RIP Kasongo Mpinda "Clayton".
Mara ya mwisho nionana na Kasongo Sigara Club sikumbuki mwaka gani alikuwa ameambatana na Marehemu Ndala Kasheba nakumbuka Ndalla alikuwa na gita baridi (gallatin guitar) kwa pamoja wakapiga nyimbo za zamani za OSS & Maquiz ukweli siku hiyo nilifurahi sana.
Marehemu Kasongo ni mwanamuziki mkubwa sana hakuwa na maringo hasa ukitilia maanani kazi yake kubwa aliyoifanya akiwa na Maquiz ,MK Group Zaita Musika na baadae wazee Sugu.Kati ya nyimbo za Kasongo amabazo mpaka leo ukizisikiliza utaburudika ni Baharia akiwa na Maquiz na Maumivu makali akiwa na MK Group gita la solo likicharazwa na marehemu Joseph Mulenga raia wa Zambia amabae pia aliwahi kupigia band za Mlimani Park & Bima Lee.Saxaphone zikipulizwa na Mafumu Bilal Bombenga,tumba zikipigw kwa umahiri mkubwa na Sidy Morris na gita zito alikuwepo Ambasodor Andy Swebe shughuli wakati huo ilikuwa kubwa kweli kweli Wazee wa ngoma za maghorofani New Afrika Hotel.Nakumbuka kila nikienda Dar Mk Group ilikuwa chaguo langu.
Mzee Kasongo Mungu akufanyie wepesi wasalimie Supreme Maestro Ndalla Kasheba,Joseph Mulenga,Rahma Shally,Dr Remmy Ongalla,Kasaloo Kyanga,Kyanga Songa,Masia Radi,Muhidin Maalim Gurumo,TX Moshi William na wengine wote waliotangulia mbele za haki.
Wimbo wako Maumivu makali nikirejea nyumbani leo nitaucheza kama sehemu ya kuenzi mchango wako mkubwa katika tasnia ya Muziki wa dansi.Bila shaka Rajab Zomboko na kipindi chake cha hizi nazo siku ya Ijumaa atatupatia wasikilizaji wake nafasi ya kumfahamu zaidi Kasongo Mpinda Clayton.
RIP Kasongo Mpinda Clayton.