TANZIA: Mwenyekiti wa CHADEMA Iringa Vijijini, Sinkala, apata ajali na kufariki

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Iringa Vijijini Sinkala Mwenda amepata ajali jioni ya leo eneo la Tanangozi.

Amekimbizwa hospitali lakini kafariki dunia usiku huu.
c477cb46c861ef4f5dbded4a915542f0.jpg

Picha nyingine hazifai
watia nia.jpg

Lucas Sinkala Mwenda wakati wa uhai wake

Sinkala Mwenda alikua Mwanasheria Kijana Msomi wa CHADEMA. Mwenda alikuwa mgombea kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga 2014 ambaye aliwashinda wagombea wengine 12 katika kura za maoni ndani ya chama, alipokwa ushindi na chama hicho na kikamteua mshindi wa pili Grace Tendega kupeperusha bendera katika uchaguzi mdogo huo.

Kwa sasa alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Iringa Vijijini

 
RIP mwenyekiti, poleni wanachadema wa mkoa wa Iringa na Tanzania yote kwa ujumla
 
R.I.P kamanda, umetutangulia tupo nyuma yako.

Picha enzi za uhai wake tafadhali
 
Sisi ni mavumbi na mavumbini tutarejea....upumzike kwa amani mpambanaji....sisi tuliobaki na pumzi tunaendeleza mapambano ingawa ni jambo lenye kuvunja moyo kumpoteza kamanda kati kati ya mapambano lakini hatuna kuendelea na mapambano kwani ndio njia pekee ya kukuenzi.....
RIP....
 
Mungu ampe pumziko la milele. Msalimie kamanda Mawazo, mwambie sisi mapambano yanaendelea
 
Back
Top Bottom