Tanzia: Rais mstaafu Kikwete afiwa na dada yake

Tanzia: Rais mstaafu Kikwete afiwa na dada yake

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,092
Reaction score
7,236
Tunapenda kumpa pole Rais wetu mstaafu wa awamu ya nne , ndugu Jakaya Mrisho kikwete
kwa kufiwa na dada yake mpendwa Bibi Tausi Khalifani Kikwete kilichotokea huko India.

Pole sana Mh. Rais mstaafu Kikwete , tunakuombea kwa Allah akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu
wewe pamoja na familia yako yote. Watanzania na wananchi kwa ujumla tuko nawe katika msiba huu mzito.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA​
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU​
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 655"]
[TR]
[TD="width: 253"] Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
[/TD]
[TD="width: 118"]
​
[/TD]
[TD="width: 284"]
OFISI YA RAIS,​
IKULU, ​
1 BARABARA YA BARACK OBAMA, ​
11400 DAR ES SALAAM.​
Tanzania.​
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amepatwa na msiba mzito wa kufiwa na Dada yake Mpendwa Bi. Tausi Khalfan Kikwete kilichotokea jana tarehe 17 Desemba, 2015 huko nchini India.


Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema anaungana na familia ya Rais Mstaafu Kikwete katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mtu muhimu kwa familia."Kwa masikitiko makubwa nakupa pole nyingi Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa kufiwa na dada yako ambaye alikua nguzo muhimu katika familia" Amesema Rais Magufuli.


Aidha Rais Magufuli amemuomba Rais Mstaafu Kikwete kumfikishia salamu nyingi za pole kwa familia nzima na amewaomba wawe na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.Rais Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aipumzishe roho ya marehemu Tausi Khalfan Kikwete mahali pema peponi, Amina.


Imetolewa na;
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
18 Desemba, 2015

ms1.jpg
ms2.jpg
ms3.jpg
ms4.jpg
ms6.jpg
ms7.jpg
ms8.jpg
ms9.jpg
ms10.jpg
ms11.jpg
ms13.jpg
ms14.jpg
ms15.jpg
ms16.jpg
ms17.jpg
ms18.jpg
 
Pole sana Mh J Kikwete. Mungu akufanyie wepesi
 
Kaz yake maulana!! 😓😓😓
 
Pole Mh. Rais mstahafu, mwenyezi mungu awape nguvu wafiwa na aiweke roho ya marehemu bi Tausi mahala pema peponi - amina
 
Pole sana mheshimiwa Kikwete....


Mwenyezi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu...

sote tu njia moja...ni suala la muda tu kabla ya kurud kwake Muumba mbingu na nchi.
 
Dah kifo ndiyo mwisho wa kila kitu hakuna ujanja sote tutakwenda.

RIP.
 
Back
Top Bottom