Tanzia: Mchungaji wa KKKT Usharika wa Sinza afariki Dunia kwa ajali

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,636
37,850
Wapendwa,

Tumeondokewa na Mchungaji wetu wa kanisa la KKKT Kigamboni ambaye kabla ya hapo alikuwa KKKT usharika wa Sinza.

Amepata ajali mbaya jana usiku akiwa anatokea Mbagala kurudi kwake Kigamboni. Gari ilipinduka na yeye kupoteza maisha hapo hapo.

Habari kamili itafuatia.......

Poleni sana Ndugu, Jamaa, Marafiki na Hususani waumini wa kanisa la KKKT magogoni - Kigamboni.

Bwana alitoa.......Bwana ametwaa.....Jina la Bwana lihimidiwe.....
 
Mi Nilidhani hawa wachungaji wapo karibu na mungu muda wote na malaika wa bwana wanawalinda muda wote wasidhurike, kumbe kama sisi tu. R. I. P mchungaji
 
Wapendwa,

Tumeondokewa na Mchungaji wetu wa kanisa la KKKT Kigamboni ambaye kabla ya hapo alikuwa KKKT usharika wa Sinza.

Amepata ajali mbaya jana usiku akiwa anatokea Mbagala kurudi kwake Kigamboni. Gari ilipinduka na yeye kupoteza maisha hapo hapo.

Habari kamili itafuatia.......

Poleni sana Ndugu, Jamaa, Marafiki na Hususani waumini kwa wa kanisa la KKKT magogoni - Kigamboni.

Bwana alitoa.......Bwana ametwaa.....Jina la Bwana lihimidiwe.....
Mungu aipumzishe Roho yake mahali pema peponi. Amen

Ungemtaja kwa jina ingependeza zaidi
 
Mungu awape faraja.
hakuna kitu huwa kinanichanganya kama mtumishi wa Mungu kufa kwa Ajali.
wakati watumishi wengine wengi kwenye bibilia waliokolewa kwenye ajali.
Hata sisi tulimpoteza mchungaji kwenye ajali, akafa peke yake abiri wengine wakapona.
 
Ni Jumapili iliyopita tu, tulikuwa naye kanisani, alikaa na sisi waumini kwani Ibada iliongozwa na viongozi kina mama kuadhimisha siku ya wanawake duniani, alipata muda kidogo tu wa kusalimia waumini, alivyosimama tu na ile suti yake kali ushairika wote ulilipuka kwa vifijo na nderemo, maskini kumbe ndiyo tulikuwa tunamuaga mchungaji wetu. RIP.

Kweli haya maisha ya duniani, tunaambiwa kila wakati tuwe tayari kwa safari ya milele...
 
Back
Top Bottom