Tanzia: Mwalimu Bahiya bint Abdulrahman

Kwahiyo huyo aliyejibiwa hivyo unafikiri ni Muislamu ?

Wakristo mna matatizo sana,yaani mnayaona ya wenzenu yenu hamyaoni,ndio maana sifa ya uadilfu huwa hamna.
Nimedili na aliyejibu si aliyejibiwa.

Uwe unaelewa.
 
Ningeweza kukujibu lakini kwa heshima na huzuni juu ya Msiba wa Huyo Marehemu Bibi na Mama yetu mpendwa pia heshima ya Mzee Mohamed Said aliyeleta huu Uzi, navuta Subira, na hapa ndipo nimepata jibu la ukafiri wako uliojinasibu kwamba unao, lugha zako zinatosha kukupambanua kwamba wewe sio tu ni kafiri mbobezi bali ni kiranja wao.

لعنة الله عليك
Ni kweli kabisa, lakini ni hekma kujibu swali
 
Azarel,
Taazia haishindaniwi huwa inasomwa na watu kubaki kimya kuchelea kumsema vibaya marehemu na hivyo kuwaumiza nduguze na waliompenda katika uhai wake.
Hujajibu swali, unaleta maelezo yasiyoendana na swali langu sheikh
 
Poleni sana! Sisi ni mavumbi na mavumbini tutarejea! Poleni sana
 
Ufunuo 14:13
13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
 
Mkuu!!!

Huyu anaweza kuwa sawa na Bibi yako au mama yako mpe heshima yake hata kama hukubaliani na mwandishi basi angalao onyesha heshima kwa huyu mama, laana siyo lazima akutamkie mzazi wako tunazipata kutokana na tunavyotumia viungo vyetu kuwasema wengine.

Wakristo hatujafunzwa hivyo ndugu yangu,nisamehe kwa kukurekebisha.


Mkuu, utawezaje kumjua mtu akiyetokana na kizazi kibaya na cha ZINAA (mwanaharamu)??, ni kupitia maneno na matendo yake ndipo utamjua na mbaya zaidi anatapika UVUNDO katika tanzia na anamtusi Marehemu, bila shaka huyo ni mwana wa Ubilisi.

Yesu, alisema; "kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara hakitapata--" (mathayo 16:4).
 
Mkuu, utawezaje kumjua mtu akiyetokana na kizazi kibaya na cha ZINAA (mwanaharamu)??, ni kupitia maneno na matendo yake ndipo utamjua na mbaya zaidi anatapika UVUNDO katika tanzia na anamtusi Marehemu, bila shaka huyo ni mwana wa Ubilisi.

Yesu, alisema; "kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara hakitapata--" (mathayo 16:4).
Sir...
Hakika nasikitika kuwa taazia hii ya mama yetu na mwalimu wetu aliyetufunza mengi mema pamoja na adabu amekuwa sababu ya Majlis kugeuzwa uwanja wa matusi.
 
Nimedili na aliyejibu si aliyejibiwa.

Uwe unaelewa.
Ndio uone wapi ulipokosea,kwa maana umekurupuka,laiti kama ungesoma alichokiandika aliye jibiwa usingeandika ujinga ulio uandika huko.
 
Hakika mzee Mohammed ni mtu ambae kweli unaijua dini... japo mimi ni mkristo lakini naomba niwe na hekima kama yako.. maana unakashfiwa, unatukanwa na maneno mbalimbali ya kejeli lakini mzee Mohammed sijawah kukuona unamjibu mtu kwa ghadhabu wala hasira, Mungu akuzidishie uheri mwingi ili tuendelee kufaidi hekima yako hapa duniani na Jf.

Umenisaidia maneno yangu pia....atakuwa mzee mwenye subra sana....
 
mie sikuelewa kuwa ni Tanzia maana imerepotiwa kama taazia basi kiswahili kinapaa
 
Sir...
Hakika nasikitika kuwa taazia hii ya mama yetu na mwalimu wetu aliyetufunza mengi mema pamoja na adabu amekuwa sababu ya Majlis kugeuzwa uwanja wa matusi.


Sir, mimi naomba unisamehe sana kwani ninashindwa kujizuia kabisa kuwajibu.
 
Mr Chopa,
Umefanya sivyo kumtukana.

Siwezi kukuhukumu lakini nadhani umeghadhibishwa na kule kuona kama vila kamdharau marehemu.

Si kitu.

Lakini kwako ilikuwa ni kumfahamisha kuwa marehemu alikuwa mama na mwalimu wetu ambae mfanowe haujapata kutokea Dar es Salaam na iitachukua miaka mingi kutokea mwalimu kama Bi. Bahia kwani ana wanafunzi katika familia moja kuanzia mume na mkewe na watoto wao na familia nzima wakawa wamesomeshwa Qur'an na yeye tofauti ikiwa ni miaka tu.

Baba na mama wamesomeshwa miaka ya 1950 na watoto miaka ya 1980 na wajukuu miaka ya 2000.

Madrasa ni ile ile na mwalimu ni yule yule na akisomesha bure.

Mwalimu Bahia ana wanafunzi kila pande ya dunia kuanzia Arabuni, Ulaya na Marekani.
Rambirambi nyingi zimepokelewa kutoka kwa wanafunzi wake kila pembe ya dunia na sasa hawa wanafunzi ni watu wazima na wamestaafu kazi.

Hakuna mtu aliyezaliwa Dar es Salaam ile ya 1950s na akakulia katika mazingira yale ambae hakuwa anamjua Mwalimu Bahia.

Mwalimu Bahia alikuwa anaingia katika nyumba za wakazi wa Kariakoo na kwengineko ama kwenye maulid au hakika ya mtoto au kwenye kufiwa.

Bi. Chiku mjukuu wa Bi. Chiku bint Said Kisusa kanitumia ujumbe ananambia kuwa, ''Mwalimu Bahia alikwenda hija na bibi yangu na waliporudi Mwalimu Bahia alikuja nyumbani kuniletea maji ya Zam Zam.

Kabla ya kunipa kunywa alinisomea dua ndefu sana na siku zote nikimpigia simu kuwa naumwa haipiti dakika teksi ishasimama nje ya nyumba yangu anakuja kunitazama basi hapo atanifanyia dua kisha ndiyo aniage.''

(Bi. Chiku bint Said Kisusa nimeweka paicha yake hapa akiwa uwanja wa ndege yeye na Bi, Tatu bint Mzee na Bi. Titi Mohamed wakimsindikiza Mwalimu Nyerere safari ya kwanza UNO 1955).

Hivi kwa mukhtasari hivi ndivyo alivyokuwa Mwalimu Bahia hadi umauti ulivyomfika.

Ndugu yetu hakuwa anamjua mwalimu na mama yetu Bi. Bahia na ndiyo fedhuli na dharau ile.

Tusimlaumu kwani Dar es Salaam ile si hii ya leo na si kila mtu kapitia malezi tuliyofunzwa sisi ya kuwa na subra, staha kwa umjuaye na usiyemjua.
Ndugu Mohamed tunapishana imani lakini najifunza "utu" sana kutoka kwako!
 
Back
Top Bottom