Tanzia: Nicola Colangelo mmiliki na muanzilishi wa kampuni ya Coastal Aviation afariki dunia

Mkuu haya ni maeneo au Airstrip zilizopo katikati ya pori la Selous
Huko ndio kuna Camps ambazo Malaya toka Dubai,Morroco,Italy na Uturuki hupelekwa na matajili,wanakula starehe,wanapandishwa ndege ndogo mpaka Dsm then wanakwea midege mikubwa kurudi kwao.

Kuna starehe na maisha ya anasa sana sana huko.Ukifika huwezi amini kama ni Tanzania


Duh!! ni kweli hii ni mpya sikuwahi kufikiria kama kuna starehe za hivyo mbugani Mkuu
 
Walaaaa hujakosea,ni vile tu huwa hatuwasemi vibaya marehemu.

Nafikiri kati ya watu wanaojua vichochoro vya tembo wa Selous na Ruaha,huyu alikuwa mmoja wao
Shukrani kwa kuliweka sawa jambo hili. Kuna watu wamekuwa mabilionea kwasababu ya Selous.
 
Nafahamu jamaa Anaitwa Julian Edmond mshenzi mshenzi fulani...yule wa Moshi Gills pia kimeo kimeo hasa, Auric wanakuja vzr sana...wanawakimbiza Coastal kwa route za Znz, Pemba, Mafia, Arusha, Tanga..vibaya sana..na mwaka huu wameanza kwenda polini..Kuondoka kwa huyu ni pigo mno kwa Coastal aisee.
Basi wewe upo kwenye Aviation ndani kabisa!!Mpaka Gills yule roho kimeo wamjua?
Huyo huyo Kaburu,hawa Auric ni wahindi fulani wa mwanza,wana kampuni ya utalii kama sikosei ya Dolphin kule Mwanza,hawa wana-take over sasa hivi kwa kasi yao.Wanaleta ndege latest sana kwa kusafiri na kutua maeneo korofi kama Jongomelo,Behobeho na Siwandu
 
Duh.sustainability ya business sijui inakaaje hapo.
Jamaa alikuwa na Viwanda vya tiles,boti za kwenda Zenji na Bongowe,kampuni ya ndege,hotel na Camps huko porini pamoja na magari ya watalii.

Kabla ya kufa,aliweka watu wake hasa ndugu kama wajomba kusimamia akiwepo mke wake Caroline.Siku za mwisho alipanga safu kwa ustadi mkubwa.Alikuwa na kansa ya utumbo,hivyo alijua kuwa siku zake si nyingi kuishi.Wazungu wanajipanga
 
View attachment 549472 View attachment 549473

View attachment 549474

Wakuu wana jukwaaa;
Kwenye sekta ya Aviation Tanzania kuna msiba mkubwa sana.Muanzilishi na mmiliki wa kampuni maarufu sana ya usafiri wa anga ya Coastal Aviation,Amicus Nicola Colangelo amefariki dunia.

Huyu ni mmoja wa wadau wakubwa sana wa "General Aviation" ambapo kampuni yake ilikuwa na zaidi ya ndege 30,nyingi aina ya Cesna206,Cesna 208 pamoja na Pilatus12(PC12) ambazo zilikuwa na "destinations" zaidi ya 42 Afrika Mashariki na Kati,huku makao yake makuu yakiwa Dsm.

Nicola ni mmoja wa wadau wakubwa sana wa usafiri wa anga na utalii,akiwa na ubia katika Hotel ya Slipway,Camps katika pori la Selous na Ruaha.Hakuna mtu aliyekuwa mtumiaji wa ndege ndogo za TB one kwenda maeneo yasiyofikika kwa barabara kama Kogatende,Behobeho,Siwandu,Likawage nk bila kutumia ndege hizi.

Nicola raia wa Italia aliyelowea Tanzania aliianzisha kampuni hiyo mwaka 1987 akiwa na ndege moja tu ndogo aina ya C206,akifanya safari zake kati ya Dsm na Selous Game Reserve.

Kwa sasa,Coastal Travel Safaris ndiyo moja kati ya kampuni kubwa za "Safari Tour".Ni bahati mbaya licha ya utajiri wote huo, Nicola amefariki bila kuwa na mtoto.

Sekta ya usafiri wa anga Tanzania, na huduma za mahoteli, watamkumbuka sana Nicola, mzee wa Coastal Steel pale Kipawa.

Binafsi nitamkumbuka Nicola, Mzungu janjajanja...
Pumzika kwa Amani Nicola...Uende salama!! Alama zako katika usafiri wa anga zitadumu kwa muda mrefu.

Acha uzushi Nicola anamtoto wa nje ya ndoa kademu ka half cast sema akili zake sio 100% sawa.. na hata mkewe alimkubali huyo binti japo mama wa binti hukomaa kuishi na bintie kwa sababu zake bibafsi
 
Acha uzushi Nicola anamtoto wa nje ya ndoa kademu ka half cast sema akili zake sio 100% sawa.. na hata mkewe alimkubali huyo binti japo mama wa binti hukomaa kuishi na bintie kwa sababu zake bibafsi
Huu ni mjadala mkuu,sio lazima uniiite muongo,unaweza kubatilisha pale nilipokosea kwa lugha ya staha tu
Kwa kumfahamu kwangu Nicola toka miaka ya 1990's sikuwahi kuwa na taarifa za mtoto,zaidi ya yule binti ambaye walikuwa wanagombea na rafiki yake wa Jongomelo kama ni mtoto wake,japo kila mtu alikuwa anasema ni wake

Hiyo yako ni mpya kwangu,inayonipa nafasi ya kujua zaidi.Najua kwa Caroline na kwingine,huyu mzee hakuwa na mtoto.Kama yupo,basi ndio unanipa mimi taarifa na wengine wengi wenye taarifa kama yangu ya hapo kabla
 
Back
Top Bottom