TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia

yekini

Senior Member
Jan 11, 2015
144
91
AB41731D-32F5-49E3-AEB9-C6044780CDED.jpeg


TAARIFA YA AWALI:


Wadau nimepata taarifa muda huu zinasema mbunge wa Songea mjini Mh. Leonidas Gama hatunaye tena....

UPDATE:

JamiiForums imepata uthibitisho wa taarifa za kifo cha Mhe. Gama ambacho kinadaiwa kutokea muda wa Saa 6 kuelekea Saa 7 usiku wa kuamkia leo.

Amefariki akiwa mbunge wa Songea Mjini na amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii Songea katika Hospitali ya Peramiho.

Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Inadaiwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu; akapooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa na akapelekwa Hospitali ya Peramiho ambako aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi.

========

Updates
Chama cha Mapinduzi chatuma salama za rambirambi kwa familia

chichiem.jpg


05663017-8D84-4EC0-8177-1E5092CD733B.jpeg

67938F42-36E6-42F0-AB45-31DA208EEE34.jpeg
 
Back
Top Bottom