini hawakuwa na la kufanya. Sheikh Muhammad Ayub aliendelea kusomaesha na mara kwa mara alikuwa akisema kuwa ile hali iliyokuwa ikimkabili katika kusomesha ilikuwa ni qadar ya Allah.

20160308_175301.jpg

Sheikh Muhammad Bakari katika uhai wake akihadhiri na wasikilizaji wakinasa
nasaha zake katika vinasa sauti

IMG-20160308-WA0206.jpg

Sheikh Muhammad Bakari akiozesha

20160308_164110.jpg

Kushoto Sharif Khitami na Sheikh Muhammad Bakari Nyuma ni Sharif
Mundhari Khitami siku ya ufunguzi wa Msikiti na Madrasa ya Shams Maarif

IMG-20160309-WA0112.jpg

Sheikh Muhammad Bakari Iddi Simba na Bakari Mwapachu siku ya ufunguzi

Kushoto Salim Bajaber, Sharif Khitami na Sheikh Muhammad Bakari
wakielekea msikitini kwenda kufanya ufunguzi wa msikiti na madras 2 May 2004

IMG-20160308-WA0188.jpg

IMG-20160308-WA0202.jpg

Kulia: Sheikh Muhammad Bakari, Salim Kisauji, Sheikh Muhammad Hariri
Mudir wa Maawal Islamiyya katika Maulid ya Bandari ya Tanga

IMG-20160308-WA0216%252520%2525281%252529.jpg

Umma ukiomba dua siku ya ufunguzi wa Msikiti na Madrasa ya Shams Maarif

IMG-20160309-WA0123.jpg

Katikati Salim Bajaber Meneja Mkuu wa Pembe Flour Mills Tanga

IMG-20160309-WA0126.jpg

Sheikh Alhad Omar akisoma Qur'an tukufu siku ya ufunguzi

20160308_172715.jpg

Kulia: Salim Bajaber wa Mombasa na Salim Bajaber wa Nairobi wakurugenzi
wa Pembe Flour Mills waliojenga msikiti na madrasa

DSCN0414.JPG

DSCN0416.JPG

Sheikh Salim Mtambo akiwa Uwanja wa Ndege akiratibu usafiri wa wazishi na maiti
kwenda Tanga

DSCN0415.JPG

Sheikh Burhani Bakari mdogo wa Sheikh Muhammad Bakari Uwanja wa
Ndege Dar es Salaam

IMG-20160309-WA0200.jpg

Mazikoni Duga

Umati uliojotokeza kumzika Sheikh Muhammad Bakari haujapatapo kuonekana Tanga. Barabara ya Mombasa ilifurika magari watu na waliokuwa wakitembea kwa miguu wakija Tanga mjini mazikoni. Vijiji vyote vya pembezoni mwa Tanga vilitoa watu walioingia mjini kwa maelfu.

Duga ilikuwa haiingiliki.

Screenshot_2016-03-09-23-12-01.jpg

Shams Maarif ilikuwa imezingirwa kila upande na wale waliopata nafasi ya kuingia msikitini ni wale ambao walifika pale asubuhi na mapema. Mji wa Tanga ulijiinamia.

Maziko haya yatazungumzwa kwa miaka mingi sana ijayo In Shaallah.
Kwa hakika haya maziko yamemueleza Sheikh Muhammad Bakari alikuwa nani.​

IMG-20160310-WA0127.jpg

Khitma

Maziko haya yamethibitisha kuwa silsila yake kama alivyopata kuieleza mwenyewe siku moja kuwa kapokea ilm kutoka kwa mwalimu wake Sheikh Muhammad Ayub na inakwenda nyuma hadi kufikia kwa Mtume SAW na kumalizikia kwa JIbril AS ambae alipokea kutoka kwa Allah SW.

IMG-20160310-WA0140.jpg

Ningependa kumaliza kwa kusema lini kwa mara ya kwanza nilipata kulisikia jina la Sheikh Muhammad Bakari.

Ilikuwa siku moja Msikiti wa Mtoro katika miaka ya 1970. Sheikh Kassim Juma alikuwa anamueleza Sheikh Muhammad Ayub.

Alipomaliza akaeleza maajabu aliyoyaona kwa Sheikh Muhammad Bakari.

Wakati ule Sheikh Muhammad Bakari alikuwa bado kijana mdogo mwanafunzi. Sheikh Kassim alisema kubwa aliloliona kwake Sheikh Muhammad Bakari ni ahklaki njema.

Kisha Sheikh Kassim Juma akaeleza umahiri wa Sheikh Muhammad Bakari katika ilm.

Ilipita miaka mingi hadi mimi kuja kujuana na Sheikh Muhammad Bakari wakati huo sasa Sheikh Muhammad Bakari alikuwa tayari ni sheikh na Mudir wa Shamsiyya chuo alichoasisi mwalimu wake Sheikh Muhammad Ayub.

IMG-20160308-WA0231.jpg

Kushoto: Sheikh Muhammad Hariri Mudir wa Maawal Islamiyya, Sheikh Muhammad
Bakari Mudir wa Shams Maarif na Mwandishi Tanga

Innalillah wainna illahyi rajiuun
 
Hapa ndio utawajua baadhi ya watu, kiongozi wao wa dini kafariki huwaoni hata waki comments, ngoja kwenye nyuzi za udini wanavyoporomosha kashfa na hata matusi. R.I.P Sheikh.
 
Hakika Tanga tumeondokewa na Mwanazuoni jamani. Sisi ni waja wake Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea. Pumzika Salama Sheikh. Hakika duniani tunapita jamani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom