Tanzia: Ofisa Ubalozi wa Tanzania nchi Malaysia Bi Apolonia Mwangosi afariki dunia

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
46,568
2,000
Afisa balozi Wa Tanzania nchini Malaysia APOLONILA MWANGOSI amefariki Hapohapo baada ya gariyake kuingia kwenye maji.

====

Ofisa Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia, Apolonia Mwangosi (46), amekufa papo hapo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutumbukia mtoni mjini Kuala Lumpar.

Mkuu wa Kituo Kikuu cha Usalama Barabarani cha Ampang, Malaysia, Hambazi Abdulrahman alisema ajali hiyo ilitokea juzi karibu na mgahawa katika eneo la Ampang Waterfront Food Court.

Abdulrahman alisema katika ajali hiyo iliyotokea saa 7.30 usiku, dereva wa gari hilo, Linus Okafor (35), raia wa Nigeria alipata majeraha kidogo.

Msemaji wa familia, Hagulwa Mbogo alisema mwili wa marehemu utawasili nchini kesho kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mindi Kisiga alithibitisha kuwapo taarifa za kifo hicho na kwamba, wizara inashirikiana na ubalozi wa Malaysia na familia ya marehemu kurejesha mwili kwa maziko.


Chanzo: Mwananchi
 

Borat69

JF-Expert Member
Jun 17, 2012
2,527
2,000
Apumzike kwa Amani dada Apolina. Kutokana na maelekezo hapo juu inabidi uchunguzi wa kina ufanyike ili kubaini Chanzo cha ajali...na huyo Dereva bwana Okafor ahojiwe vizuri. Huo muda wa ajali ulikuwa saa 7:30 usiku (1:30 am) au saa moja na nusu jioni (7:30pm)!?@Pdidy.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom