TANZIA: Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya (TFF) Hamidu Mbwazeleni amefariki dunia leo

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka nchini TFF, Hamidu Mbwazeleni amefariki dunia leo

Kufuatia msiba huo Rais wa TFF Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki pamoja na wanafamilia wa mpira wa miguu nchini.

Karia amesema Mbwezeleni alikuwa mwanamichezo mzuri ambaye amekuwa akishiriki shughuli mbalimbali za mpira wa miguu, mwenye uweledi katika shughuli zake mchapakazi hodari.

Ameongeza kuwa katika kipindi chote alichokuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo amefanya kazi kwa moyo wote wa kuutumikia mpira wa Tanzania.

IMG_20190116_192817_025.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rip mbwezeleni namkumbuka tu kwa hukumu zake ndan ya kamati ya MASAA 72 kaumiza watu vbaya nadhan wambura na dastan mkund wa mtwara hii kwao s habar ya HUZUN zaid ya furaha kwan wanajua walyopitia nadhan nayule wa yanga bwana BAKILI MAKELE naye n shangwe tu kwake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom